Serikali imesema ina mpango wa kununua ndege nne mpya kwa ajili ya usafiri wa abiria

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
ATC-A-L-620x308.jpg

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Medard Kalemani, Naibu Waziri wa Nishati na Madini wakati akijibu swali la nyongeza la Joyce Sokombi, Mbunge wa Viti Maalum, (Chadema).

Katika swali la nyongeza mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mpango gani wa ununuzi wa ndege ili kuondokana na adha ya usafiri wa ndege nchini.

Amesema serikali imekuwa ikitenga bajeti kwa ajili ya ukarabati wa viwanja vya ndege lakini bado kuna tatizo kubwa la usafiri wa ndege kutokana na taifa kuwa na ndege moja.

Awali katika swalili la msingi la mbunge huyo, alitaka kujua ni lini serikali itajenga Uwanja wa Ndege wa Musoma katika hadhi ya kitaifa kama siyo kimataifa.

Alitaka kuelezwa ni kiasi gani cha fedha kinachopotezwa taifa kutokuwa na ndege zake kwa ajili ya kuleta watalii hapa nchini.

Akijibu maswali hayo Dk. Kalemani amesema kwa sasa taifa lina mpango wa kununua ndege mbili mpya zenye uwezo wa kubeba abiria 78 kila moja.

Amesema licha ya kununua ndege hizo pia serikali itanunua ndege nyingine mbili mpya ambapo moja ina uwezo wa kubeba abilia 120 na nyinine ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 155.

Amesema serikali imekuwa ikifanya matengenezo ya miundombinu ya Kiwanja cha Ndege cha Musoma ili kuendelea kutoa huduma kama ilivyokusudiwa wakati wa mpango wa kukijenga kwa hadhi stahiki ikiendelea.
 
Hawajasema kama ni kwa bajeti hii au ya mwakani!! Tujitahidi tupate hata ndege 4 zinatosha kuanzia! Naomba wajitahidi sana! Wangeenda airbus wapate 2 na ATR 72....ziwe 2 pia!
 
Kwa soko la Tanzania lilivyo kwa sasa angeanza na ndege ya abiria 155 na hiyo ya abiria 80 ili kupambana na competition ya Fastjet. Kumbuka shirika litatakiwa kujiendesha na sio kupewa ruzuku baada ya kupata mtaji wa ndege nne.
 
Ndege mbili za mwanzo zitakua Bombardier CRJ900 halafu baadae Airbus A319 na Airbus A320.
 
Kwa soko la Tanzania lilivyo kwa sasa angeanza na ndege ya abiria 155 na hiyo ya abiria 80 ili kupambana na competition ya Fastjet. Kumbuka shirika litatakiwa kujiendesha na sio kupewa ruzuku baada ya kupata mtaji wa ndege nne.
Hawajasema kama ni kwa bajeti hii au ya mwakani!! Tujitahidi tupate hata ndege 4 zinatosha kuanzia! Naomba wajitahidi sana! Wangeenda airbus wapate 2 na ATR 72....ziwe 2 pia!
Hela walizokula wajanja kwa kukodisha ndege zingeweza kununua ndege mpya kibao. hii ndio nchi watu wanapeana vyeo kama tiketi ya kuiba fedha ya umma. waroho wanakula hadi wanavimbiwa. jpm kazi bado ya kutumbua majipu. hata kama wamestaafu tumbua tu umma wa wananchi watafurahi sana.
 
Nadhani kuna ka laana flan hapo kati jamani. Tanzania isijekukopa hizo hela kwani wakina Mataka wapo wengi na sasa weshaanza kusuuza koo zao.
Chonde mh Magu usikope hiyo hela, tumia za majipu, kwani tangu Julius awanyang'anye watu jasho lao, naona alichukua na za kizee kisichoibiwa ndo maana kila mnayemuweka hapo hata ka hajui kuiba anajifunzia hapo. Wanasemaga; Muosha huoshwa. Aliwaosha watu naye lazima aoshwe.
 
Waste of money hizo hela zingewekezwa kwenye ujenzi wa nyumba za bei, miundo mbinu ya umeme, viwanda vya uzalishaji vingesaidia watanzania wengi directly kuliko kwenda kununua ndege na all those investment have quick return as opposed to aeroplane investment. Kwa hali ya Tanzania kununua ndege ni luxury ya serikari sio need ya jamii.
 
Are you sure? Economics ulisomea shule gani au ndio akili za kuokotea mitaani kwenye kahawa?
 
