DOKEZO Serikali imeshindwa kusimamia syllabus na mihula ya shule: Shule binafsi zina mihula na likizo zao

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Midas Touch

Senior Member
Joined
Jan 23, 2008
Posts
191
Reaction score
203
WAZIRI WA ELIMU PAMOJA NA MKURUGENZI WA TAASISI YA ELIMU WAMESHINDWA KUSIMAMIA SYLLABUS NA MIHULA YA SHULE: SHULE BINAFSI ZINA MIHULA NA LIKIZO ZAO TOFAUTI

Katika suala hili msomaji zingatia haya:

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ina jukumu la kutafsiri kwa vitendo Sera za Serikali kuhusu Elimu kwa kubuni mitaala na Programu za elimu zitakazowezesha utoaji wa elimu bora katika ngazi ya Elimu ya awali, Msingi, Sekondari na Elimu ya Ualimu. Kazi hii hufanywa na Taasisi ya Elimu chini ya miongozo ya Waziri wa Elimu, kwa sasa kufikia May 2025 waziri wa elimu ni Prof. Adolf Mkenda na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania ni Dr. Aneth Komba.

Kwa mujibu wa Programu za elimu zitakazowezesha utoaji wa elimu bora, silabasi (syllabus) inatumiaka kama muongozo wa vipindi, muda, mihula na upimaji (mitihani). Silabasi ni hati inayoangazia taarifa muhimu kwa ajili ya kozi, ikijumuisha mada zinazoshughulikiwa, kazi, tarehe za kukamilisha na sera za uwekaji alama. Inatumika kama mwongozo kwa waalimu na wanafunzi, ikifafanua matarajio na majukumu.
  • Sifa Muhimu za Silabasi:
  • Maelezo ya Kozi: Hutoa muhtasari mfupi wa somo na malengo ya kujifunza.
  • Masomo Yanayohitajika: Huorodhesha vitabu vya kiada, nakala, au nyenzo zingine ambazo wanafunzi wanahitaji kusoma.
  • Ratiba ya Kozi: Inabainisha mada zitakazoshughulikiwa kila wiki au kipindi, pamoja na tarehe za kukamilisha kazi na mitihani.
  • Sera za Kozi: Inabainisha sheria na taratibu kuhusu mahudhurio, ushiriki, na uadilifu kitaaluma.
BAADHI YA SHULE BINAFSI HAZIJALI MUDA NA MIONGOZO ELEKEZI YA MITAALA, MIHULA NA HATA SILABASI KWA MUJIBU WA TAASISI YA ELIMU TANZANIA: ZINAJALI BIASHARA TU

Shule ya wasichana ya St. Clara pale Same mkoani Kilimanjaro ni mfano halisi ikiwakilisha shule nyinginezo nyingi. Shule ilifunguliwa tarehe 11/1/2025 na likizo imepangwa kufanyika kwa kidato cha II na kidato cha IV kati ya tarehe 24/6/2025 hadi 5/7/2025 sawa na siku 11 kati ya miezi 6 (siku 182). Kidato cha kwanza na Kidato cha tatu wenyewe watakuwa likizoni kati ya tarehe June 7 na July 5 2025. Kidato cha pili na kidato cha nne watabaki shuleni kwa siku 17 wakipatiwa ELIMU YA KIKASUKU kwa siku 17 wakilipia Tsh 100,000/= nje ya ada ya kawaida. HII NI KWA KISINGIZIO HAFIFU, ETI NI MADARASA YA MITIHANI YA KITAIFA 2025!

Likizo fupi na ndefu ni muhimu sana kwa wanafunzi kama mitaala na silabasi za Taasisi ya Elimu Tanzania zinavoelekeza. Swali ni kwa sababu zipi waziri wa elimu na timu yake pamoja na Taasisi ya Elimu Tanzania hawafuatilii kwa karibu mienendo ya elimu, mihula na utendaji mashuleni? Wakaguzi wa elimu wako wapi?​
WAZIRI WA ELIMU ATOA AGIZO POLE (SOFT ORDER) MWEZI APRILI 2025

Mh. Adolf Mkenda
, waziri wa elimu kunako mwezi Aprili 2025 alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akisisitiza kuhusu shule zote kuzingatia na kuheshimu mihula, mitaala na likizo za wanafunzi kwa mujibu wa miongozo ya Taasisi ya Elimu Tanzania. Lakini hali imekuwa tofauti kabisa baada ya wamiliki wa shule binafsi kutumia nguvu ya pesa/rushwa hadi kupata vibali vya kuongeza mida na ada nyakati za likizo ya mwezi June 2025. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, vibali vya kuminya likizo za mwezi wa nne na mwezi wa sita vinatolewa na viongozi wa elimu wilayani na mikoani. Haiwezekani na si MPANGO watoto wa miaka 12,13,14,15 kubaki shuleni kwa siku 182 bila likizo kwa mujibu wa miongozo ya elimu na hata mashariano na wazazi.

