Serikali iangalie jambo hili

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,594
20,753
Baada ya kufungwa kwa maduka maarufu yanayojulikana kama Bureau de Change nchini, huduma ya kubadirisha fedha imepewa nguvu na watoa huduma za kibenki kwa sasa.

20191125_093851.jpg

Kwa utaratibu uliozoeleka hapa nchini kama si duniani, benki nyingi zinafanya kazi siku 5-6 kwa siku ukiondoka siku ya jumapili ambayo ni siku ya mapumziko.

Katika sehemu kadhaa nilizopita au kufika nimeona huwezi kupata huduma ya kubadirisha pesa za kigeni kupata Tshs kwa siku za mwishoni mwa juma kutokana na benki nyingi kufunga huduma.

Kwa jinsi dunia inavyosonga siyo vibaya kuweka dirisha maalumu kwa siku za mwisho wa wiki, vinginevyo benki na serikali mtakosa fedha hii kwa kiasi kikubwa ikizingatiwa mwisho wa wiki matumizi ya pesa huwa maradufu.

Serikali na watoa huduma za kibenki mliangalie hili na Ikiwezekana ziwekwe ATM za kuweza kufanya muhamala wa kubadirisha fedha.
 
TODAYS,

Lakini hata kabla ya zoezi hilo BD nyingi tena zenye exchange rate nzuri kule mitaa ya Samora na Kisutu, Jamhuri nk zilifungwa Jumapili isipokuwa chache kule Kariakoo, lakini baadhi ya Banks kama CRDB na TPB wana matawi yapo wazi Jumapili katika miji mikubwa, sijui mkuu unaandika kutokea mji gani.
 
Nimekuwa Mwanza, Zanzibar na Sasa Arusha.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom