Serikali ilimpenda, ilimchukia au ilimuogopa Reginald Mengi?

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,498
Reaction score
28,720
KILIO kikubwa cha bilionea Reginald Mengi ni sera za Serikali kiuchumi. Mpaka amefariki dunia, amekuwa kielelezo cha mtu mwenye uthubutu wa kupinga utaratibu wa Serikali hususan utoaji fursa za uwekezaji.

Mwanzoni mwa miaka ya 1970, Mengi aliporejea nchini akitokea Scotland, alikokwenda kusomea shahada ya Uhasibu, alikuta nchi imeshashika usukani katika mfumo wa ujamaa. Na kwa vile ndoto yake ilikuwa biashara, aliona mazingira yalikuwa magumu mno.

Katika kitabu chake, "I Can, I Must, I Will; The Spirit of Success", kwa maana ya "Naweza. Lazima. Nitafanikiwa; Nafsi ya Mafanikio", anasema kuwa nyakati za ujamaa fursa zilikuwa chache na zilitolewa kwa upendeleo kwa Watanzania wenye asili ya Asia.

Anasema Watanzania weusi walidhibitiwa kufanya biashara na kufanikiwa kwa sababu walihofiwa kama wangekuwa na fedha nyingi, basi wangehodhi siasa za nchi kutokana na nguvu kubwa kubwa ya kiuchumi ambayo wangekuwa nayo.

Anatolea mfano alipoanzisha kiwanda cha vinywaji baridi cha Bonite Bottlers (Coca Cola), kwamba mwaka 1987, Mwalimu Julius Nyerere alikikosoa kwa maelezo kuwa malighafi zake zilitoka nje, kwamba huo ulikuwa ubepari.

Mengi anasema, kiwanda cha Fahari Bottlers Limited, kilianzishwa mwaka 1983, Nyerere akiwa madarakani, kikawa kinazalisha bidhaa za Pepsi, alikiruhusu kwa sababu kilikuwa cha Watanzania wenye asili ya Asia na Nyerere hakukikosoa.

Ukimsoma Mengi, utaona kwamba matumaini ya kufanikiwa zaidi kibiashara ni baada ya Rais wa Pili, Ali Hassan Mwinyi, kuingiza sera za ulibelari na kuruhusu kila mtu afanye anachoweza ilimradi asivunje sheria. Hata hivyo, alilalamika kuwa kipindi cha Mwinyi bado Mwalimu Nyerere alikuwa na nguvu sana.

Kipindi cha Rais wa Tatu, Benjamin Mkapa, uliibuka mgogoro mkubwa kati ya Mengi na aliyekuwa Waziri wa Uwekezaji, Wilson Masilingi. Sababu ilikuwa uwekezaji wa Hoteli ya Kilimanjaro, sasa inaitwa Hyatt Regency, The Kilimanjaro.

Mengi alitaka kuwa mwekezaji wa hoteli hiyo, lakini alinyimwa, wakapewa wawekezaji kutoka nje. Mengi aliishambulia Serikali kwamba haikuwa ikiwapa kipaumbele wazawa, na kupendelea zaidi wageni. Haya ni malalamiko ya muda mrefu ya Mengi.

Aliamini kuwa wazawa wanapaswa kupewa kipaumbele katika fursa za uwekezaji ndani ya nchi. Hata pale wazawa wangekuwa na uwezo mdogo, Mengi aliamini kwamba lilikuwa jukumu la Serikali kuwawezesha kufikia viwango vinavyokidhi uwekezaji husika.

Kipindi cha Rais wa Nne, Jakaya Kikwete, mara kadhaa Mengi aliingia kwenye mgongano na mawaziri. Zipo nyakati alituhumiwa kuihujumu Serikali ya Kikwete. Aliyekuwa mbunge wa Mkuranga, Adam Malima, aliwahi kumsema Mengi bungeni kuwa alitumia vyombo vyake vya habari kujitangaza kuliko Rais.

Hoja hiyo ya Malima ilisababisha mzozo mkubwa bengeni, huku Mengi akisimama imara kujitetea. Televisheni ya ITV ilirudia taarifa za Mengi na Rais Kikwete kuonesha kwamba Malima hakusema kweli. Mengi pia alimwandikia barua Spika Samuel Sitta kulalamika. Mwisho Malima aliomba radhi.

