Serikali imulike kivuko cha Kamanga Ferry Ltd

NUMAN

JF-Expert Member
Sep 3, 2019
614
831
Binafsi naamini katika kuchukua tahadhari kabla ya hatari kitokea.Hali iliyopo ni mbaya sana naamini hatua stahiki bado hazijachukuliwa. Abiria ni wengi sana na ferry inajaa sana. Hii ni baada ya ferry ya Kitana kusimama kutokana na kufanyiwa figisu.

Awali ferry ya Kitana ulikuwa inatia nanga eneo la karibu na Mjini ila baadae ilitolewa na kupelekwa mbali na Mjini hivyo abiria wengi kuona bora wapande Kamanga Ferry Ltd. Hali hii imepelekea jamaa abaki mwenyewe bila ikiwa na mpinzani hivyo kupelekea abiria kujaa kupita kiasi.

Naamini juu ni muda muafaka kwa Serikali kutipia macho kivuko hiki kabla hakijaleta madhara kama ya MV Nyerere huko Ukara.

Vilevile katika kipindi hiki ambapo tunapambana na Corona. Kumbuka hili ndio lango la kuingia watu wa nchi jirani Rwanda, Burundi na Uganda. Hivyo tahadhari inahitajika mno.
 
Cheki hapo ni pa kisubiria abiria yaani ni shida. ...ugonjwa ukija ni shida tupu
IMG_24032020_100030.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kifupi feri zote upande wa Kamanga hazina uwezo wa kuhimili ziwa likichafuka hii inatokana na feri hizo kujengwa au kutengenezwa kishamba hasa kuzijenga kwa kwenda juu huku mkao wake ukiwa mwembamba. Kama huniamini rejea feri za Busisi au boti za Azam zinazoenda Zanzibar

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom