Serikali inacheza na swala hili! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali inacheza na swala hili!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zipuwawa, Jul 1, 2012.

 1. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Je Kama kweli Serikali imedhamilia kuleta madaktari wa kigeni kuchukua nafasi ya hawa waliogoma kutokana na mazingira magumu ikiwemo maslai duni na kutokuwepo kwa vifaa mbalimbali hosp. Je kama Hao Madaktari kutoka nje ya nchi watakuja na vifaa?
  Je Wauguzi watakubali kushirikiana nao? kwani wauguzi katika mgomo wa kwanza walipelekwa Madaktari wa Jeshi la Wananchi lakini Wauuguzi walionekana kutokukubali kitendo hicho. Je Wauguzi watakubali kushirikiana nao? Au ndio serikali inatafuta mgomo mwingine? Je itaweza tena kutafuta wauguzi kutoka nje ya nchi? Maswali haya yanapaswa kujibiwa na serikali ambayo inapanga mipango yake bila kuangalia matokeo ya baadae! Sio haja ya serikali kuendelea kulaumiwa kwa maamuzi mabovu.

  Ni sielewi wanaopanga haya mambo wanafikiria nini? Na Je Hao madaktari wanautaalamu gani au kwakuwa watanzania ni vichwa vya wandawazimu basi tuwe watu wa majaribio kwa miili yetu. Mi sikubaliani kabisa na madaktari kutoka nje kuja kutupoka maisha yetu.
   
Loading...