Wakati wa Kikwete, ukatokea mzozo kati ya Mengi na aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Sophia Simba. Tuhuma zilitolewa na Sophia kuwa Mengi hakuwa mwana CCM na alikuwa anaihujumu Serikali, vilevile alimtuhumu kutaka kuwania Urais.

Mengi aliitisha mkutano na vyombo vya habari, akaonesha kadi zake za Tanu kisha ya CCM ya mwaka 1977. Akasema hajawahi kuwa na mpango wa kuwa Rais. Hata hivyo, ilikuwa dhahiri kwamba hakukuwa na kuaminiana kati ya Mengi na mawaziri wa Kikwete.

Uliibuka mvutano mwingine pale Mengi alipoitisha vyombo vya habari na kulalamika kwamba alipewa taarifa kutoka kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri, kwamba kuna waziri alipendekeza Serikali imfilisi Mengi mali zote.

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Laurence Masha, alimpa Mengi siku saba awe amethibitisha madai yake. Mengi akamjibu siku saba alizompa ni nyingi sana, kwamba siku moja ingetosha. Siku iliyofuata, mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, wakati huo akiwa mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alimtaja Masha kuwa ndiye alitoa wazo la kumfilisi Mengi kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri. Sakata hilo likaisha kimyakimya.

Hautasahaulika mzozo kati ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo dhidi ya Mengi. Mzozo ulihusu uwekezaji sekta ya madini na uvunaji gesi asilia. Muhongo alisema hakuna mzawa mwenye uwezo. Mengi aliamini wazawa wakipewa kipaumbele wataweza.

Aliwahi kufanya kikao na vyombo vya habari na kuelezea taarifa alizozipata ndani ya jeshi la polisi kuwa kulikuwa na mpango wa kumwekea dawa za kulevya mtoto wake ili kumkamata nazo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ili kuifanya jamii imuone yeye na familia yake ni wauza dawa za kulevya.

Mizozo hiyo ya mara kwa mara ambayo Mengi alikuwa nayo dhidi ya Serikali, na kwa kukumbuka kauli yake kwamba Watanzania wazawa (weusi), walianza kubaguliwa kwenye fursa za kiuchumi tangu wakati wa Nyerere, kwa hofu kwamba wangehodhi siasa na utawala, je, Serikali ilikuwa ikimuogopa Mengi au ilimchukia?

Pamoja na misimamo hiyo, Mengi aliwahi kuwa Mwenyekiti wa wa Bodi ya Magazeti ya Serikali (TSN), Kamishna wa Tume ya Mishahara (SRC), Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu Tanzania (NBAA), Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC), Kamishna wa Tume ya Kupambana na Ukimwi (TACAIDS) na kadhalika. Nafasi hizo zote ni za kuteuliwa na Rais. Amekuwa akiteuliwa tangu wakati wa Nyerere hadi Kikwete. Je, Serikali ilimpenda?

Mengi hakufurahia mfumo wa Serikali kujigeuza dereva wa biashara badala ya kuwaacha huru wafanyabiashara. Aliumia kuuawa kwa vyama vya ushirika. Alisema, vyama hivyo viliuawa ili kuwafanya Watanzania weusi wasiendelee na kupata nguvu kubwa ya kiuchumi. Kwamba wangehodhi siasa.

Aliamini kuwa Watanzania wenye asili ya Asia walipendelewa na Serikali. Takriban muongo mmoja uliopita, alitaja majina matano ya wafanyabiashara Watanzania wenye asili ya Asia kuwa wanafilisi nchi. Aliwaita mafisadi papa. Je, Mengi alikuwa mbaguzi? Hakuwapenda Watanzania wenye asili ya Asia?

Tumuombee Mengi pumziko jema. Kila mja ni wa Mwenyezi Mungu na kwake ndipo yalipo marejeo ya lazima.

Ndimi Luqman MALOTO
 
Japokuwa Nyerere kiuhalisia alikuwa na busara ila lile tatizo la kujifanya anajua kila kitu lilimtafuna. Kiongozi ukishakuwa na sifa hii lazima nchi uipeleke peleke kama gari bovu. Na kama u kiongozi mwenye busara utajitambua kuwa una sifa hii kutokana na wasaidizi wako wanavyokuchukulia. Ukiona wanapiga sana matarumbeta kukushangilia huku n wao wakijipamba kwa kila jema basi jua una hiyo sifa.
 
