Serikali imekwenda mchomo- JUMIKI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali imekwenda mchomo- JUMIKI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, May 3, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Posted on May 3, 2012 by zanzibaryetu


  Pia Katiba ya Zanzíbar imetoa uhuru wa kuabudu kwa kusema katika ibara ya 19:2 “Bila ya kuathiri sheria zinazohusika kazi ya kutangaza dini kufanya ibada na kueneza dini itakuwa huru na jambo la hiari ya mtu binafsi” kwa maana hiyo basi Jumuiya za Kiislamu katu hazitosita kuendelea na uhuru huo unaolindwa na Katiba ya Zanzíbar usio athiriwa na sheria ndogo ndogo zinazotungwa kwa malengo maalum pia zitaendeleza mihadhara yake ikizingatia kudumisha amani ambayo inaonesha wazi kuwa kwa wale madhalimu wasiowatakia mema Wazanzibar tayari wameanza kujichomoza kutaka kuvunja amani kwa visingizio visivyokuwa na hoja ya kisheria pia inaonesha dhamira yao mbaya ya kutaka kumpaka matope Mhe. Rais wetu wa Zanzíbar Dr. Mohamed Shein pamoja na Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa lakini hatushangazwi na watu hao kujitokeza kutaka kuhatarisha na kuvunja amani kwani hao ndio waliosimama kidete kupinga kuanzisha Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa jambo ambalo linaonesha kuna ajenda ya siri ya kutaka kuwagawa Wazanzibar na kuhatarisha amani.
  TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM ZANZIBAR.

  KWA VYOMBO VYA HABARI BAADA YA KAULI YA MHE. MOHAMED ABOUD YENYE NIA YA KUVUNJA NA KUVURUGA AMANI YA NCHI ILIYOTOKA JANA TAREHE 2/5/2012 ZBC.

  03/05/2012


  NDUGU WAANDISHI WA HABARI

  ASSALAMA ALAYKUM WARAHMATU -LLAH WABARAKATU


  Awali nachukua fursa hii kumshukuru Allah subhana wataala muumba mbingu na ardhi mwenye kumpa Ufalme amtakae na kumnyima amtakae pia tunamtakia rehma kipenzi cha umma Mtume wetu Muhammada (S.A.W) baada ya shukurani hizo tunatoa shukurani zetu za dhati kwa Rais wetu mpenzi Dr. Ali Mohammed Shein kwa uongozi wake imara uliojaa uadilifu, hekima pamoja na serikali yetu ya Kitaifa na usimamizi wake madhubuti wa kuhakikisha anatandika zulia la demokrasia na kuhubiri amani, umoja na mshikamano.


  Ndugu waandishi wa habari.

  Kwa kweli tumesikitishwa sana na kauli ya Mhe. Mohammed Aboud aliyoitoa jana kwenye vyombo vya habari yenye lengo la kuzuia mihadhara inayoendeshwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu kwa kusimamiwa na Jumuiya ya Uamsho JUMIKI kwa kisingizio cha sheria No. 8 ya mabadiliko ya Katiba kwa maana hiyo tunapenda tutoe ufafanuzi juu ya sheria hiyo katika ibara zake zinazohusu suala la utoaji elimu. Ibara ya 17:8 “Mtu au asasi yoyote itakayotaka kuendesha programu ya kutoa elimu juu ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba, kabla ya kuanza kutoa elimu hiyo sharti, iwe imesajiliwa ……… na itawajibika kueleza kwa tume chanzo cha fedha ya kuendesha programu hiyo” ibara ya 21:2C “Mtu yeyote atakaeendesha programu ya elimu… kinyume na masharti ya sheria hii atakuwa ametenda kosa”


  Ndugu waandishi wa habari

  Napenda mzingatie kuwa:
  1. programu ya elimu inayomtia mtu hatiani kwa mujibu wa sheria hiyo ni elimu inayohusu sheria ya mabadiliko ya Katiba.
  2. Masharti yaliyoekwa ni kuwa Jumuiya imesajiliwa Serikalini.

  3. Inalazimika kutoa taarifa tu na kueleza chanzo cha fedha sio kutaka ruhusa au kuomba kibali.

  Kwa bahati nzuri Jumuiya za Kiislamu imeliona hilo mapema na tayari
  programu za elimu juu ya mabadiliko ya Katiba zimemaliza kwa muda
  mrefu kwa sasa hivi Jumuiya inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuweza
  kujua sheria za nchi na Katiba yao jambo ambalo kwa muda mrefu Serikali
  haikuwa na utaratibu endelevu wa kuelimisha raia zake na hiyo ndio kazi
  inayoifanya Jumuiya kuisaidia Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa sambamba
  na kutoa elimu ya Kiislamu kufunza maadili mema, kudumisha amani,
  umoja, utulivu na mshikamano kwa wazanzibari wote bila kujali tofauti zao
  za kidini, kisiasa, rangi na ukabila pamoja na kusisitiza umuhimu wa kudai haki zao na uhuru wa maoni pamoja na kulinda mali ya umma na kutii Katiba ya Zanzibar na sheria za nchi. Ibara ya 23:1 ya Katiba ya Zanzíbar inasema “kila mtu anawajibu wa kufuata na kutii Katiba hii na sheria za Zanzíbar” 23:3 inasema “watu wotewote watatakiwa na sheria kulinda vizuri mali ya Zanzíbar na kwa pamoja kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu… kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya badea ya Taifa lao”.


