Serikali huwa inakuwa wapi

egari

Member
Jan 3, 2017
40
37
Unakuta raia wakulima na wafugaji wamevamia hifadhi mfano Ruaha Mbeya, Katavi Rukwa, Pori la Tabora, Serengeti Simiyu.., unakuta wanavamia na kuanza shughuli za kibinadam kwa mda hata wa miaka kadhaa na vingine hujengeka na kuwa vijijini. Cha kushangaa ni pale serikali inapoanza kuwafukuza kwa kuwachomea moto nyumba zao, mazao na kukamata mifugo yao kwa kuwaita wavamizi.., cha kujiuliza hapa serikali huwa inakuwa wapi mwanzon kabisa raia hawa wanapovamia.
 
tatizo ni wananchi.
unadhani huwa hawafahamu kama ilo eneo either ni pori tengefu, hifadhi au ni pori la akiba. sema tu wananchi huwa tuna test kwanza tukizani serikali itakaa kimya milele.
 
Ni kutowajibika tu kuanzia ngazi za vijiji,wilaya,mkoa hadi Taifa,lakini pia elimu yapaswa kutolewa kwa jamii ili kulinda misitu/hifadhi na umuhimu wake kwa jamii..
 
Hapa tutailaumu serikali kwa kutokuwajibika. Najaribu kuwaza tu kwa sauti, sisi wenyewe wananchi tunatimiza wajibu wetu ipasavyo katika maeneo yetu?
 
Back
Top Bottom