Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,169
- 48,451
Kimsingi Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania haitokani na Serikali yenyewe bali inatokana na wananchi.
Watanzania ndiyo wenye Serikali na siyo Serikali ndiyo inawamiliki watanzania. Serikali inawajibika kwa Watanzania na watanzania wanawajibika kwa sheria za nchi na baadhi ya yaliyomo kwenye Katiba ya JMT.
Na ndiyo maana wanasiasa wamewekewa kwenye Katiba kuwepo madarakani kwa miaka mitano, watumishi wa Umma wanaruhusiwa kufanya Kazi mwisho miaka sitini na baada ya hapo wanatakiwa kustaafu Kazi.
Lakini hakuna muda wa mwisho wa Mtanzania kuwa Mtanzania.
Kwa hivyo, Maelekezo, maonyo, mazuio, makatazo yoyote yanayotolewa na waliomo serikalini KINYUME cha Katiba na sheria za nchi, bila ya kujali vyeo walivyo navyo, ni BATILI.
Kwa mfano watanzania wanao Uhuru wa kujieleza unaolindwa na Katiba. Mtanzania hazuiwi na Katiba anapotaka kuelezea hisia zake. Na Serikali haina haki ya kulazimisha hisia zake ndiyo ziwe hisia za Watanzania.
Kwa mfano kwa kuwa hakuna kipimo cha kisayansi kuthibitisha wanaokufa kama wanakufa kwa COVID 19 au la, basi wananchi wanaohisi ndugu zao wamekufa kwa COVID 19 wasizuiwe kueleza hisia zao hizo kwamba ndugu zao wamekufa kwa COVID 19.
Kama Serikali inataka Watanzania waache kutumia hisia kwenye kuelezea vifo vya ndugu zao vinavyotokea sasa, basi Serikali itumie vipimo vya kisayansi kupima CORONA.
Maana tangu Mheshimiwa Rais aseme vipimo vilivyokuwa vinatumiwa kupimia CORONA ni FEKI, Serikali haijawahi kusema kama imeagiza vipimo vingine.
Kwa ivo inawezekana na Serikali nayo haina uhakika kama wanaokufa nao wanakufa kwa COVID 19 au la.
Ili wananchi waache kuhisi ndugu zao kama wamekufa kwa CORONA, ni LAZIMA Serikali Sasa ianze kupima wagonjwa wote wanaohisiwa kuwa wamembukizwa COVID 19.
Kinyume cha hapo serikali itakuwa inahisi tu kuwa wanaokufa hawafi kwa COVID 19 haki ambayo wananchi nao pia wanayo ya kusema kuwa ndugu zao wanakufa kwa COVID 19.