Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,181
Mheshimiwa Damian Lubuva mwenyekiti wa NEC (sasa ni mstaafu) alitoa mapendekezo serikalini ya Tume ya Uchaguzi kutengana na wakala wake wa uchaguzi ambaye ni serikali ya mitaa kusimamia na kuratibu chaguzi zetu ili NEC iwe huru na chaguzi ziwe huru na za haki.
Serikali imeyakalia mapendekezo tajwa hadi uchaguzi mkuu wa 2020 upite na NEC wameuchapa usingizi mwororo pengine kwa kuhofia kutumbuliwa na huu utawala ambao unaendeshwa kwa misingi ya shuruti na kukomoana.
Uwakala wa serikali za mitaa umekuwa ni kichocheo kikubwa cha chaguzi zetu kutokuwa za huru au haki.
Ukianzia ujazaji wa fomu za udiwani na hususani ubunge, uwakala wa serikali za mitaa umechangia sana kufuta baadhi ya wagombea wa upinzani kwa madai batili ya hati za viapo zina dosari wakati hakuna. Waathirika wa maamuzi ya wakala tajwa huwa ni wapinzani na wanapokata rufani huibuka videdea na kuthibitisha wakala ni kada wa CCM.
Unapokuja uchaguzi mkuu wakurugenzi wa Halmashauri hugeuka na kuwa wasimamizi wa chaguzi na kubatilisha uhalali wa baadhi ya matokeo ya chaguzi.
Kesi nyingi za wapinzani mahakama kuu ni za kulalamikia kutoheshimiwa kwa matokeo yaliyokusanywa kwenye fomu za uchaguzi. Baadhi ya wakurugenzi hutamka matokeo ya uchaguzi ambayo hayana uhusiano na hesabu za kura kwenye fomu husika!
Haya ni mapungufu makubwa ya chaguzi zetu na ndiyo maana Mheshimiwa Jaji mstaafu Damian Lubuva alipendekeza mwiba serikalini wa kuiondoa serikali wa mitaa kama wakala wa NEC na hivyo kuajiri watumishi wake wa kudumu na kuondoa chemuchemu za ufedhuli.
NEC hadi leo haina mkakati wala nia ya kuandikisha wapigakura wapya kila siku kama RITA wanavyotekeleza majukumu yao.
Kila siku wapo vijana wanafikisha umri wa miaka 18 lakini haki yao ya kikatiba hunyimwa ya kuandikisha siku ile ile waliyofikisha umri tajwa kama ni siku ya kazi.
Kwa kuelewa vijana wengi wako upinzani mazingira magumu yamejengwa ya kuwaandikisha kwa malengo ya kuwakatisha tamaa wasijandikishe na kupunguza idadi za kura za wapinzani kwenye sanduku la kura.
Hakuna sababu za kimsingi kwanini NEC hawaandikishi wapiga kura kila siku ya kazi kama RITA wanavyotekeleza majukumu yao.
Kama NEC hawataki au hawezi kazi ya kuandikisha wapigakura kila siku ya kazi ni vyema jukumu hilo akapewa RITA ambaye yuko fiti na anaweza kulisawazisha daftari la wapigakura kwani anazo takwimu zote za uzazi na vifo.
Ninaomba kuwakilisha mada...