Serikali Inahusika kwenye Kughushi vyeti - wazo

mandokwa

JF-Expert Member
Jun 5, 2013
620
865
Wakuu nawasalimu wote....Nashukuru nipo salama na cheti changu safiii mimi ni halali sio wakughushi....

Napenda kutoa hoja ambayo wenye akili waipime juu ya huu mchakato wa vyeti feki. Ni aibu kwamba idadi kubwa ya wadau wameumbuka na kuathirika katika huu mchakato...hoja zangu hapa ni mbili:

1. Serikali kwa muda mrefu imekuwa ikiwanyima kuwapa vyeti wahitimu wa form iv na vi ambao hawakufaulu vizuri. Hili jambo kwa mtazamo wangu limechangia kughushi vyeti kwani wengi wanaoghushi ni katika kundi ambalo physically walisoma na kumaliza elimu husika but wakakosa kupata cheti... swala la kulifahamu ni kwamba hatakama hawa ndugu hupewa vyeti vya living na shule husika, vyeti vile havitambuliwi kitaifa na kupelekea mtu kupoteza sifa yakuwa mhitimu wa level husika. jiulize kwanini wasipewe wakati wamehitimu? kwani kuna ubaya gani ukampatia lakini ni daraja likawa zero?

Mantiki ya kutaka hawa jamaa wapewe vyeti ni kwamba mara nyingi kwenye ajira kama uhudumu, udereva nakadhalika unachotakiwa ni utambulisho tu kwamba umehitimu form iv na sio watokeo ya ulipata grade gani... kwamaana mtu kama driver tayari anakuwa amepata leseni ya udereva ambayo ndio msingi na pia anaweza kusoma, kuandika na kuhesabu kiasi kwamba hawi mzigo.... kuna tofauti kubwa sana kati ya kufika form iv ukapata zero na kuishia darasa la saba ndio maana hawa jamaa lazima tuwape haki ya msingi...

2. Hoja yangu ya pili ni kwamba serikali kupitia kanuni zake za utumishi, pale ambapo mtumishi akisha ajiriwa, hupewa mwaka mmoja wa kuangaliwa kabla hajapewa ajira kamili. maafisa rasilimali watu na mabosi wao wanapaswa kumkagua huyu muarijiwa ikiwemo kucheck records za vyeti vyake.. so uwepo wa wafanyakazi 9000 + wasio na vyeti halali naiona ni masive failure ya hawa HRs... kwanini serikali isiwatumbue hawa waliosababisha tatizo kupitia negligence? naamini wakitumbuliwa tutajenga nidhamu ya kazi ambayo itahakikisha mbeleni haya mambo hayajirudiii

regards,

Nangu mandokwa
 
Back
Top Bottom