tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 23,516
- 21,542
Siku za nyuma aliyekuwa Meya wa Jiji, Dr Didas Masaburi aliwahi kutamka hadhrani kwamba baadhi ya makada wa CCM hufikiri kwa kutumia kiungo fulani cha mwili (jina limehifadhiwa). Juzi kati January Makamba amekaririwa na vyombo vya habari akiikashfu serikali ya kikwete kuwa ilikuwa ikiwabeba watu (na yeye akiwamo).
Nimetafakari sana mantiki ya kashfa hii sijapata jawabu mujarabu. Ndio maana imenichukua muda kuandika makala haya ili wananchi wenye nia njema na Chama Chetu Cha Mapinduzi tujadiliane hili suala kwa ufasaha mpaka tupate jawabu. Mimi nadhani huyu Makamba Jr anafikiri kwa kutumia kile kiungo alichokitaja Dr Masaburi kwani hawezi kuwa na ujasiri kiasi hiki kumtukana mwenyekiti wetu wa chama huku wanachama tumekaa kimya. Ikumbukwe kwamba serikali ya JK ilikuwa makini kuliko hii serikali ya KUKURUPUKA. Sasa iweje huyu mwendawazimu aikashfu serikali ya JK hadharani?
Inapofika hatua mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama chetu anamkashfu mwenyekiti wa chama jambo hili haliwezi kufumbiwa macho hata kidogo. Chama chetu kina utaratibu mzuri wa kushughulikia matatizo ya chama na nidhamu za wananchama badala ya kusemana hadharani kama hivi, jambo ambalo linazidi kukiweka vibaya chama chetu mbele ya wananchi. Mkumbuke kwamba wananchi wa leo ni werevu sana kuliko wa enzi zile za Mwalimu. Chama chetu kimefika hapa kwa sababu ya kuwafumbia macho watu wanafiki na wenye wivu wa kike kama Makamba.
Hivyo basi, niumuombe mwenyekiti wa chama chetu, Prof Jakaya Kikwete, achukue hatua anazoona zinafaa dhidi ya mjumbe huyu wa Halmashauri Kuu aliyeamua kwa utashi wake mwenyewe kukichafua chama na serikali yetu hadharani bila kuzingatia madhara yake kwa wananchi tunaowaongoza.
Kama ndugu Makamba ataona kwamba chama chetu ni chama cha kubebana, yuko huru kuhamia chama atakachoona kinamfaa kuliko kubaki ndani ya chama huku akimtukana mwenyekiti wetu bila soni. Kama alizoea kubebwa ni yeye sio kila mtu anabebwa. Asikate tawi huku amekaa juu yake, akae pembeni kwanza halafu ndipo aanze kukata!
Naomba kutoa hoja.
#HAPA_KAZI_TU!