Embu tupe walau basi fikra zako za return za makampuni ya ndege zinazofanya kazi kwa sasa Tanzania uone return zao zikoje; halafu angalia na return za wapangaji au wazalishaji kama akina Bakhresa wenye viwanda. Kwa nchi yenye shida kipi kipaumbele.

Tanzania hakuna wachumi ni wachache sana kwa ma-professor ninao wasikia hakuna kitu pale.
 
Waste of money hizo hela zingewekezwa kwenye ujenzi wa nyumba za bei, miundo mbinu ya umeme, viwanda vya uzalishaji vingesaidia watanzania wengi directly kuliko kwenda kununua ndege na all those investment have quick return as opposed to aeroplane investment. Kwa hali ya Tanzania kununua ndege ni luxury ya serikari sio need ya jamii.

Mmmhhh,,, kazi kweli,, Hakuna maendeleo bila usafiri wa anga katika Dunia ya Sasa,,, unaonaje una vyanzo vingi vya utalii lakini nchi zingine ndo zinanufaika na ujio wa watalii kwa ndege zao huku ww ukisubiri makusanyo ya kuangalia wanyama tuu,, think wide guy
 
Hao watalii unaenda wabeba bure au inabidi ushindane bei Kenya airways tu sasa imeanza kushindwa kuwaleta wanao tua kwao kuelekea Tanzania swala hapo ni bei; ndio inabidi ujiulize return za kununua ndege na return za invesmtment kama nyumba inayotoa ajira, katika kipindi hiki watu wanacho lalamika mzunguko wa hela umepungua, ajira zinaitajika which is the better option to waste over $100 economically.
 
Aibu sana kwa familia kuwa na mtoto kama wewe. Tumia kichwa kufikiri sio kufugia nywere tu. Wewe ni kipofu huoni unaenda wapi ili mradi unakula tu.
Kula inataka maarifa ya kutengeneza hela sio kulelewa kwa kunyonya vipapa na kujiongopea una value yoyote duniani wakati watoto kike wanalea wanao unajua hela wanawatoa wapi
 
Ili hili shirika lisimame waziri husika anatakiwa atambue kwamba hii sekta ya usafiri wa anga haitakiwi ubabaishaji.
Inatakiwa ipa wafanyakazi wazoefu na hii kazi wakianza kuweka watu wasio na ujuzi hakina kitu kitafanyika.

Wapo watanzania wengi sana wanaofanya kazi kwenye mashirika ya ndege za kimataifa watumie strategy hii ya kutoa nafasi ya upendeleo kwa ajira kadhaa ili kuleta changamoto ya maendeleo na mawazo mapya.

Lakini wakitegemea akili za wafanyaka hao hao wanaoendesha ndege moja kwa siku tutafeli.
 
Wewe huna hata hela wewe unategemea kupewa na shemeji yako. Kichwa kikuuuubwa kama Kalonzo Musyoka lakini akili ndooogo kama za kuku.
Teh teh teh ni hivi rudisha salamu waambie wakirudia tena nawawasha full blast sina muda wa kucheka na nyani wenye njaa siku hizi nasonga mbele ntawapa sababu sasa nilizowapa wenzao wanune na awatopenda trust.

Heshima sio uwoga
 
Nimesema akili zako sio nyingi haziwezi kujaa hata kwenye kijiko cha sukari. Unabwabwaja tu bila hata mpango. Serikali inanunua ndege. Mpango unaotaka nenda kafanye na shemeji yako mme wa dada yako.
Umeishiwa choko tu mwingine
 
Embu tupe walau basi fikra zako za return za makampuni ya ndege zinazofanya kazi kwa sasa Tanzania uone return zao zikoje; halafu angalia na return za wapangaji au wazalishaji kama akina Bakhresa wenye viwanda. Kwa nchi yenye shida kipi kipaumbele.

Tanzania hakuna wachumi ni wachache sana kwa ma-professor ninao wasikia hakuna kitu pale.

Uliza watu wa utalii wakwambie ni namna gani kukosa national carrier kunaathiri utalii
 
Kwani umeambiwa ukosoe hoja kama sio kujishaua tu. Huna maisha yoyote wewe.
Maisha yana mtazamo tofauti kwanza the whole concept ya JF na siasa kwa ujumla ni hoja; ps sijawaji kufanya kitu au kutaka kitu maishani mwangu nikashindwa ambacho sina sijakitaka tu huo ndio uhalisia wenyewe waulize unadhani kununisha watu jambo rahisi.
 
Back
Top Bottom