Serikali hebu fanyieni kazi hii kitu

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,096
22,621
Katika ulimwengu wa biashara kuna vitu viwili ambavyo vinafanana ila si kitu kimoja.....navyo ni HATI MILIKI na HAKI MILIKI.

Kwa haraka haraka tu, HATI MILIKI hudili na umiliki rasmi wa uvumbuzi wa kitu chochote ambacho huweza kutumika aidha kumletea mtu heshima katika jamii yake ama faida na tija ya kibiashara.
Kwa mfano ukibuni kinywaji ambacho hakikuwahi kuonekana popote na ladha yake ni mpya na wewe ndiye mvumbuzi, basi wewe ndiye unayeshikishwa hati miliki ya uvumbuzi wa hicho kinywaji na pia mtu yoyote hataruhusiwa kukitengeneza bila wewe kumpa kibali au kumruhusu iwe ni bure au kwa malipo.

Kwa upande mwingine, HAKI MILIKI hudili na haki ya kuhusika na uvumbuzi wa jambo au kitu fulani. Nitatumia mfano wa hapo juu kufafanua nini maana ya haki miliki.
Kwa mfano aliyevumbua hicho kinywaji hapo juu ni mzazi wako au ni ndugu, rafiki, jamaa, mpenzi, au mtu yeyote ambaye mnaukaribu wa kuweza hata kukurithisha mali yake. Then ikatokea huyu mtu akiwa bado hai au amefariki akaamua kukupatia ile hadhi na mamlaka ya umiliki, wewe sasa unakuwa na haki miliki......kwa maana kuwa mamlaka yako juu ya kile kinywaji hayajatokana na weww kukivumbua ila ni kwasababu umehamishiwa Hati miliki toka kwa mvumbuzi kuja kwako ambaye haujavumbua.

Kwann nimeleta hilo somo hapo juu japo kwa ufupi. Lengo ni kutaka kuhoji maendeleo ya ujasiliamali tanzania na namna gani serikali ushirika wake ni mdogo sana huku kila siku wakitoatoa macho na matamko hewa juu ya swala la ajira.

Ningependa kuwajuza kuwa hakuna taifa linaweza fikia kasi nzuri ya maendeleo kama linakuwa linakwenda na sera mbovu kuhusiana na mfumo wa sekta binafsi. Sisi Tanzania ni miongoni mwa mataifa yenye sera mbovu serikalini juu ya sekta binafsi maana sera za serikalini juu ya shughuli za kampuni, taasisi na biashara za watu binafsi ni za ajabu na sio zenye mlengo wa maendeleo na hadi leo sijajuia nani huzitunga.

Mojawapo ya cornerstone ya kuleta maendeleo katika sekta binafsi ni sheria na taratibu kali juu ya Hati na haki miliki za wajasiria mali. Kwa maana akili waliyotumia katika uvumbuzi, thamani waliyoleta au kuongeza, na jitihada zao kwa ujumla haviwezi kupimwa kirahisi na hivyo wanatakiwa kuwa na last say juu ya uvumbuzi wao hata kwa namna wanavyoona inakuwa fair kuwalipa. Leo hii tanzania kuna watu wengi huwa wanabuni aina fulani ya biashara anatokea mtu out of no where anacopy bila kujua ni kosa kisheria na kibaya zaidi anacopy na anafanya kitu hicho hicho mtaa wa pili hapo hivyo basi mbali na kuharibu tu tija ya kile kitu kumfikia mbunifu, hii hali huvunja kabisa mzuka wa watu wenye akili za ubunifu kubuni vitu vipya kwa kuhofia kukopiwa na wao kutopata tija yoyote.

Sijajua kama serikali wanatambua hili kupitia watalaamu wao ila huku mitaani kuna watu huwa wanajitahidi sana kubuni vitu vidogo vidogo lakini wanashindwa kuviendeleza kwa hofu ya mawazo yao kuibwa, pia kukosa pesa za kufanyia hilo wazo. Imagine una idea nzuri ambayo ili ifanyike kwa level za kimataifa wake ni milioni kuanzia 50 halafu wakati huo wewe unaamua kuifanya kibishi kwa kuanza na milioni 5, sasa kuna watu huwa wanapesa but kubuni idea hawapo vizuri ila wako vizuri kwenye kunyapia na kuendeleza idea za watu, wanakuja wanacopy wazo lako na kulifanyia kazi bila kukuconsult kwa lolote.

Kuna mengi huwa yanatokea ila ningependa tu wadau tulitambue hili swala na tulijadili kwa kina kwa maana ni mojawapo ya changamoto ya maendelo ya sekta binafsi.

