W
Well said Mkuu, Tanzania tunaiatamia ardhi bila kufaidika nayo. Ardhi ina thamani kubwa kuliko madini, mbuga na viwanda. Pesa iliyotumika kuzuusha ukuta mererani sijui ingetosha kununua matrekta mangapi na kuyagawa kwenye vijiji. Chuo cha kilimo cha sokoine kimejaa wababaishaji ambao hawajalisogeza taifa mbele japo hata kwa sm 1. Tanzania ingeweza kuwa ghala la chakula katika ukanda Wa east and central Africa.
Hapo Mererani sidhani kama walitumia pesa nyingi sana sababu ni JKT ndio waliojenga huo ukuta. Btw hao hao JKT pia wanaweza kufundishwa mbinu sahihi za kilimo cha kisasa na wataalamu wa SUA (kuchagua mbegu, bora, Irrigation, how operate and repair tractors, mbolea sahihi, jinsi ya kupata masoko ya ndani na nje) wakitoka hapo wanaenda kuwafundisha wakulima nchi nzima.
Anyway it is not too late. Muhimu kuchagua vipaumbele sahihi vinavyoweza kulikomboa taifa na kuwasaidia watu wengi kwenye muda mchache.
Uwezo tunao wa kufanya mapinduzi kwenye secta ya kilimo tukijipanga vizuri na kuweka mikakati madhubuti, kiasi kwamba ndani ya miaka kumi tukawa ghala la chakula katika ukanda wa East, Central and Southern Africa na labda dunia nzima.
Mahitaji ya mazao ya kilimo yanaongezeka na yataongezeka sana tu duniani kutokana na kukuwa kwa idadi ya watu kila mwaka na kuongezeka kwa kipato kwa watu wengi duniani. Opportunities are immense.
Kwanza ni kufanya maamuzi, pili kupanga mikakati ya kufikia hayo malengo, tatu mipango madhubuti ya kutekeleza haya malengo.
Serikali inaweza kuwaalika wananchi, wataalamu na wadau wote wenye maoni jinsi ya kufikia na kutekeleza hayo malengo watoe maoni yao. Pia inaweza kujifunza kwa nchi nyingine kama Brazil, Argentina, India, Thailand, Japan, China, Russia, South Africa, Spain, Italy etc.
Serikali inaweza kutumia mitandao, kutengeneza website, kwa barua, emails, au uso kwa uso. Muhimu kuwasikiliza wadau wote na kuchukua yale mapendekezo mazuri zaidi. Inawezekana ni kujipanga tu.
Nimeangalia takwimu za UN kuhusu uzalishaji wa chakula Duniani Tanzania ni ya tano kwenye maharage, ya tatu kwenye viazi vitamu, ya pili kwenye katani hapo hata hatujaanza kujaribu. Je tukiamua kufanya kwa dhati, kiukweli tutafika wapi?
List of largest producing countries of agricultural commodities - Wikipedia