Kumbe kitabu chake kina elimu nzuri hivo natamani kukipata sijui nitakipata wapi, upendeleo wa dhahiri upo kabsa, mim binafsi huwa naona katka nchi moja kuna nchi mbili,
 
Serikali inayo ongozwa na sera imara za ccm ni serikali inayo jali na kuheshimu wawekezaji wazawa nikiri kuna viongozi kazaa waliingia kwenye migogoro na wawekezaji wa ndani kwa manufaa yao binafsi laki serikali madhubuti ililiona na kuwashuhulikia mapema mfano ni hao ulio wataja,wengi wamepelekwa ubalozini na wengine wako bench,inatosha kusema we are on right truck.
 
Kumbe kitabu chake kina elimu nzuri hivo natamani kukipata sijui nitakipata wapi, upendeleo wa dhahiri upo kabsa, mim binafsi huwa naona katka nchi moja kuna nchi mbili,
Huu ni muda muafaka watanzania wapewe fursa za uwekezaji, sio hawa kina gabachori dewji
 
Kumbe kitabu chake kina elimu nzuri hivo natamani kukipata sijui nitakipata wapi, upendeleo wa dhahiri upo kabsa, mim binafsi huwa naona katka nchi moja kuna nchi mbili,
Ata mimi nakitafuta mkuu utakapo kipata utanitag.
 
Kumbe kitabu chake kina elimu nzuri hivo natamani kukipata sijui nitakipata wapi, upendeleo wa dhahiri upo kabsa, mim binafsi huwa naona katka nchi moja kuna nchi mbili,
Bora ningenunua cha Mengi, cha Yerico nimenunua masimlizi yake yamejaa chenga tupu
 
Nimeisoma kwa umakini sana na sikutegemea kabisa
Kumbe Mengi kafa na Mengi
Hali ilianza kubadilika na kuanza kuwaona wazawa wakiamua kufanya biashara kwa wingi ila ni wachache wenye maono ya biashara kubwa kubwa na kufika mbali.
Elimu na kuiga watu na kuwa na vision ni muhimu sana katika biashara, na Mengi alikuwa na vision
Nimeshangaa sana kuona mawazo ya viongozi kuona kuwa mzawa akiwa tajiri anakusudi lingine na atakuwa na nguvu that's bullshit
Mzawa kama anapambana na wapinzani wenye asili ya asia well and good
Kama una akili ya kuweza kuwekeza na kuuza bidhaa zako chini ya bei anayouza mhindi au mwarabu safi tu kwani ndio maana ya biashara.
Mataifa mengi uchumi unashikiliwa na foreigners au wenye asili nyingine lakini haina sababu kuwa serikali zao zinawazuia wazawa kufanya vizuri

Natamani kukisoma hicho kitabu
 
Kumbe kitabu chake kina elimu nzuri hivo natamani kukipata sijui nitakipata wapi, upendeleo wa dhahiri upo kabsa, mim binafsi huwa naona katka nchi moja kuna nchi mbili,
Kaeleza ukweli halis alipotoka ,hadi alipifika hapo alipo,

Kaeleza changamoto zote za biashara

Maana wengi walikuwa wanamuuliza mwanaume Rodney baba yako amefikaje hapo alipo, ndio akamuomba baba yake kabla hajaondoka duniani aandike kitabu kuhusu mafanikio yake alipotoka hadi alipo.

Ni kizuri , ila kuna mpango wakukitafsiri kwa kiswahili
 
KILIO kikubwa cha bilionea Reginald Mengi ni sera za Serikali kiuchumi. Mpaka amefariki dunia, amekuwa kielelezo cha mtu mwenye uthubutu wa kupinga utaratibu wa Serikali hususan utoaji fursa za uwekezaji.

Mwanzoni mwa miaka ya 1970, Mengi aliporejea nchini akitokea Scotland, alikokwenda kusomea shahada ya Uhasibu, alikuta nchi imeshashika usukani katika mfumo wa ujamaa. Na kwa vile ndoto yake ilikuwa biashara, aliona mazingira yalikuwa magumu mno.

Katika kitabu chake, "I Can, I Must, I Will; The Spirit of Success", kwa maana ya "Naweza. Lazima. Nitafanikiwa; Nafsi ya Mafanikio", anasema kuwa nyakati za ujamaa fursa zilikuwa chache na zilitolewa kwa upendeleo kwa Watanzania wenye asili ya Asia.

Anasema Watanzania weusi walidhibitiwa kufanya biashara na kufanikiwa kwa sababu walihofiwa kama wangekuwa na fedha nyingi, basi wangehodhi siasa za nchi kutokana na nguvu kubwa kubwa ya kiuchumi ambayo wangekuwa nayo.

Anatolea mfano alipoanzisha kiwanda cha vinywaji baridi cha Bonite Bottlers (Coca Cola), kwamba mwaka 1987, Mwalimu Julius Nyerere alikikosoa kwa maelezo kuwa malighafi zake zilitoka nje, kwamba huo ulikuwa ubepari.

Mengi anasema, kiwanda cha Fahari Bottlers Limited, kilianzishwa mwaka 1983, Nyerere akiwa madarakani, kikawa kinazalisha bidhaa za Pepsi, alikiruhusu kwa sababu kilikuwa cha Watanzania wenye asili ya Asia na Nyerere hakukikosoa.

Ukimsoma Mengi, utaona kwamba matumaini ya kufanikiwa zaidi kibiashara ni baada ya Rais wa Pili, Ali Hassan Mwinyi, kuingiza sera za ulibelari na kuruhusu kila mtu afanye anachoweza ilimradi asivunje sheria. Hata hivyo, alilalamika kuwa kipindi cha Mwinyi bado Mwalimu Nyerere alikuwa na nguvu sana.

Kipindi cha Rais wa Tatu, Benjamin Mkapa, uliibuka mgogoro mkubwa kati ya Mengi na aliyekuwa Waziri wa Uwekezaji, Wilson Masilingi. Sababu ilikuwa uwekezaji wa Hoteli ya Kilimanjaro, sasa inaitwa Hyatt Regency, The Kilimanjaro.

Mengi alitaka kuwa mwekezaji wa hoteli hiyo, lakini alinyimwa, wakapewa wawekezaji kutoka nje. Mengi aliishambulia Serikali kwamba haikuwa ikiwapa kipaumbele wazawa, na kupendelea zaidi wageni. Haya ni malalamiko ya muda mrefu ya Mengi.

Aliamini kuwa wazawa wanapaswa kupewa kipaumbele katika fursa za uwekezaji ndani ya nchi. Hata pale wazawa wangekuwa na uwezo mdogo, Mengi aliamini kwamba lilikuwa jukumu la Serikali kuwawezesha kufikia viwango vinavyokidhi uwekezaji husika.

Kipindi cha Rais wa Nne, Jakaya Kikwete, mara kadhaa Mengi aliingia kwenye mgongano na mawaziri. Zipo nyakati alituhumiwa kuihujumu Serikali ya Kikwete. Aliyekuwa mbunge wa Mkuranga, Adam Malima, aliwahi kumsema Mengi bungeni kuwa alitumia vyombo vyake vya habari kujitangaza kuliko Rais.

Hoja hiyo ya Malima ilisababisha mzozo mkubwa bengeni, huku Mengi akisimama imara kujitetea. Televisheni ya ITV ilirudia taarifa za Mengi na Rais Kikwete kuonesha kwamba Malima hakusema kweli. Mengi pia alimwandikia barua Spika Samuel Sitta kulalamika. Mwisho Malima aliomba radhi.

Wakati wa Kikwete, ukatokea mzozo kati ya Mengi na aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Sophia Simba. Tuhuma zilitolewa na Sophia kuwa Mengi hakuwa mwana CCM na alikuwa anaihujumu Serikali, vilevile alimtuhumu kutaka kuwania Urais.

Mengi aliitisha mkutano na vyombo vya habari, akaonesha kadi zake za Tanu kisha ya CCM ya mwaka 1977. Akasema hajawahi kuwa na mpango wa kuwa Rais. Hata hivyo, ilikuwa dhahiri kwamba hakukuwa na kuaminiana kati ya Mengi na mawaziri wa Kikwete.

Uliibuka mvutano mwingine pale Mengi alipoitisha vyombo vya habari na kulalamika kwamba alipewa taarifa kutoka kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri, kwamba kuna waziri alipendekeza Serikali imfilisi Mengi mali zote.

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Laurence Masha, alimpa Mengi siku saba awe amethibitisha madai yake. Mengi akamjibu siku saba alizompa ni nyingi sana, kwamba siku moja ingetosha. Siku iliyofuata, mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, wakati huo akiwa mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alimtaja Masha kuwa ndiye alitoa wazo la kumfilisi Mengi kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri. Sakata hilo likaisha kimyakimya.

