Serikali imeamuru katiba ya sasa ya tff ifutwe

Serikali imeamuru katiba ya sasa ya tff ifutwe

bemg

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2010
Posts
2,799
Reaction score
644
SERIKALI imeingilia kati sakata la uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kuamuru kufutwa kwa katiba ya sasa ya shirikisho hilo na badala yake kuamuru itumike katiba ya zamani (mwaka 2006) baada ya kubaini kuwa iliyopo ina kasoro nyingi.
Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari leo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo imeeleza kuwa katiba ya sasa ya TFF si halali. Imeelezwa vilevile kuwa msajili wa vyama vya michezo aliyedaiwa kuipitisha katiba hiyo ameondolewa.
Mchakato wa uchaguzi mkuu wa TFF umesimamishwa kutokana na mgogoro mzito uliotokana na kuenguliwa kiutata kwa wagombea kadhaa, wakiwamo Jamal Malinzi anayewania urais na Michael Wambura anayetaka kugombea nafasi ya makamu wa rais.
Kamati ya rufani ya TFF inayoongozwa na Iddi Mtiginjola ndiyo iliyozua balaa lote la sasa baada ya kuwaengua kina Malinzi na mwishowe kumuacha makamu wa sasa wa rais, Athumani Nyamlani abaki kuwa mgombea pekee.
Hata hivyo, tayari mchakato wa uchaguzi huo uliozua mabishano makali umeshasimamishwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na maafisa wa chombo hicho cha juu cha mchezo wa soka duniani wameshaanza kuwasili kufuatilia kinachotokea nchini.
Uamuzi wa serikali wa kufuta katiba ya sasa na kutaka itumike ya 2006 unampa ahueni kubwa Wambura ambaye alishasema hadharani kuwa ataiburuza TFF mahakamani kama isipoachana na katiba mpya na kufuata ya zamani; huku akitoa sababu kadhaa za kupinga matumizi ya katiba mpya, mojawapo ikiwa ni kupitishwa kwake kwa njia ya waraka wa barua pepe (e-mail) kwenda kwa wajumbe badala ya kufuata maelekezo ya katiba yanayotaka mabadiliko kufanywa na wajumbe kupitia mkutano mkuu.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taratibu za FIFA, ni marufuku kwa shughuli za soka kuingiliwa na serikali au mahakama na nchi yoyote inayokwenda kinyume na taratibu hizo hujikuta ikifungiwa kama ilivyowahi kutokea nchini Kenya.
(CHANZO: straikamkali.blogspot.com)
 
nilijua tu hizi kamati za kujuana zina ajenda ya siri Idi Mtiginjola na Athuman Nyamlani ni maswahiba lazima wabebane...... Idi alikuwa mbele ya Nyamlani tumaini univ llb. So huo ulikuwa mkakati maalum
 
Ubaba ishaji tu soka letu we kiongozi unakaa madarakani miaka nane alafu unashindwa simamia uchaguzi je tutafika...!!
 
kama ni kufungiwa bora tu,kwani hii tff ilikuwa imegeuka kama chama cha wateule wachache tu,kama hauko nao hata ufanyeje huwezi ingia pale,mf.michael wambula kila anapoibukia wapo!Na Tenga anaondoka kwa aibu kubwa!wa tz wa sasa sio wale wa zamani,mmeifanya tff kama nyumba zenu,unaamua unavyotaka,m2 akitaka kupata haki yake,inakuwa ngumu kwani hizo kamati zote mlizoweka ni usanii tupu,'nyani wale wale msitu tofauti'ukitaka kwenda mahakamani oh!fifa hairuhusu!
 
Nilikwisha sema Iddi na NYAMLANI WANA LAO... TULIMKATAA MHESHIMIWA NYAMLANI ambaeni HAKIMU MKAZI WA MAHAKAMA YA MKOA KINONDONI. Haiwezekani Hakimu Mwajiriwa wa serikali akawa Rais wa TFF. Haiwezekani tena etui wakasuka njama eti ndo awe mgombea pekee wa TFF uRAIS. iMEKULA KWAO NA FITINA AZAO
 
Imekula kwao TFF na fitina za kubebana mchana kwepu zimeshindwa
 
Mdau amenena haya hapa:

Uchaguzi huu wa TFF umenifanya niweza ku-prove hypothesis yangu. Naomba ni-share nanyi ili mnipe mawazo yenu kama nipo sahihi. Hypothesis yangu ni kuwa. Unapokuwa na Chama Tawala, chochote kile, kilichopoteza dira, kimegubikwa na vitendo vyote vichafu kama vile rushwa, wizi, majungu, kupakana matope, kuchafuana, kuzushiana uongo n.k. basi utamaduni huu haushii tu kwa chama hicho tawala, bali husambaa katika kila segment ya jamii. Husambaa katia serikali, wizara, idara, mahakama, vyombo vya usalama, Bunge, vyombo vya habari, taasisi, agencies mbalimbali, mashirika, asasi za kiraia, vyama vya michezo na wakati mwingine hata vyama vya upinzani. Ninachotaka kusema utamaduduni huu wa kupindisha mambo na kufanya mizengwe ni ugonjwa ambao unaambukiza. Mgonjwa namba moja ni chama tawala na sasa ametuambukiza gonjwa hili, tumeambukizwa gonjwa baya kutoka chama tawala, gonjwa hili linatafuna hata vyama vyetu vya vinavyohusika na michezo na jamii nzima kwa ujumla. Nikiangalia uchaguzi wa TFF ninaona kuna a lot of similarities na chaguzi zote zinazofanyika ndani ya CCM. Eti CCM wanapofanya uchaguzi, Mwenyekiti wao, anawaambia TAKUKURU waende kuwakamata watoa rushwa. Halafu bado kinakaa madarakani??!! Duh!!! Gonjwa hili tumerithi au tumeambukizwa kutoka chama tawala. Hatuwezi kufanya mambo yetu kwa kufuata sheria na kanuni kwani chama kilichopo madarakani kinaonyesha mfano mbaya. Chama Tawala ni taasisi muhimu sana katika kunyoosha mustakabali wa Taifa lolote lile. Chama legelege huzaa serikali dhaifu , taasisi dhaifu, asasi za kiraia dhaifu na hata vyama vinavyosimamia michezo dhaifu. Tusubiri mizengwe ya uchaguzi wa Chaneta unaokuja.

Selemani
 
Hii serikari nayo inamaslahi yake kwanini tff imetoa mimacho sana wakati uchaguzi wa kamati ya olimpiki chini ya kada wa chama tawala filbet bahi pamoja na zengwe zote zilizojitokeza ilikaa kimya.,.


Tuwe makini sana na jambo linaloingiliwa na hii serikali maana mara nyingi linakua inamikono ya makada.
 
Back
Top Bottom