KWA MAELEZO HAYA, MH. WAZIRI WA ELIMU TUNAOMBA UTOE TAMKO RASMI NA KALI KUELEKEA LIKIZO NDEFU ZA NUSU MWAKA, JUNE 2025 WAKATI BAJETI YA WIZARA YA ELIMU IKIJADILIWA BUNGENI WIKI HII.
 
Attachments

  • mkenda px.jpeg
    mkenda px.jpeg
    2.2 KB · Views: 19
  • ANNETTE.png
    ANNETTE.png
    784.6 KB · Views: 24
  • WAZIRI WA ELIMU PAMOJA NA MKURUGENZI WA TAASISI YA ELIMU WAMESHINDWA KUSIMAMIA SYLLABUS NA MIH...pdf
    WAZIRI WA ELIMU PAMOJA NA MKURUGENZI WA TAASISI YA ELIMU WAMESHINDWA KUSIMAMIA SYLLABUS NA MIH...pdf
    542 KB · Views: 23
Bora Gwajima yuko sharp sana kusikiliza na kutolea ufafanuzi.Huyu wa elimu Profesa Maandazi usitegemee lolote.Mimi mwanangu lazima apumzike mwezi mzima.
 
Mkuu umeenda mbali saana.
kusema shule binafsi. Anzia shule za serikali tena za vijijini na mjini maafisa elimu wilaya na mkoa ikifika wakati wa likizo ndio wanaotoa maelekezo kuwa madarasa ya mtihani yaani drs la pili, darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili na kidato cha nne hawaendi likizo.
eti walimu wapambane wafaulu mitihani yao🤣🤣 hii nchi aliyeturoga nae karogwa.
 
WAZIRI WA ELIMU PAMOJA NA MKURUGENZI WA TAASISI YA ELIMU WAMESHINDWA KUSIMAMIA SYLLABUS NA MIHULA YA SHULE: SHULE BINAFSI ZINA MIHULA NA LIKIZO ZAO TOFAUTI

Katika suala hili msomaji zingatia haya:

  • Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ina jukumu la kutafsiri kwa vitendo Sera za Serikali kuhusu Elimu kwa kubuni mitaala na Programu za elimu zitakazowezesha utoaji wa elimu bora katika ngazi ya Elimu ya awali, Msingi, Sekondari na Elimu ya Ualimu. Kazi hii hufanywa na Taasisi ya Elimu chini ya miongozo ya Waziri wa Elimu, kwa sasa kufikia May 2025 waziri wa elimu ni Prof. Adolf Mkenda na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania ni Dr. Aneth Komba.
  • Kwa mujibu wa Programu za elimu zitakazowezesha utoaji wa elimu bora, silabasi (syllabus) inatumiaka kama muongozo wa vipindi, muda, mihula na upimaji (mitihani). Silabasi ni hati inayoangazia taarifa muhimu kwa ajili ya kozi, ikijumuisha mada zinazoshughulikiwa, kazi, tarehe za kukamilisha na sera za uwekaji alama. Inatumika kama mwongozo kwa waalimu na wanafunzi, ikifafanua matarajio na majukumu.
  • Sifa Muhimu za Silabasi:
    • Maelezo ya Kozi: Hutoa muhtasari mfupi wa somo na malengo ya kujifunza.
    • Masomo Yanayohitajika: Huorodhesha vitabu vya kiada, nakala, au nyenzo zingine ambazo wanafunzi wanahitaji kusoma.
    • Ratiba ya Kozi: Inabainisha mada zitakazoshughulikiwa kila wiki au kipindi, pamoja na tarehe za kukamilisha kazi na mitihani.
    • Sera za Kozi: Inabainisha sheria na taratibu kuhusu mahudhurio, ushiriki, na uadilifu kitaaluma.
  • BAADHI YA SHULE BINAFSI HAZIJALI MUDA NA MIONGOZO ELEKEZI YA MITAALA, MIHULA NA HATA SILABASI KWA MUJIBU WA TAASISI YA ELIMU TANZANIA: ZINAJALI BIASHARA TU
  • Shule ya wasichana ya St. Clara pale Same mkoani Kilimanjaro ni mfano halisi ikiwakilisha shule nyinginezo nyingi. Shule ilifunguliwa tarehe 11/1/2025 na likizo imepangwa kufanyika kwa kidato cha II na kidato cha IV kati ya tarehe 24/6/2025 hadi 5/7/2025 sawa na siku 11 kati ya miezi 6 (siku 182). Kidato cha kwanza na Kidato cha tatu wenyewe watakuwa likizoni kati ya tarehe June 7 na July 5 2025. Kidato cha pili na kidato cha nne watabaki shuleni kwa siku 17 wakipatiwa ELIMU YA KIKASUKU kwa siku 17 wakilipia Tsh 100,000/= nje ya ada ya kawaida. HII NI KWA KISINGIZIO HAFIFU, ETI NI MADARASA YA MITIHANI YA KITAIFA 2025!
  • Likizo fupi na ndefu ni muhimu sana kwa wanafunzi kama mitaala na silabasi za Taasisi ya Elimu Tanzania zinavoelekeza. Swali ni kwa sababu zipi waziri wa elimu na timu yake pamoja na Taasisi ya Elimu Tanzania hawafuatilii kwa karibu mienendo ya elimu, mihula na utendaji mashuleni? Wakaguzi wa elimu wako wapi?​
  • WAZIRI WA ELIMU ATOA AGIZO POLE (SOFT ORDER) MWEZI APRILI 2025
  • Mh. Adolf Mkenda, waziri wa elimu kunako mwezi Aprili 2025 alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akisisitiza kuhusu shule zote kuzingatia na kuheshimu mihula, mitaala na likizo za wanafunzi kwa mujibu wa miongozo ya Taasisi ya Elimu Tanzania. Lakini hali imekuwa tofauti kabisa baada ya wamiliki wa shule binafsi kutumia nguvu ya pesa/rushwa hadi kupata vibali vya kuongeza mida na ada nyakati za likizo ya mwezi June 2025. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, vibali vya kuminya likizo za mwezi wa nne na mwezi wa sita vinatolewa na viongozi wa elimu wilayani na mikoani. Haiwezekani na si MPANGO watoto wa miaka 12,13,14,15 kubaki shuleni kwa siku 182 bila likizo kwa mujibu wa miongozo ya elimu na hata mashariano na wazazi.
  • KWA MAELEZO HAYA, MH. WAZIRI WA ELIMU TUNAOMBA UTOE TAMKO RASMI NA KALI KUELEKEA LIKIZO NDEFU ZA NUSU MWAKA, JUNE 2025 WAKATI BAJETI YA WIZARA YA ELIMU IKIJADILIWA BUNGENI WIKI HII.

Usiwapeleke wanao huko
 
Hakuna kitu kinanikera kama likizo time watoto wanakimbizana na shule, maana ya likizo nini sasa?
 
Acha umbea …umeona hawaendani na matakwa yako wahamishe watoto wako peleka shule nyingine , siku hizi shule zote sio za serikali, binafsi au za kanisa mwezi wa sita wanasoma njoo Mbeya shule zote za sekondari madarasa ya mitihani hawatoki na wanalipia
 
Bora Gwajima yuko sharp sana kusikiliza na kutolea ufafanuzi.Huyu wa elimu Profesa Maandazi usitegemee lolote.Mimi mwanangu lazima apumzike mwezi mzima.
Hakuna atakaekushikia kiboko hata ungetaka apumzike mwaka mzima sawa ila kama wazazi walikubaliana ilo deni utalipa utake usitake
 
  • Thanks
Reactions: EEX
Hakuna kitu kinanikera kama likizo time watoto wanakimbizana na shule, maana ya likizo nini sasa?
Hili swali najiuliza hata mimi kama hao wataalamu wameona na wameweka likizo kama hakuna umuhimu zifutwe tujue moja.
 
haya mambo ya kubaki kipindi chetu hayakuwepo, ila wazaz/walez walitupa pesa ya tuition, kama mzaz/mlezi hana pesa unakausha tu. siku hizi ni kisanga kwelikweli si primary wala secondary.
 
