Ndugu zangu, Natoa taarifa za kusikitisha kuhusu Chuo cha Afya cha Saint Aggrey kilichopo jijini Mbeya, Mwanjelwa eneo la Sido. Chuo hiki kinatoa mafunzo katika kozi za Nursing, Clinical Medicine na Maabara katika ngazi ya Cheti. Chuo hiki kinaongozwa na familia ya Mwambusi chini ya Mkurugenzi wake Mboka Mwambusi. Chuo hiki kinaendeshwa bila kufuata mitaala, miongozo ya Wizara na Sheria na Kanuni zinazoendesha Vyuo vilivyopo chini ya Nacte pamoja na kuvunja Sheria za Nchi.
Mosi, kuhusu mitaala sisi wanafunzi wa clinical medicine mwaka wa 2 tunatakiwa kuwa tumepewa matokeo yetu ya Semista ya 1 ambayo iliisha April , lakini mpaka leo miezi 3 imepita Chuo kimeshindwa kutoa matokeo,na kwa sasa tupo Semista ya 2 bila kujua kama tunastahili ama la kutokana na kutokujua matokeo ya Semista iliyopita, kibaya zaidi imebaki mwezi mmoja kufanya mitihani ya Taifa.
Pia Chuo kimeshindwa kutupeleka katika Hospitali ili kujifunza kwa vitendo na tulipoamua kufuatilia kwa DMO na DC wa Mbeya Chuo kimefukuza wanafunzi wenzetu siku ya leo kwa kosa la kutokufuata taratibu.
Pamoja na kulipa ada takribani milioni tatu, Chuo kimeshindwa kusimamia taaluma badala yake kinatumia ubabe.
Kwa makusudi kabisa Chuo kinamtumia Dr. Stephen Muchina ambaye ni raia wa Kenya anayefanya kazi nchini bila kufuata taratibu kutufukuza bila kufuata taratibu za kisheria.
Kwa hiyo tunaomba Serikali kuchunguza Chuo hiki ambacho kinapoteza muda wetu, fedha za Wazazi masikini na kinadidimiza taaluma ya Afya kwa kutoa wahitimu wasio na ujuzi. Pia kuchukua hatua dhidi ya Mkurugenzi ambaye anatumia Chuo chake kama kichaka cha wahamiaji haramu wanaoishi na kufanya kazi nchini kinyume na Sheria.
Nawasilisha.