Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Ni maamuzi ya busara na Magumu ambayo Mheshimiwa Rais amechukua. Kufuta vibali vya kuagiza sukari nje ya nchi. Naam. Uamuzi wa kuagiza sukari nje ya nchi haukumnufaisha mwananchi bali ulitajirisha mabepari kama akina Mohamed Dewji. Ukweli ni kwamba gharama ya kuagiza mfuko mmoja wa kilo 50 wa sukari hadi unamfikia mfanyabiashara wa rejareja haizidi shilingi 60,000. Kwa hali hiyo, mfanyabiashara wa rejareja alipaswa kununua sukari kwa shilingi 1,200 kwa kilo moja. Hivyo kama anataka faida ya kawaida, bei ya sukari isingezidi shilingi 1,500 kwa kilo.
Hata hivyo, kwa vile waagizaji toka nje ya nchi ndio hao hao wanamiliki maduka ya jumla, kinachofanyika ni kwamba wanaagiza kwa gharama ndogo then wanauza kwa bei kubwa ili kupata super profit. Kibaya zaidi ni kwamba, waagizaji hao wa sukari nje ya nchi ndio hao hao wanunuzi wakubwa wa sukari ya ndani. Kwamba wao ndio wananunua sukari viwandani na kuuza kwa wananchi kwa bei ile ile ya sukari ya nje. Matokeo yake ni kwamba, hakuna utofauti wa bei ya ya sukari ya nje na ya ndani.
Baada ya uamuzi wa serikali, wafanyabiashara hao wakiongozwa na Mohamed Dewji wameanza mgomo wa kutaka kuishinikiza serikali kufuta uamuzi wake. Siku moja tu baada ya serikali kutangaza uamuzi huo, bei ya mfuko wa sukari ilipanda kutoka shilingi 70,000 hadi 80,000 na bei inaendelea kupanda ambapo mahala pengine mfuko wa sukari wa kilo 50 unauzwa hadi 90,000. Wamefanya hivyo si kwa sababu sukari imekuwa adimu, la hasha bali wanatengeneza mazingira ili ionekane kuwa kuna uhaba wa sukari nchini.
Rais wangu Magufuli, yanayoendelea kwenye sukari ni hayo hayo yanayoendelea kwenye soko la Saruji. Kuna waagizaji wa saruji nje ya nchi hasa Pakistani ambao ndio hao hao wanunuzi wa jumla wa saruji kwenye viwanda vyetu. Ukweli ni kwamba gharama halisi ya mfuko mmoja wa saruji kiwandani ni shilingi 7,890. Hata hivyo, kutokana na ukiritimba wa biashara hiyo, mwananchi hununua wastani wa shilingi 12,000 hadi 14,000. Bei hiyo ni kwa wale tu walio karibu na kiwanda cha saruji kama Mbeya, Tanga na Dar es Salaam.
Hata hivyo, ili kuhakikisha kuwa wafanyabiashara hawa wanaendelea kupata faida kubwa, wamefanya makubaliano na wenye viwanda. Kwamba, hakuna mwananchi ataenda kununua saruji moja kwa moja kiwandani na kama akienda atauziwa kwa bei ya rejareja. Lengo ni kuhakikisha kuwa siri hiyo haiwafikii wananchi.
Kwa upande wa saruji ya nje, mfuko mmoja wa saruji toka Pakistani mpaka unafika nchini haizidi shilingi 7,000. Na bei inakuwa chini ya hapo kama saruji hiyo itasafirishwa kwa njia ya unga yaani haijawekwa kwenye mifuko yake. Hata hivyo, kwa kuwa waagizaji wa nje ndio hao hao wanunuzi wa saruji za viwanda vyetu, unafuu huo wa bei haumfikii mwananchi. Matokeo yake Saruji haijawahi kushuka chini ya shilingi 12,000 ambapo kwa wale walio mbali zaidi kama huku kwetu Songea tunanunua mfuko mmoja wa saruji hadi shilingi 18,000 na ile saruji ya nje huuzwa hadi 19,000 licha ya gharama za kuagiza kuwa ndogo. Hoja zinazotolewa ni kuwa saruji hiyo ina kiwango kikubwa na bei ya kununulia ipo juu ijapokuwa hawatuelezi wananunua kwa kiasi gani.
Kinachouma zaidi hata ile saruji ya Kiwanda kikubwa barani Afrika, Dangote nayo inauzwa kwa bei ya juu sana ambapo tumeambiwa kuwa inauzwa shilingi 13,500 kwa Mtwara. Kama Mtwara inauzwa bei hiyo, ni dhahiri kwamba watanzania watanunua mfuko mmoja wa saruji ya Dangote hadi shilingi 20,000.
Sasa swali la kujiuliza, ni nini basi faida ya kuwa na viwanda vingi ilhali bei inabaki ile ile? U wapi ushindani wa biashara kama wanunuzi wa saruji viwandani ni wale wale wanaoagiza nje ya nchi? Kwa nini basi viwanda visiwe na utaratibu wa kuuza saruji kwa wananchi moja kwa moja badala ya biashara hiyo kuwaachia watu wa kati ambao ndio wanyonyaji wakubwa? Kwa nini basi wasifungue maduka yao kila wilaya ili mwananchi apate nafuu? Ni nini kinawashinda?
Mheshimiwa Rais, ukweli ndio huu. Ukitumbua majipu haya kisawasawa hakika nchi hii itasonga mbele kwa kasi ya ajabu. Dangote alikuwa tayari kuuza saruji kwa shilingi 8,000. Ila haya manyang'au yamemzunguka na kujikuta akiuza saruji yake kwa bei kubwa kuliko hata wanavyouza Twiga, Simba, Camel, Rhino, Nyati nk. Je tutafika?