Hautasahaulika mzozo kati ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo dhidi ya Mengi. Mzozo ulihusu uwekezaji sekta ya madini na uvunaji gesi asilia. Muhongo alisema hakuna mzawa mwenye uwezo. Mengi aliamini wazawa wakipewa kipaumbele wataweza.

Aliwahi kufanya kikao na vyombo vya habari na kuelezea taarifa alizozipata ndani ya jeshi la polisi kuwa kulikuwa na mpango wa kumwekea dawa za kulevya mtoto wake ili kumkamata nazo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ili kuifanya jamii imuone yeye na familia yake ni wauza dawa za kulevya.

Mizozo hiyo ya mara kwa mara ambayo Mengi alikuwa nayo dhidi ya Serikali, na kwa kukumbuka kauli yake kwamba Watanzania wazawa (weusi), walianza kubaguliwa kwenye fursa za kiuchumi tangu wakati wa Nyerere, kwa hofu kwamba wangehodhi siasa na utawala, je, Serikali ilikuwa ikimuogopa Mengi au ilimchukia?

Pamoja na misimamo hiyo, Mengi aliwahi kuwa Mwenyekiti wa wa Bodi ya Magazeti ya Serikali (TSN), Kamishna wa Tume ya Mishahara (SRC), Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu Tanzania (NBAA), Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC), Kamishna wa Tume ya Kupambana na Ukimwi (TACAIDS) na kadhalika. Nafasi hizo zote ni za kuteuliwa na Rais. Amekuwa akiteuliwa tangu wakati wa Nyerere hadi Kikwete. Je, Serikali ilimpenda?

Mengi hakufurahia mfumo wa Serikali kujigeuza dereva wa biashara badala ya kuwaacha huru wafanyabiashara. Aliumia kuuawa kwa vyama vya ushirika. Alisema, vyama hivyo viliuawa ili kuwafanya Watanzania weusi wasiendelee na kupata nguvu kubwa ya kiuchumi. Kwamba wangehodhi siasa.

Aliamini kuwa Watanzania wenye asili ya Asia walipendelewa na Serikali. Takriban muongo mmoja uliopita, alitaja majina matano ya wafanyabiashara Watanzania wenye asili ya Asia kuwa wanafilisi nchi. Aliwaita mafisadi papa. Je, Mengi alikuwa mbaguzi? Hakuwapenda Watanzania wenye asili ya Asia?

Tumuombee Mengi pumziko jema. Kila mja ni wa Mwenyezi Mungu na kwake ndipo yalipo marejeo ya lazima.

Ndimi Luqman MALOTO
seriakali zote zilimpenda,iliyo[po ilimchukia na wakanza kwa kumkomoa kumnyima vitalu vya mafuta, kilimanjaro kempisky, wakamyima na Tanzanite wakajenga ukuta, huyu jamaa ana wivu sana na kumalizia ITV ikazuiwa kuonyesha habari za kichunguzi ambazo ndio kituo pekee watu wanakitegemea na sasa watu wamejhamia watsup video ambazo ni fupi fupi
 
Ukweli tangu tupate uhuru serikali zote hakuna ambazo zimewahi kumjali mfanya biashara mzawa mweusi. Zote zimekuwa zikiweka mazingira ya kupendelea wageni. Haya yaliyomkuta Mengi yanathibitisha hilo.

Ni wakati sasa serikali kuweka juhudi ya kuinua wafanya biashara wazawa wanaoweza kuja kuwa wachangiaji wakubwa wa uchumi kuliko hawa wahindi wanaweka hela Canada na Uswis
 
seriakali zote zilimpenda,iliyo[po ilimchukia na wakanza kwa kumkomoa kumnyima vitalu vya mafuta, kilimanjaro kempisky, wakamyima na Tanzanite wakajenga ukuta, huyu jamaa ana wivu sana na kumalizia ITV ikazuiwa kuonyesha habari za kichunguzi ambazo ndio kituo pekee watu wanakitegemea na sasa watu wamejhamia watsup video ambazo ni fupi fupi
Hayakuanza leo mkuu kama mleta mada alivyotafsiri
Hii inadhihirisha ubaya wetu na mfumo duni na hawa wanaendeleza na sasa sio kwa tajiri mzawa tu bali wanavyeka na matawi yote yanayoanza kuchipua kama wamachinga na mama ntilie
Yaani tunajua kwamba muuza ugoro hata siku moja hawezi kuwa na kiwanda cha kuweza ku pack ugoro na kuuza ulaya lakini unahakikisha anafunga biashara kwa 20000
 
Back
Top Bottom