Serikali imesitisha ajira zote na nyongeza za mishahara nchini

Samahani jamani hivi ni kweli kwamba hata kama ulishafanyiwa promotion kabla ya huo walaka let say miez minne nyuma, basi mshahara unashushwa yaan unarud ulipotoka. Je habari hii ni kweli? Naomba ufafanuzi kwa anayejua
 
SERIKALI imesitisha ajira zote, kama njia ya kukabiliana na wimbi la watumishi hewa.

Kutokana na uamuzi huo hivi sasa hakuna nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa Serikali na wakala zake pamoja na utoaji wa vibali wa likizo ya bila malipo.

Akizungumza na MTANZANIA jana jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu Utumishi, Dk. Laurean Ndumbaro, alisema kuwa Serikali imesitisha kwa muda utoaji wa ajira, ili kupitia upya muundo wa Serikali na taasisi zake.

Alisema utekelezaji wa mkakati huo utakwenda sambamba na kusitisha kwa muda utoaji wa vibali vya ajira zote mbadala pamoja na uidhinishaji wa ajira hizo zilizopo Sekreterieti ya Ajira katika utumishi wa umma na kwenye mfumo wa taarifa za kiutumishi.

“Ni kweli tumesitisha kwa muda ili kupitia mfumo wa Serikali na hata kuangalia ulipaji wa mishahara kama upo katika malipo stahiki.

“…na hili litakwenda sambamba na hata kusitishwa malipo ya mishahara yanayotokana na upandishwaji wa vyeo kwa watumishi. Tukimaliza zoezi hili ndipo tunaweza kuanza kutoa ajira za Serikali,” alisema Dk. Ndumbaro.

Alisema muundo mpya wa utumishi wa Serikali unakwenda sambamba na uhakiki wa malipo ya mishahara, hivyo ni lazima ujue ni nani unayemlipa kuliko ilivyo sasa.

Kwa mujibu wa maelekezo hayo uhamisho na uidhinishaji katika mfumo wa watumishi ambao wamehamishwa kutoka kwa mwajiri mmoja kwenda kwa mwajiri mwingine ambao atalipwa mshahara mkubwa kuliko ule wa sasa pia utaangaliwa kwa lengo la kupata taarifa sahihi za mtumishi husika.

“Baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki watumishi pamoja na tathmini ya muundo wa Serikali na taasisi zake, wote wataarifiwa ni lini utekelezaji utaendelea,” alisema.

Taarifa kutoka maeneo mbalimbali nchini, zililiambia gazeti hili kuwa maelekezo hayo yalitolewa Juni 13, mwaka huu na kusambazwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwa makatibu wakuu wote, makatibu tawala wa mikoa, kwa wakuu wa idara za Serikali zinazojitegemea.

Waliotakiwa kutekeleza maelekeo hayo ya Serikali ni wakurugenzi wote wa majiji, manispaa na miji, wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya, watendaji wa taasisi za umma na watendaji wa wakala za Serikali kwa upande wa Tanzania Bara.
 
Ngoja nijipange kuandaa shamba langu la mihogo mvua hazipo mbali. Kuendelea kuwaza haya mambo ya mshahara nitakufa kwa BP bure.
 
Acha wee... nilikutega nione how far you know this issue... kumbe hujui bado...!! I just wanted to know how deep u understood the LETTER FROM UTUMISHI...!!

NIKUELEZE TU...!!

1: Kwa kawaida kila mwaka wa SERIKALI unaanza July, na kunakuwepo na promotion, kupandishwa vyeo, ajira mpya kwa waliopita interviews na nyongeza ya mishahara kila July ya mwaka... sasa hiyo HAITAKUWEPO...!" immediately July... but itakuwa PENDING..!! umeelewa... kisha wakimaliza kuhakiki watumishi hewa wataendelea na kuwaajiri, again be careful, kuna wale ambao TAYARI WASHAINGIZWA KTK PAYROLL hao watapata mshahara na ajira zao kama kawa.. hata June hii mwishoni kama yuko ktk payroll atalipwa...!! So sio kujibu kirahisi rahisi tu... huo waraka ni mfupi kuelewa na kutoa majibu hapa kama ww ndio umeandika..!!

2: Ile 2% ya punguzo from PAYE ya Rais alisema May Mosi ipo, so unafuu ni huo, ni kidogo but ndio hivyo..!!

3: Kuna watumishi ambao kwa sbb moja au nyingine hawakupanda vyeo kwa miaka kadhaa hadi 7 hv na wana sifa na skills zote, na very competent, na walishawasilisha their complains hata kama ni say 3 hao WATAPEWA PROMOTION tena kwa double...!! mserereko..!! So promotion pamoja na kupandishwa vyeo kwa baadhi ya watumishi ambao kuna rare cases kama hizo zipo kabisa... HATA WAZIRI KAIRUKI alisema wazi juzi.... ingia blog ya UTUMISHI utaona hilo tangazo la ANGELA KAIRUKI...!! www.utumishi.go.tz hapo kuna HABARI ZOTE ZA KILA SIKU ZA UTUMISHI WA UMMA.. so usiwe wa kupotosha watu humu..!!

So i just wanted to see how far you understand this adverts ya UTUMISHI... bado hujaielewa vema...!!

Nilitaka kujua tu uko vp... maana nimeona unajibu watu humu ndani as IF UKO UTUMISHI... NA UMESEMA UMEMUULIZIA MTU WA UTUMISHI..!! Hauko sahihi...!!

Be very very keen once you answer things you don't know well... na kutoa majibu kumbe hujui kitu... is BETTER UKAULIZA... i demeaned you..!!

Mkuu vipi na wale ambao tulishafanyiwa promotion na tukapokea na mshahara mpya kwa miezi kadhaa, je tamko hili linatuhusu?
 
Wapinzani wameipenda sana hii habar kwa kujua watu watamchukia Magu kiukwel wanaosubr ajira hawana hamu na Magu ila hili lisipelekwe kwenye kuichukia ccm maana nchi haiendi kiccm ccm bali ki Magufuli Magufuli
 
Hapo nyuma watumishi ktk sekta binafsi walkuwa wakiishi kimashaka mashaka kwa kutokuwa na uhakika na ajira zao, sasa hivi watumishi wa umma ndo vinara wa kuishi/kufanya kazi kwa mashaka, wasi wasi, hofu, kutojua hatima ya kesho, uoga kwa JPM, n.k yaani sasa hivi kuwa mtumishi wa umma ni presha tosha!!!!
 
Back
Top Bottom