Peter Mwaihola
JF-Expert Member
- Jun 23, 2022
- 289
- 489
Rais wa Taifa la Marekani Joe Biden ametangaza Msamaha wa kiasi cha dolla 10,000 za kimarekani kwa wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu wenye kipato cha chini na cha Kati.
Uamuzi huo unalenga kutoa nafuu ya maisha kwa wananchi wa Hali ya Kati na ya chini ambao walisomeshwa kwa mkopo wa Serikali ya shirikisho la marekani.
Biden alibainisha kuwa msamaha huo utakuwa chachu kwa wananchi kupambana na ugumu wa maisha ya ajira zao na kuwapa nafasi ya kutumia mishahara yao vizuri.
Kupitia Kurasa zake za mitandao ya kijamii Biden amechapisha ujumbe alioupata kutoka kwa mwanamke mmoja ambae alimwandikia ili kumpongeza kwa hatua hiyo ya kutoa msamaha.
"Mimi na mume wangu wote ni waalimu, kwa msamaha huu wa deni Sasa tunaweza kuishi mwezi hadi mwezi kwa kujiamini na kuanzisha familia, deni hili lilikua linaturudisha nyuma Asante Rais Biden" alihitimisha mwanamke huyo mdogo.
Kitendo hiki kimewagusa wananchi wa Marekani kwa ujumla sio tu wale wa kipato cha chini bali hata wale wa kipato cha juu ambao hawanufaiki na msamaha huo.
Wakati hayo yanaendelea huko nchini Marekani kwa Tanzania mambo ni tofauti malalamiko kuhusu tozo za Miamala ya simu na benki yameteka vijiwe na mitandao ya kijamii.
Serikali inajaribu kutoa ufafanuzi lakini hauonekani kuwa na mashiko kwa raia walio wengi isipokuwa Viongozi wenye dhamana ya serikali kuu.
Suala la tozo limekua gumzo kwa mwaka wa pili mfululizo licha ya serikali kuongeza mshahara kwa watumishi wa kiima cha chini lakini bado chumvi ya tozo inatiririka kwenye kidonda kuamsha malalamiko.
Je serikali yetu inajifunza nini kuhusu maisha ya watu wa chini?
Peter Mwaihola ni Mwandishi wa habari na Mchambuzi wa masuala ya Siasa na jamii.