Kwa wale ambao mtauliza hii kitu itasaidia nini, hebu tazameni watu kama wa akina AY na Mwana FA wamesimamia hizi hizi sheria finyu zilizopo na wamelipwa mafao yao kabla hata ya uzee kuwafika wameshapata mafao yao ya zaidi ya Shilingi Bilioni 2.5 za kitanzania hela ambayo baadhi yetu hatutaishika hata kidogo......




SONY Xperia Z5 Premium
 
Hahahah ushindani ni lazima mkuu, don't hate the player hate the game!

Kwa kuingatia taaluma ya ujasiriamali tunapendekeza ubuni biashara ambayo haitakuwa rahisi kufanyiwa immitation.CREATIVITY... Patner!

Ni ngumu kuanzisha biashara usipate mshindani kibongo bongo, soko ni huru na hata kulalamika haitasaidia. Kuwa mbunifu zaidi ndio silaha tosha. Andaa formula ambayo itakuwa ngumu watu kuiga! Ingia sokoni...biashara ikikubali umetoka.

Ila kwa idea zetu za biashara cheap kama udalali, ulanguzi unategemea utakuwa pekeyako au duka na biashara ya pikipiki.
 
Hahahah ushindani ni lazima mkuu, don't hate the player hate the game!

Kwa kuingatia taaluma ya ujasiriamali tunapendekeza ubuni biashara ambayo haitakuwa rahisi kufanyiwa immitation.CREATIVITY... Patner!

Ni ngumu kuanzisha biashara usipate mshindani kibongo bongo, soko ni huru na hata kulalamika haitasaidia. Kuwa mbunifu zaidi ndio silaha tosha. Andaa formula ambayo itakuwa ngumu watu kuiga! Ingia sokoni...biashara ikikubali umetoka.

Ila kwa idea zetu za biashara cheap kama udalali, ulanguzi unategemea utakuwa pekeyako au duka na biashara ya pikipiki.
Nadhani haujaelewa vema concept ya fair competition........usije ukafananisha ushindani ninaouzungumzia mimi na ule wa pepsi na cokacola......maana ni vitu tofauti.


Wewe unaozungumzia ni ule ushindani kuwa mimi nimetengeneza juice ya passion kavu nauza na keki wewe ukaja na kitu yako ambayo imeboreshwa.... say....juice ya passion yenye mchanganyiko wa vanilla flavour na grape colour halafu na chocolate.....thats fair competition...... But nimegundua ugali wangu wa kutumia unga wa ubuyu na wewe umekuja kufanya kazi kwangu ukajifunza kesho ukanitoroka ukafungua biashara hiyo hiyo kwa kutumia ujuzi ulioupata kutoka kwangu hiyo sio fair competition hata kidogo.......

Rejea kesi ya kampuni ya apple na samsung juu ya kuibia designing ya tablet kutoka kwa Ipad.

SONY Xperia Z5 Premium
 
Nikweli hili in tatizo, Hii inatokana na udhaifu wa kujua tafsiri sahihi kwa valiopewa mamlaka. Wanadhanisoko huria ndio solo holela. ni vena solo huria isaidie kuleta Tija na sio kuwa holelacbila kulinda maslahi ya mmiliki. Au no makusudi mbona wasanii Nazi zao zinajulikana na kulindwa kwanini Nazi za Wajasiliamali Nazi zao zinapuuzwa. Tunatakiwa tujitafakari Watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikweli hili in tatizo, Hii inatokana na udhaifu wa kujua tafsiri sahihi kwa valiopewa mamlaka. Wanadhanisoko huria ndio solo holela. ni vena solo huria isaidie kuleta Tija na sio kuwa holelacbila kulinda maslahi ya mmiliki. Au no makusudi mbona wasanii Nazi zao zinajulikana na kulindwa kwanini Nazi za Wajasiliamali Nazi zao zinapuuzwa. Tunatakiwa tujitafakari Watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umetofautisha vema na vizuri kabisa........

Kuna SOKO HOLELA na SOKO HURIA.Hivi ni mafuta na maji kwa maana ya vitu viwili tofauti. Huwezi kufanya biashara kiuweledi katika soko holela ila inawezekana katika soko huria.

SONY Xperia Z5 Premium
 
ni kweli mkuu mleta mada.miaka ya 90 kuna nzee mmoja hapa Dodoma aliyeitwa MUNUO.Alianzisha "CHAMA CHA KUTETEA HAKI ZA WANAUME"Akajitangaza na kukitangaza chama hiko WAJANJA WALIPO KIPATIA NAFASI WAKAKISAJILI NA KUKIMILIKI ILHALI MUANZILISHI AU MBUNIFU HAKUFAIDIKA NA WALA HAFAIDIKI KWA LOLOTE!
 
Back
Top Bottom