Wazazi kwenye vikao vya shule wanakubaliana na mkuu huko SIMIYU hasa shule za serikali wanakataa lakini mikoa kama kilimanjaro, Kagera , Mbeya , na sehemu za Arusha ni kama must
 
Hii sio solution, tunataka mifumo sio matamko. Tatizo tunaongozwa na watu design kama hivi, "usiwapeleke wanao huko"!
Kila siku serikali inatangaza wanafunzi waende likizo kwa calenda iliyopo na wewe unajua.

Sasa wewe mzazi au mlezi unapoamua kuwapeleka wanao huko wasikokuwa na likizo unashangaza.

Halafu kusema private schools hawafuati ratiba ya likizo unakosea pia. Kuwa specific kwa shule sio wote.

Wanangu wanasoma private na ratiba ya likizo iko sawa na muongozo wa serikali; na ni marufuku kumpeleke mtoto tuition akiwa likizo.
Mzazi ukimpeleka mwanao tuition akiwa likizo ikagundulika unarudishiwa umtafutie shule ingine. Wanataka likizo ibebe maana halisi ya likizo.... yaani kubadilisha activities za mtoto na kumpa muda wa kujifunza mambo mengine tofauti na ya darasani
 
WAZIRI WA ELIMU PAMOJA NA MKURUGENZI WA TAASISI YA ELIMU WAMESHINDWA KUSIMAMIA SYLLABUS NA MIHULA YA SHULE: SHULE BINAFSI ZINA MIHULA NA LIKIZO ZAO TOFAUTI

Katika suala hili msomaji zingatia haya:

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ina jukumu la kutafsiri kwa vitendo Sera za Serikali kuhusu Elimu kwa kubuni mitaala na Programu za elimu zitakazowezesha utoaji wa elimu bora katika ngazi ya Elimu ya awali, Msingi, Sekondari na Elimu ya Ualimu. Kazi hii hufanywa na Taasisi ya Elimu chini ya miongozo ya Waziri wa Elimu, kwa sasa kufikia May 2025 waziri wa elimu ni Prof. Adolf Mkenda na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania ni Dr. Aneth Komba.

Kwa mujibu wa Programu za elimu zitakazowezesha utoaji wa elimu bora, silabasi (syllabus) inatumiaka kama muongozo wa vipindi, muda, mihula na upimaji (mitihani). Silabasi ni hati inayoangazia taarifa muhimu kwa ajili ya kozi, ikijumuisha mada zinazoshughulikiwa, kazi, tarehe za kukamilisha na sera za uwekaji alama. Inatumika kama mwongozo kwa waalimu na wanafunzi, ikifafanua matarajio na majukumu.
  • Sifa Muhimu za Silabasi:
  • Maelezo ya Kozi: Hutoa muhtasari mfupi wa somo na malengo ya kujifunza.
  • Masomo Yanayohitajika: Huorodhesha vitabu vya kiada, nakala, au nyenzo zingine ambazo wanafunzi wanahitaji kusoma.
  • Ratiba ya Kozi: Inabainisha mada zitakazoshughulikiwa kila wiki au kipindi, pamoja na tarehe za kukamilisha kazi na mitihani.
  • Sera za Kozi: Inabainisha sheria na taratibu kuhusu mahudhurio, ushiriki, na uadilifu kitaaluma.
BAADHI YA SHULE BINAFSI HAZIJALI MUDA NA MIONGOZO ELEKEZI YA MITAALA, MIHULA NA HATA SILABASI KWA MUJIBU WA TAASISI YA ELIMU TANZANIA: ZINAJALI BIASHARA TU

Shule ya wasichana ya St. Clara pale Same mkoani Kilimanjaro ni mfano halisi ikiwakilisha shule nyinginezo nyingi. Shule ilifunguliwa tarehe 11/1/2025 na likizo imepangwa kufanyika kwa kidato cha II na kidato cha IV kati ya tarehe 24/6/2025 hadi 5/7/2025 sawa na siku 11 kati ya miezi 6 (siku 182). Kidato cha kwanza na Kidato cha tatu wenyewe watakuwa likizoni kati ya tarehe June 7 na July 5 2025. Kidato cha pili na kidato cha nne watabaki shuleni kwa siku 17 wakipatiwa ELIMU YA KIKASUKU kwa siku 17 wakilipia Tsh 100,000/= nje ya ada ya kawaida. HII NI KWA KISINGIZIO HAFIFU, ETI NI MADARASA YA MITIHANI YA KITAIFA 2025!

Likizo fupi na ndefu ni muhimu sana kwa wanafunzi kama mitaala na silabasi za Taasisi ya Elimu Tanzania zinavoelekeza. Swali ni kwa sababu zipi waziri wa elimu na timu yake pamoja na Taasisi ya Elimu Tanzania hawafuatilii kwa karibu mienendo ya elimu, mihula na utendaji mashuleni? Wakaguzi wa elimu wako wapi?​
WAZIRI WA ELIMU ATOA AGIZO POLE (SOFT ORDER) MWEZI APRILI 2025

Mh. Adolf Mkenda
, waziri wa elimu kunako mwezi Aprili 2025 alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akisisitiza kuhusu shule zote kuzingatia na kuheshimu mihula, mitaala na likizo za wanafunzi kwa mujibu wa miongozo ya Taasisi ya Elimu Tanzania. Lakini hali imekuwa tofauti kabisa baada ya wamiliki wa shule binafsi kutumia nguvu ya pesa/rushwa hadi kupata vibali vya kuongeza mida na ada nyakati za likizo ya mwezi June 2025. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, vibali vya kuminya likizo za mwezi wa nne na mwezi wa sita vinatolewa na viongozi wa elimu wilayani na mikoani. Haiwezekani na si MPANGO watoto wa miaka 12,13,14,15 kubaki shuleni kwa siku 182 bila likizo kwa mujibu wa miongozo ya elimu na hata mashariano na wazazi.

KWA MAELEZO HAYA, MH. WAZIRI WA ELIMU TUNAOMBA UTOE TAMKO RASMI NA KALI KUELEKEA LIKIZO NDEFU ZA NUSU MWAKA, JUNE 2025 WAKATI BAJETI YA WIZARA YA ELIMU IKIJADILIWA BUNGENI WIKI HII.
Ratiba ya likizo ifuatwe kikamilifu.
 
THIS IS STATE CAPTURE MY FRIEND.
 
Nakuunga mkono mleta mada kwa sasa elimu ya Tanzania ni kama dodoki la chooni, imebeba uchafu ambao unanuka na unawarukia watoto nao sahivi wananuka uchafu wa mfumo huu mbovu wa hiki kinachoendelea.

Mie nataka nianze na nyakati za 200 kurudi nyuma wakati sie tukiwa shule. Siku za shule zilikuwa 5/wiki, hapakuwa na tuition, waalimu walikuwa wachache, resources zilikuwa shida, mitihani ilikuwa ni migumu sana lakini ajabu tulifaulu sana na ulikuwa ukikutana na mwanafunzi kamaliza fm4 kafaulu ukikaa nae kwa dakika tano tu zilitosha kukwambia kweli huyu kamaliza fm4 lakini sahivi unaweza ukakaa naye lisaa lizima na bado usielewe kama kweli hata katika kidato cha pili.

Kusema kweli elimu ya Tanzania imepoteza dira sana. Suala la elimu ni suala la kitaalamu na suala la likizo pia ni la kitaalamu na linahusisha saikolojia kwa kiasi kikubwa lakini sasa inavyoonekana ni kwamba wanasiasa wameteka elimu na hakuna tena utaalamu (professionalism). Wataalamu wamewekwa kando wamebaki wanasiasa ndo wanaendesha elimu ya nchi hii, hiki ni kifo cha elimu ya Tanzania.

Jambo jingine la kujadili hapa ni hii ishu ya remedial classes. Nakumbuka sisi zamani hatukuwa na huu uhuni unaitwa remedials, waalimu walifumdisha taratibu na mada zilifundishwa hadi wiki moja kabla ya Necta ndo mada zilikuwa zinaisha na bado tulikuwa tunapata uelewa na tulifaulu. Leo mada zinalazimishwa ziishe mwezi wa tano alafu baada ya hapo remedials zinaanza hadi Oktoba, miezi zaidi ya minne ni remedials tu. Hii haiwezi njia ya watu kupata elimu ..huku ni kukalilishwa tu na ndo maana ukiwaangalia wanafunzi wa leo vichwani hawako vizuri kiasi ukikaa nao wanakupa hadi mashaka

Serikali inalazimika kurudi nyuma Ili kuikomboa elimu ya nchi hii kama kweli wanna nia ya kuvikomboa vizazi hivi la nchi hii inakuja kuwa na wahitimu wajinga wajinga tu
 
Back
Top Bottom