Serikali Imefuta kesi ya Negligent driving dhidi ya jaji Rugazia, ndio utawala bora? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali Imefuta kesi ya Negligent driving dhidi ya jaji Rugazia, ndio utawala bora?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ibange, Feb 5, 2012.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nimepata taarifa kuwa serikali imefuta kesi ya negligent driving dhidi ya jaji ambaye aligonga na kuuwa mtu. Nina washangaa sana watanzania. wakati Kenya naibu jaji mkuu anashughulikiwa kwa kutishia mtu kwa bastola, hapa kwetu tunamkingia kifua jaji ambaye ana dereva na gari ya serikali anayeamua kuendesha usiku wa manane na kwa uzembe analeta madhara. ni madereva wangapi wamepelekwa court kwa uzembe? Je, bila hukumu waathirika watalipwaje na bima? Kwanini jaji awe juu ya sheria? kama taarifa hizi ni za kweli basi tz imefika pabaya
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  serikali ipi unayozungumzia?nchi hii ina serikali toka lini?
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Katiba inasemaje kwa majaji wakifanya makosa ya jinai???labda katiba iko kimya ndio maana...wenzetu katiba yao inasema hivyo walivyoamua
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Feb 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu katiba haiko kimya. Kwa hilo la majaji tunafuata utaratibu wa jumuiya ya madola. Ni sawa tu kama walivyofanya Kenya kwa Naibu Jaji Mkuu, Nancy Baraza. Kwa Kenya kumeundwa tume ya majaji wa jumuiya ya madola ikiongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Augustino Ramadhani, ili kumchunguza Baraza na kutoa taarifa kwa Rais. Lakini tume imebidi isimame kufanya kazi yake kwa kuwa Baraza ameenda naye mahakamani.
  Hii ya Rugazia inashangaza kwa hatukusikia chochote. muda tu umevutwa basi. Tunadhalilishana. Jaji Ramadhani atapata wapi moral authority ya kumchunguza Baraza ambaye anatuhumiwa kumtishia mlinzi kwa bastola wakati Jaji wa nchini mwake ameua na hakuchukuliwa hatua zozote? Kwa hilo tu inabidi Jaji Ramadhani ajikusanye na kurudi nyumbani.
   
Loading...