Serikali iachane na Elimu Bure, ni gharama sana!

Serikali iachane na Elimu Bure, ni gharama sana!

mafwitanda

Member
Joined
Jul 10, 2016
Posts
58
Reaction score
29
Elimu bure inaigharimu sana serikali. Kila mwezi serikali inagharimia tsh bil 18 kwa shule zote za serikali. Hii ni gharama kubwa na inawezekana baadhi ya mambo hapa nchini hayaendi kama vile ajira mpya kwa walimu; kupanda madaraja, nyongeza ya mishahara na boom kutofika kwa wakati.

Ushauri kwa mujibu wa Plato na wanafalsafa wengi wanasisitiza elimu sharti ichangiwe ili wanafunzi na wazazi waone uthamani wa elimu.

Pili ni vema serikali iachane na zoezi hili la elimu bure kama walivoacha ada elekezi kwa shule binafsi.

Tatu, ili kuongeza mapato serikali ianzishe mgodi wa kuchimba madini unomilikiwa na serikali kama serikali za kikoloni zilivoanzisha mashamba ya serikali za kikoloni wakati wa mdororo wa uchumi 1929-1933.

Karibuni kwa michango.
 
Mwacheni think tank wa tz anajua tutakapoamkia kesho; he knows where we gonna be by tomorrow. He needs no any advice from any person.
 
Mleta Uzi uko sahihi, lakini je wewe ni Profesa, Dr, MHANDISI Hata wa vibatari? Kama hauko kwenye kundi moja wapo, usihangaike kusema unapoteza muda huwezi sikilizwa NCHI hii. Kasome kwanza upate japo PhD Hata ya wadudu ndio uje ushauri
 
Kwani hata hao wenye sifa za kushauri wanashauri na wanasikilizwa?
 
Kiranja alisema huwa anapitia humu JF ni jambo la kheri akipita na akakuta ushauri huu...akauzingatia...
 
Elimu bure inaigharimu sana serikali. Kila mwezi serikali inagharimia tsh bil 18 kwa shule zote za serikali. Hii ni gharama kubwa na inawezekana baadhi ya mambo hapa nchini hayaendi kama vile ajira mpya kwa walimu; kupanda madaraja, nyongeza ya mishahara na boom kutofika kwa wakati.

Ushauri kwa mujibu wa Plato na wanafalsafa wengi wanasisitiza elimu sharti ichangiwe ili wanafunzi na wazazi waone wathamini elimu.

Pili ni vema serikali iachane na zoezi hili la elimu bure km walivoacha ada elekezi kwa shule binafsi.

Tatu, ili kuongeza mapato serikali ianzishe mgodi wa kuchimba madini unomilikiwa na serikali km serikali za kikoloni zilivoanzisha mashamb ya serkal za kikoloni wakati wa mdororo wa uchumi 1929-1933.

Karibuni kwa michango.

Naunga hii hoja kwa asilimia kubwa. Kuendelea kuwa na elimu bure Tanzania imewafanya wanaofaidika wasiwe accountable anaona hana la kupoteza. Kama ingekuwa amejigharamia, au walimkaramia wangewapushi wasome kwa bidii na ingesadia kuongeza hata uelewa wa wanafunzi in a process.

Wengi mtawaza Zaidi, iweje, ila nafikiri sio lazima kila mtu apite hii formal education Zaidi ya kusoma madarasa ya kujua kusoma na kuandika, Elimu ya msingi ipewe kipaumbele na gharama iwe chini ili iwe affordable kwa kila mtu, wanafunzi wapewe maarifa muhimu, content zote zisizo na manufaa katika level hii haziitajiki.

Baada ya hapo viwepo vyuo vya ujuzi ili watu wapate ujuzi wajitafutie maisha na ajira mapema, wale waliotaka kuendelea na shule Zaidi na Zaidi ndio wakitwe huko na wagharamikie ili wasome kwa bidii, la sivyo tutabeba Zaidi wanafunzi wa kuchora watu na kuandika nyimbo kwenye mitihani yao.
 
Hilo halitawezekana kwasababu kwanza hiyo ya elimu bure wamelazimshwa na ndio maana sometime mambo hayaendi sawa.

Kuna nchi moja ya ulaya ilikua inaida tanzania pesa nyingi sana kwahiyo lile deni ikasamehe kwa kwa mashaliti wakasema tanzania wafute ada shuleni ili wawe welipana kihivyo.
 
Kiliochangu uko sahihi...kwa utafiti Mdogo tu kwa baadhi ya wakuu wa shule na wanafunzi hawaafiki suala hili la elimu bure...kwa SBB za kuchanganya wananchi baadhi ya mikoa na wilaya hawakufanya mitihani ya Mock kisa elimu bure hakuna wa kuchanga...tinaenda wapi?
 
Erasto kumbeeee hiki kimbembe kwa hiyo deni likiisha watarudisha ada
 
Naunga hii hoja kwa asilimia kubwa. Kuendelea kuwa na elimu bure Tanzania imewafanya wanaofaidika wasiwe accountable anaona hana la kupoteza. Kama ingekuwa amejigharamia, au walimkaramia wangewapushi wasome kwa bidii na ingesadia kuongeza hata uelewa wa wanafunzi in a process.
Wengi mtawaza Zaidi, iweje, ila nafikiri sio lazima kila mtu apite hii formal education Zaidi ya kusoma madarasa ya kujua kusoma na kuandika, Elimu ya msingi ipewe kipaumbele na gharama iwe chini ili iwe affordable kwa kila mtu, wanafunzi wapewe maarifa muhimu, content zote zisizo na manufaa katika level hii haziitajiki. baada ya hapo viwepo vyuo vya ujuzi ili watu wapate ujuzi wajitafutie maisha na ajira mapema, wale waliotaka kuendelea na shule Zaidi na Zaidi ndio wakitwe huko na wagharamikie ili wasome kwa bidii, la sivyo tutabeba Zaidi wanafunzi wa kuchora watu na kuandika nyimbo kwenye mitihani yao.
Sera ya bure kabisa kwa maana ya bure kwa dunia ya leo, imepitwa na wakati. Ila kuwasaidia wananchi ni jambo jema.

Kuna mleta uzi mmoja alikuja na nadharia moja iliyotumiwa na professor mmoja huko Ughaibuni aliyeamua kufundisha kwa vitendo madhara ya nadharia za Ujamaa na Equality. Kwamba wanafunzi walifanyiwa Standardization kwenye pass mark. Lakini kila awam walijikuta wakiporomoka hadi darasa zima likaishia kupata zero baada ya majaribio kama ya awamu tatu/nne hivi.

Nadharia ya Elimu bure inaangukia kwenye nadharia ya Ujamaa ambayo siyo jambo baya lakini kwa dunia ya sasa ni China pekee wameweza na kufanikiwa. Wengine wote wameshindwa!
 
Mock mkoa wa Dar imeshindwa kusahihishwa, wanafunzi wa serikali hawajatoa mchango. Private wametoa. Hapa kazi tu
 
Lakini watanzania sijui no watu WA namna gani elimu imekuwa bure tunaona haifai ,elimu ikiwa ni kulipia napo nikulaumu tu.Wananchi wengi tunafurahia elimu kwani sasa visingizio vya kutopeleka mtoto kwa kukosa ada vimekwisha safi sana MHESHIMIWA RAIS.
 
Mchumi nina imani kuwa tukitazama Leo na kesho elimu bure nisafi ila baada ya miaka mitano madhara ni makubwa sana...
 
Chaza nadharia ya ujamaa iliisha rasmi 1990 Leo tukiifuata hatutafiki mbali...
 
Elimu bure inaigharimu sana serikali. Kila mwezi serikali inagharimia tsh bil 18 kwa shule zote za serikali. Hii ni gharama kubwa na inawezekana baadhi ya mambo hapa nchini hayaendi kama vile ajira mpya kwa walimu; kupanda madaraja, nyongeza ya mishahara na boom kutofika kwa wakati.

Ushauri kwa mujibu wa Plato na wanafalsafa wengi wanasisitiza elimu sharti ichangiwe ili wanafunzi na wazazi waone uthamani wa elimu.

Pili ni vema serikali iachane na zoezi hili la elimu bure kama walivoacha ada elekezi kwa shule binafsi.

Tatu, ili kuongeza mapato serikali ianzishe mgodi wa kuchimba madini unomilikiwa na serikali kama serikali za kikoloni zilivoanzisha mashamba ya serikali za kikoloni wakati wa mdororo wa uchumi 1929-1933.

Karibuni kwa michango.

Mafwitanda!
Uko sahihi ! Tatizo kubwa la JPM na watu wote wanaoongoza Serikali ya awamu ya tatu wamekurupuka as if tumepata uhuru Mwaka jana 2015 au tulikuwa vitani. Ukweli ni kwamba Serikali ni ile ile ya CCM kilichobadilika ni JK kumkabidhi JPM aongoze. Kwa sababu amepaniki na hakuwa na mission wala strategy ya kuingia Ikulu alidandia sera ya Elimu bure bila ya kufanya a detailed feasibility studies to identity stakeholders as well as risks and the magnitude of the problem. The intervention of just starting with massive enrollment bila kujua challenges is the core problem. Kazi ya Elimu ni mtambuka it requires alignment of stakeholders. Miaka ya nyuma enzi za Mwalimu we attempted to provide free education and we all know how the system collapsed. Bila ya kujifunza kutokana na makosa Serikali ya awamu ya Tano inaingia Mkenge and here we have a serious problem. Tumeandikisha wanafunzi Mara hakuna madawati , tukipata madawati tutajikuta hakuna madarasa and mind you inabidi kuwepo na gradual increase in terms of teachers and classrooms , tutakuwa hatuna walimu and later on no enough vyoo, hakuna mkataba , hakuna maabara and so on and so on na mwishowe maaeneo ya kujenga hayatoshi. Nawahakikishia bila ya ushiriki wa Wazazi and the public in general kutoa Elimu bure is a day dream take whether you like it on not! Wazazi wakilipa watakuwa na ownership ya Elimu and they will by default follow up on quality and that children do their homework and get support including food and uniforms and another requirements. You can continue filling the list and this is not nuclear science. Huu Mwendokasi it's just mbio za sakafuni kwani huishia ukingoni! Mambo ya kufanywa na Serikali yanajulikana don't try to what should be done by the wananchi! Mnapiga marufuku michamgo and then akina Makonda wamchangisha fedha za madawati! Why the confusion? Let us take time and learn from past mistakes? Huko kote mmejaza watu wenye Ph.D. everybody has a Ph.D. unafikiri Ph.D. Holder anatakiwa afanye nini kwa mfano?
 
Back
Top Bottom