Serikali imemaliza maandalizi ya riot, isije kukamata watu kwa makosa ya uhaini. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali imemaliza maandalizi ya riot, isije kukamata watu kwa makosa ya uhaini.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Consigliere, Feb 1, 2012.

 1. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,042
  Likes Received: 7,488
  Trophy Points: 280
  Malalamiko mapya yameibuka kwa wafanyakazi wa idala tofauti za serikali. Malalamiko hayo ni juu ya makato ya mishahara ya watumishi.
  Imethibitika hivyo baada ya watumishi kukuta mapungufu katika mishara yao ya mwezi huu, na walipojaribu kuwasiliana na DED's kwa ufafanuzi waliambiwa kuwa walipewa maagizo hayo kupitia maafisa uajiri kuwa mishara ipunguzwe kwa wote ambao waliongezewa kwa sababu tofauti kwa kigezo kuwa nyongeza hizo zilifanywa kimakosa.

  Hapa ndipo najiuliza kuhusu utendaji wa wakubwa hawa wa serikalini kama una make any sense.
  Ieleweke kuwa uongezwaji wa mishahara ulifuata taratibu zote kama ilivyoanishwa kisheria lakini hili la ku-suspend ongezeko hilo limekuja as a suprise, na kuonekana kama kituko cha kihistoria kwa mshahara wa muajiriwa mwenye vigezo kupunguzwa badala ya kuongezeka.
  Ni jambo la kichonganishi lenye kuchokoza hisia na kudunisha hadhi za watumishi, na ndipo ninapo thubutu kusema serikali imemaliza kufanya maandalizi ya 'riot' na isijekutafuta wa kuwatupia makosa ya 'uhaini'.
   
Loading...