Mukulu wa Bakulu
JF-Expert Member
- Aug 12, 2014
- 4,052
- 12,906
Serikali iliahidi kufika Novemba 2019 reli ya kiwango cha kati kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro ingekuwa imekamilika na kuanza safari ila hadi sasa hakuna maendeleo yoyote, ujenzi haujafika hata 70%.
Mwaka 2016 Serikali iliahidi kufikia 2020 nchi itakya na umeme megawati 5,000 na itaanza kuuza nje ila hadi sasa sidhani hata megawati 1500 tumefikisha. 2025 itafika hata megawati 3000 hatujafikisha. Naunga mkono mradi wa umeme mto rufiji.
Mwaka 2016 Serikali iliahidi kufikia 2020 nchi itakuwa ya viwanda, bado miezi 2 viwanda viko 4,000 kwenye makaratasi ila live havifiki hata 20.
Mwaka 2016 Serikali iliahidi itakua imehamia Dodoma once and for all, na kuuza Ikulu ya Dar es Salaam, hadi sasa serikali yote kivitendo iko Dar es Salaam, iko Dodoma kwenye makaratasi.
Je, Serikali yetu hii huwa inaamini kwenye miradi itakamilika kwa matamko? Kwanini inapenda kusema uongo wa wazi, au ukishakuwa kiongozi unaamini wote unaowaongoza hawana akili ila wewe?