Serikali inajitahidi Kufanya Mema

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
pokea.jpg

Mariam Lukandamila (kulia), mkazi wa Kipawa, Jijini Dar es Salaam, akipokea hundi yake ya Sh. milioni 21 kutoka kwa afisa Malipo, Simon Chuwa, kama fidia ya nyumba yake iliyovunjwa kupisha ujenzi wa uwanja wa Ndege wa kimataifa ya Julius Nyerere.
 
pokea%281%29.jpg

Mariam Lukandamila (kulia), mkazi wa Kipawa, Jijini Dar es Salaam, akipokea hundi yake ya Sh. milioni 21 kutoka kwa afisa Malipo, Simon Chuwa, kama fidia ya nyumba yake iliyovunjwa kupisha ujenzi wa uwanja wa Ndege wa kimataifa ya Julius Nyerere.


<style type="text/css"> <!-- @page { margin: 0.79in } P { margin-bottom: 0.08in } --> </style>
Ulipaji fidia kwa wakazi wa Kipawa, jijini Dar es Salaam waliovunjiwa nyumba zao kupisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, ulianza jana.
Ulipaji fidia huo ulifanyika jana katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kwa kutumia hundi zilizotolewa kwa wakazi hao wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 200.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa iliyoko chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Edgar Japhet, alisema mchakato wa ulipaji fidia ulifanyika vizuri licha ya kuwepo kasoro ndogo ndogo.
Japhet alisema kasoro zilizojitokeza katika kutoa hundi ya malipo ni baadhi ya watu kutambulika kwa majina tofauti, kama yalivyoonekana kwenye kitambulisho huku jina la mmiliki wa kiwanja likiwa jingine.
Naye Mwenyekiti wa wenye nyumba zilizovunjwa, Magnius Bulisa, alisema hawajaridhika na malipo yanayotolewa na serikali kwa madai kwamba hayalingani na thamani ya nyumba.
 
huyo Bibi anahitaji mtu mwaminifu wa kumsaidia jinsi ya ku-control hiyo pesa otherwise wajanja wataifaidi sana na yeye kuambulia patupu. Inabidi kabla serikali haijawavunjia watu nyumba iwe inawapa elimu ya kisaikolojia na ushauri wa matumizi bora ya pesa zao ili kuwasaidia kuepukana na janga la kutumia pesa yote pasipo faida
 
Back
Top Bottom