Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,395
- 39,531
Kwa siku kadhaa sasa machafuko dhidi ya wahamiaji yamepamba moto huko Afrika ya Kusini. Hadi hivi sasa wananchi wa nchi kadhaa za Kiafrika wameuawa na idadi yao imefikia karibu 40 hivi. Miongonni mwa wanaodaiwa kuuwa ni pamoja na raia 6 wa Tanzania walioko Bondeni.
Hata hivyo ikiwa imetingwa na mambo mengine serikali yetu haijatoa msimamo wowote au juhudi zozote zinazoeleweka kuhusu kuhakikisha usalama wa wananchi wetu uko Afrika ya Kusini.
Hofu yangu ni kuwa wakati Serikali inataka watanzania walioko nje ya nchi wachangie maendeleo ya nyumbani kwa kutuma fedha, kuwakeza na hata kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo, inaonekana hamu yao inaishia hapo tu.
Serikali haina mpango wowote au sera yoyote inayoeleweka ya kuwa mtetezi wa raia wake walioko nje ya nchi. Mara kadhaa sasa watanzania wanapata matatizo nje ya nchi na serikali yetu aidha inafunga kinywa au inakuwa na attitude "si mliondoka Tanzania" au kuwaona kuwa watanzania walioko nje ya nchi ni nusu raia au wana haki kidogoo na hawana protection yoyote ya State.
Pendekezo:
Serikali ya Tanzania yenye madege makubwa ya kutosha iandae ndege kwenda Afrika ya Kusini na kumchukua Mtanzania yoyote anayetaka kurudi nyumbani. Hili linawezekana na si gumu. Serikali pia ioneshe kujali raia wake isiwafanye kama ilivyowafanyia vijana wetu kule Ukraine au ilivyojifanya imesahau suala la vijana wetu waliouawa hapa US. Serikali yetu isifumbie macho kama inavyofumbia macho suala la kijana Fupi ambaye amewekwa kwenye kundi la Maghaidi uko Guantanamo.