Serikali haitawanyang'anya walionunua viwanda vya umma

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,738
3,198
Serikali imesema haina mpango wa kunyang'anya watu walionunua viwanda vilivyokuwa vya umma badala yake ina lengo la kuvisaidia ili vizalishe kwa tija.

Moja ya mkakati wao kwa mujibu wa Waziri Mwijage ni kushughulikia viwanda vinavyosuasua na vilivyofungwa ili kujua sababu zilizosababisha hali hiyo na kuitatua.

My take: Kauli ya waziri inakinzana na ahadi za Magufuli wakati wa kampeni,yeye alisema vitataifishwa na serikali visivyofanya kazi.

Pia ni aibu kwa waziri kueleza kuwa hajui sababu za baadhi ya viwanda vilivyouzwa kufa! Kuna ripoti mbalimbali zimeandika namna baadhi ya viwanda vilivyohujumiwa na hao wamiliki mpaka wakauza hata mashine walizozikuta humo!

Leo hii uwe na mkakati wa kuwasaidia wezi kama hao? wengine hata aina ya bidhaa wanazozalisha wamebadili bila utaratibu.Wengine wamegeuza maeneo ya viwanda ni PUB na maghala.

Uzwazwa huu watanzania tutaelea kwenye umaskini wa wasiokuwa nacho kwa miaka mingi tukiwa na viongozi aina ya Mh. Mwijage.
 
makubwa mpaka tufike 2020 tutakua tumeona na kusikia mengi
leo wameanza kugeukana
 
Kuna mawaziri bado hawajamuelewa Magufuli, hao siku zao zinahesabika maana alisema tuwape muda mawaziri wafanye kazi
 
Ingekuwa mtu ukisema tu kitu kinakuja chenyewe basi tungekuwa mbali sana. Haya mambo yanahitaji mikakati.
 
Kadiri siku zinavyokwenda mizuka inapungua watu wanarudi kwenye uhalisia!!
 
Kuna mawaziri bado hawajamuelewa Magufuli, hao siku zao zinahesabika maana alisema tuwape muda mawaziri wafanye kazi
Waziri anapotoa contraadicting statement inaleta shida juu ya dhamira ya serikali kuleta maendeleo.
 
Back
Top Bottom