Mariam Lukandamila (kulia), mkazi wa Kipawa, Jijini Dar es Salaam, akipokea hundi yake ya Sh. milioni 21 kutoka kwa afisa Malipo, Simon Chuwa, kama fidia ya nyumba yake iliyovunjwa kupisha ujenzi wa uwanja wa Ndege wa kimataifa ya Julius Nyerere.
<style type="text/css"> <!-- @page { margin: 0.79in } P { margin-bottom: 0.08in } --> </style>
Ulipaji fidia kwa wakazi wa Kipawa, jijini Dar es Salaam waliovunjiwa nyumba zao kupisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, ulianza jana.
Ulipaji fidia huo ulifanyika jana katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kwa kutumia hundi zilizotolewa kwa wakazi hao wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 200.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa iliyoko chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Edgar Japhet, alisema mchakato wa ulipaji fidia ulifanyika vizuri licha ya kuwepo kasoro ndogo ndogo.
Japhet alisema kasoro zilizojitokeza katika kutoa hundi ya malipo ni baadhi ya watu kutambulika kwa majina tofauti, kama yalivyoonekana kwenye kitambulisho huku jina la mmiliki wa kiwanja likiwa jingine.
Naye Mwenyekiti wa wenye nyumba zilizovunjwa, Magnius Bulisa, alisema hawajaridhika na malipo yanayotolewa na serikali kwa madai kwamba hayalingani na thamani ya nyumba.