Serikali imewatega wabunge na wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali imewatega wabunge na wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Apr 21, 2012.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Apr 21, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Pamoja na tuhuma zote zilizoibuliwa kuhusu ubadirifu na matumizi mabaya ya madaraka kwa baadhi ya mawaziri, imeonekana dhahiri hakuna hatua zitakazochukuliwa dhidi ya watuhumiwa wakuu ambao ni mawaziri.
  Mawaziri kwa upande wao inaonekana wameitunishia misuli serikali, kwamba hawako tayari kuwajibika.
  Inaonekana pia madudu yote yaliyofanyika yanaonekana ni ngeni mbele ya bunge, lakini siyo ngeni mbele ya Rais na serikali yake.
  Kilichoonyeshwa na waziri mkuu ambaye ni kiongozi wa shughuli za serikali kwa kutokuchukua hatua ni udhaifu mkubwa mbele ya watanzania. Ni katika mazingira haya ambayo kila mtanzania mzalendo aliyekereka na wizi mkubwa uliofanywa na watendaji wa serikali kuachwa mdomo wazi baada ya waziri mkuu kushindwa kuwajibika.
  Sote tunafahamu kuwa waziri mkuu hana madaraka ya kumwondoa mteule wa rais. Lakini kama kweli waziri wetu mkuu kama mbunge na kama waziri mkuu naye ameguswa na wizi mkubwa namna hii, alitakiwa kufanya kile ambacho kiko kwenye uwezo wake, ambayo ni kuachia ngazi badala ya kulialia mbele ya wabunge.

  Waziri mkuu amewatega wabunge pamoja na wananchi waliokereka na huu ujambazi uliofanywa na watendaji wa serikali.
  Serikali imetega wabunge waliokereka kwa kutochukua hatua za dhati za uwajibikaji, kuona nini kitatokea endapo kama haitachukua hatua. Serikali ilichokifanya ni kuweka ahadi feki kusema kuwa waziri mkuu atatoa tamko la maamuzi ya serikali dhidi ya tuhuma zilizotolewa kwa mawaziri wake.
  Ninachokiona ni kwamba hii game ya serikali itachezwa bila mtu kuwajibishwa, kutokana na baadhi ya mawaziri waliotuhumiwa kusema wao wakimwaga mboga na sisi tunamwaga ugali.

  Hatari kwa afya ya Tanzania
  Hatari kwa afya ya wazalendo

  Imefikia wakati ambao watanzania hawatakuwa na uwoga na mabomu ya machozi, maji yanayowasha, na wapo tayari kufa kwa ajili ya haki au kufungwa kwa uonevu kwa kutetea haki yao.

  Mungu Ibariki Tanzania ya watu waliostaarabika, wapole, wanyenyekevu, wakarimu, wenye huruma, lakini siyo wanyonge.
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ngoma ikipigwa sana ikalia... ikalia.. ikalia..mwishowe hupasuka
   
 3. Kikarara78

  Kikarara78 JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,161
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Mungi na Wana JF,
  Unajua wahenga walisema Ukila na Kipofu usimwekeee mifupa sana, mwishowe nae kipofu atajua tu. Tatizo Kubwa la Watanzania ni huu Ugumu wa Maisha na Watawala wasiojali Misingi ya Sheria na kuilinda na kuifuata katiba ya Nchi.
  Mwisho wa udhalimu waja.
  Nawakilisha   
 4. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,320
  Likes Received: 840
  Trophy Points: 280
  Huyu mtoto wa mkulima angeachia ngazi mwenyewe, kama ulivyosema Mungi hakuna kitu serikali itawafanya hawa mawaziri kwa sababu huwezi kata tawi ulilokalia mwenyewe, utaonekana ni mwendawazimu.

  JK na hao mawaziri wake ni wale wale tu waizi. hakuna aliye nafuu wala afadhali.Pinda kaa pembeni acha kulia lia.
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Apr 21, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Ni kweli kwamba kujiuzulu kwake kusingebadilisha chochote, lakini kwa upande mwingine ingeonyesha kuwa serikali inawajibika mbele ya wananchi.
  Nakumbuka miaka ya 80 Mwinyi aliwahi kujiuzulu baada ya mauaji ya wakwongwe kule shinyanga, na haikumaanisha kuwa yale mauaji yaliisha, bali Mwinyi mwenyewe alikereka na yale mauaji.
  Hivyo kama waziri mkuu ameguswa na ule wizi, alitakiwa kuchukua hatua kuonyesha kuwa serikali inawajibika, na kuonyesha matumaini kwa wananchi.
  Haya mambo yangefanyika wakati wa mr white head nadhani angetoa tamko. Tatizo Pinda yupo kama remote hana maamuzi yoyote.
   
Loading...