  Ndugu waandishi wa habari.

  Jumuiya ya Uamsho inaendesha mihadhara kwa miaka mingi kuzingatia Katiba yake pamoja na kufuata Katiba ya Zanzíbar inayotoa uhuru wa maoni kutipia ibara ya 18 inayosema “Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yupo huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake na kutafuta kupokea na kutoa habari na dhana kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi”.

  Pia Katiba ya Zanzíbar imetoa uhuru wa kuabudu kwa kusema katika ibara ya 19:2 “Bila ya kuathiri sheria zinazohusika kazi ya kutangaza dini kufanya ibada na kueneza dini itakuwa huru na jambo la hiari ya mtu binafsi” kwa maana hiyo basi Jumuiya za Kiislamu katu hazitosita kuendelea na uhuru huo unaolindwa na Katiba ya Zanzíbar usio athiriwa na sheria ndogo ndogo zinazotungwa kwa malengo maalum pia zitaendeleza mihadhara yake ikizingatia kudumisha amani ambayo inaonesha wazi kuwa kwa wale madhalimu wasiowatakia mema Wazanzibar tayari wameanza kujichomoza kutaka kuvunja amani kwa visingizio visivyokuwa na hoja ya kisheria pia inaonesha dhamira yao mbaya ya kutaka kumpaka matope Mhe. Rais wetu wa Zanzíbar Dr. Mohamed Shein pamoja na Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa lakini hatushangazwi na watu hao kujitokeza kutaka kuhatarisha na kuvunja amani kwani hao ndio waliosimama kidete kupinga kuanzisha Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa jambo ambalo linaonesha kuna ajenda ya siri ya kutaka kuwagawa Wazanzibar na kuhatarisha amani.


  Jumuiya za Kiislamu zinawatahadharisha watu hao na kuwataka mara moja waache kuhubiri uchochezi na uvunjifu wa amani na kuwakumbusha kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria ibara ya 12 ya Katiba inasema “ Watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki bila ya ubaguzi wowote” vile vile wajue hizi ni zama za uwazi haki na sheria hivyo tunawasihi wasijisahau wakavitumia vyeo na ngazi za uongozi kwa maslahi ya wachache sana wasioitakia mema Zanzíbar watambue kufanya hivyo ni kuvunja Katiba ya Zanzíbar na sheria za nchi rejea ibara ya 14,16,23 ya Katiba ya Zanzíbar.


  Pia Jumuiya zinapenda kuchukua fursa hii kumtaka Mwanasheria Mkuu wa Zanzíbar kutoa ufafanuzi juu ya kifungu cha 17:8 na 21:2C kwa kuzingatia uhuru wa kuabudu na uhuru wa maoni unaolindwa na Katiba ya Zanzíbar. Pia kutoa ufafanuzi juu ya kifungu cha 10 cha Sheria hiyo hiyo No.8 ya mabadiliko ya Katiba kinachoipa Tume uhuru na mamlaka kamili ambayo Mhe. Mohamed Aboud anaonekana kuvikiuka na kuingilia kazi za tume kwani Katibu Mkuu wa Tume hakuwa na taarifa yoyote wakati Jumuiya zinawasiliana nae akiwa bado ndio kwanza anataka kuisoma taarifa hiyo kwenye mtandao.

  Imani yetu huu ndio Mwanzo wa uvunjifu wa sheria hiyo. Tunapenda kumkumbusha Mhe. Mohamed Aboud maneno ya Rais Dr. Shein aliwataka wananchi wa Zanzíbar wanaishi kwa umoja na mshikamano inapaswa hitilafu ziondolewe ili Wazanzibar waishi vizuri kwa amani na utulivu na kamwe asitokee mtu akiwa ana lengo la kuivunja amani iliyopo rejea gazeti la Zanzíbar leo lenye kichwa cha maneno TUSICHAFUE AMANI toleo No 3743.


  Ndugu waandishi wa habari .

  Tunapenda kumalizia taarifa hii kwa kutoa shukurani zetu za dhati kwa jeshi la polisi kusimama imara katika kudumisha amani ya nchi na kutokubali kuburuzwa na hao wachache wasioitakia mema nchi yetu ya Zanzíbar.

  Ahsanteni sana.


  Nakla:

  Rais wa Zanzíbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,

  Mwanasheria Mkuu wa Zanzíbar,

  Waziri wa Katiba,

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais,

  Jeshi la Polisi,

  Idara ya Mufti Zanzibar ,

  Share this:
  Email
  Digg
  Print
  Twitter
  Facebook
  Reddit
  StumbleUpon


  Like this:

  Like
  Be the first to like this post.
  This entry was posted in Uncategorized by zanzibaryetu. Bookmark the permalink.


  About zanzibaryetu
  Mwandishi wa khabari wa Zanzibar kwa miaka 10
  View all posts by zanzibaryetu →

  2 thoughts on “Serikali imekwenda mchomo- JUMIKI”
  Issa Mohammed on May 3, 2012 at 1:47 pm said:

  Hee ! Kazi ipo baina ya wenye kutetea haki [Jumiki] na wenye kutetea dhulma kina Mohammed Aboud, Balozi Idi na wenziwao. Inshaallah haki itasimama.

  Reply ↓
  makame silima on May 3, 2012 at 2:14 pm said:
  Your comment is awaiting moderation.

  A/allaykum Ndugu zangu Wazanzibar kesho ni ijumaa kwa hio ndio siku ya Kumshtakia Allah kwa dua kubwa kubwa za hawa wanafiki na wababaishaji walio kumbatia Dunia na wakaasha uadilifu.

  Reply ↓

  Serelly on May 3, 2012 at 2:13 pm said:

  Kwanza napenda kukumbasha kwamba hawa sio viongozi wa UAMSHO tu bali ni pamoja na taasisi nyengine mbali mbali za Dini ikiwemo JUMAZA, waandishi tunaomba mtumie phrase ya “JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU ZANZIBAR” ili kuonesha sura halisi ya UMOJA WETU.

  Alhamdulillah huu ndio msimamo wetu kama walivyoutanguliza KAKA zetu As-haabul-kahfi, Nabii Mussa kwa Firaun na Mtume {s.w} na Maswahaba wake {r.a} kwa Makurayshi. Na mwisho waliipata Nusra ya Allah {s.w}
  Ndugu zangu tushikamane kikweli kweli mpaka tuupate uhuru wetu mahbuub. MASHEIKH tuko pamoja mpaka kieleweke.

  Moh’d (MADUDU) Aboud angalia umekuja Duniani kutafuta radhi za Allah {s.w} na sio kugombana na Masheikh kwa ajili ya tumbo lako eheee! Madrasa kama umesoma hukusomeshwa na polisi isipokuwa umesomesha na Masheikh na ulikuwa ukiwapa tabu sana maana ni kichwa ngumu hufahamu kirahisi hata muungano umeshindwa kuyaona madhara yake- maana ninashaka kama umefika angalau Juzuu ya pili, wenzio hao wanaokutuma washaona mbaaali wewe mwenzangu mie ndio unajifanya shehaaata haya mkataa la Mussa hupata la Firauni, endelea bosi masharubu kugombana na wenye NDEVU langu jichoo, na kusudi haina pole. Kocha wenu Komandoo yuko wapi leo ? Leo hii ukimtoa barabarani na ukamwambia tayari tushafika chooni anza kukojoa bila shaka atakojoa tu, Jee! Mbona leo hatukuoneni mkitembea na yeye kwenye mikutano,semina na hafla zenu mbali mbali ? Wapiii ! Mmemtupaa na kumsaliti ili mtanuwe au vipi ? Basi na wewe naona huko mbali kukumbana na kipigo cha Allah (s.w). Nani asiyejua kuwa Masheikh hawa hapa Zanzibar ndio wenye kujitahidi kilillah katika kuujenga Umma wa kiislamu Zanzibar ukilinganisha na kina-Juma Faki, Soraga, Khamisi Haji n.k (Allah ajaalie watubie) ambao wao kijio ndio main first and last target {shabaha kuu ya mwanzo na ya mwisho} yao bwana.
  Chunga usigombane na waja wa Allah utaumbuka, mwambie na Ustadh wako Seif Ally Idd huu upepo mwengi sio ule wa CUF na CCM 2001.

  JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA
  vyama na njaa zenu baadae.
  Nawasilisha.
  SERELLY.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Japo sote tunalilia mabadiliko katika taifa letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania LAKINI napenda niwatahadharisheni hapa hivi sasa kwamba ZANZIBAR KUNA TATIZO TENA KUBWA SANA hadi dakika hii na linaendelea kuitika mithili ya bomu na kuweza kulipuka wakati wowote hivo nawaambieni; watch this space!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. k

  karafuu Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haki yetu allah akipenda tutaipa zanzibar kwanza chama baadae
   
 4. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,118
  Trophy Points: 280
  Mmmh hawa nao si tungejitenga nao tu jamani?
   
 5. m

  mzaire JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijui tunawanga'nga'nia kwa nini ???
   
Loading...