Field80,
sidhani kama unaifahamu Afrika Kusini, na kama unaifahamu labda majina ya miji tu! Hivi unajua ubalozi wa Tanzania uko wapi? Uko Pretoria, mtu wa Cape Town, Durban - (KwaZulu Natal, Pietmarziburg, New Castle, nk) au Mpumalanga, Limpopo, au Western cape atafikaje huko pretoria!! Hivi wewe unajua kweli Afrika Kusini, au umekaa hapo Mikindani, Mtwara unafikiri nchi zote ziko hivyo!
Watanzania hawataki msaada wowote kwasasa, BALI tamko rasmi la serikali dhidi ya raia wake wa Afrika Kusini, na hata ikiwezekana kushinikiza serikali ya Afrika Kusini tuzuia machafuko zaidi! Mbona tumekuwa tukitoa maonyo kwa Burundi, DRC, ... why not Afrika Kusini? Rais Mbeki yuko nchini Tanzania, Makamu wake yuko Nigeria, wote hawa wamefunga midomo (kama Ben Mkapa) hawataki kuzungumzia machafuko! Ni zamu ya serikali kuwakaripia kwa hili, kwani wanaokufa ni raia wa TZ, na pia inajenga uhasama ndani ya Afrika kwa waafrika wenyewe! Utajisikiaje ukisikia Mozambique wameaanza kupiga raia wasioongea kireno!!