Serikali Haina Msimamo wa Katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali Haina Msimamo wa Katiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jun 28, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Makamo wa Bili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi
  [h=3][/h]


  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema haina msimamo na wala haiwezi kuwashawishi wananchi wakaseme nini katika tume ya kuratibu na kukusanya maoni ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Kauli hiyo imetolewa jana Makamo wa pili wa rais, Balozi Seif Ali Iddi alipokuwa akitoa ufafanuzi wa masuala mbali mbali ya katika kikao cha baraza la wawakilishi Njini Zanzibar. “Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haina maoni wala haina msimamo kwa wananchi wake kuhusu katiba mpya na pia hatuwezi kuwashawishi wananchi wala kuwaandaa utaratibu maalumu wa suala hilo…. maoni ya wananchi yatakuwa ndiyo ya mwisho na yataheshimiwa tunawataka wawakilishi muwaongoze wananchi wakatoe maoni yao katika tume” alisisitiza Balozi Seif
  Aidha aliwatumia lawama wajumbe wa baraza hilo katika suala zima la katiba kutokana na kushindwa kutoa elimu katika majimbo yao na badala yake kuwaachia watu wengine kuwapotosha wananchi. “Serikali haina maoni lakini sisi tuliopo hapa ndio twende kwa watu kwa sababu wajumbe wa baraza hili wamechaguliwa na watu huko majimbo kwani hivyo nyinyi muwawakilishe wananchi katika suala hili muwaelimishe wananchi wenu majimbo lakini msiwapotoshe ….” Alisema.

  Na kuongewa kwamba “Tena tunawaomba sana wawakilishi muwe mnawakusanya wananchi majimboni mwenu kuwapa elimu wananchi kwa sababu naamini mpaka sasa hakuna hata mwakilishi hata mmoja aliyewaita wananchi wake jimboni na kuwaeleza suala hili la katiba” alisema.
  Alisema hilo ndilo lengo na majukumu ya wajumbe wa baraza la wawakilishi kutoa elimu kwa wapiga kura wao zaidi katika suala la muungano ikiwemo faida zake, matatizo yake na faida ikiwemo na madhara ya kuvunjika muungano.
  “Huo ndiyo wajibu wa wajumbe wa baraza la wawakilishi katika majimbo ya uchaguzi……kutoa elimu kwa wananchi kuhusu muundo wa Muungano na faida zake na hata hasara ukivunjika lakini msiwasemee nyinyi waacheni wenyewe waseme” alisisitiza balozi Seif.
  Makamo wa pili wa rais alisema serikali katika suala la katiba limetoa fursa kubwa kwa kuwapa wananchi uhuru wa kutoa maoni kwa njia za salama na kuonya kwamba serikali haitamvumilia mtu ambaye atakwenda kinyume na sheria za nchi.
  Kauli ya Balozi Seif imekuja kufuatia maombi ya baadhi ya wawakilishi walipokuwa wakichangia bajeti ya wizara yake ambapo pamoja na mambo mengine waliitaka serikali kutoa muongozo na msimamo wa pamoja kuhusu katiba mpya ili wananchi wasiweze kubabaika waktai wa kutoa maoni katika tume itakapoanza kukusanya maoni mwanzoni mwa wiki ijayo.
  “Sio kazi ya serikali kuwashawishi wananchi kuhusu Muungano na kutoa maelekezo yake mbele ya Tume ya marekebisho ya katiba kwani tunaamini suala hilo serikali inawaachia wenyewe wananchi kutumia fursa ya demokrasia kuamua mfumo wanaoutaka wa serikali” alisema Balozi Seif.
  Akizungumzia suala la elimu kwa wananchi Balozi Seif alisema wananchi wa Zanzibar wanao ufahamu mkubwa kuhusu suala zima la katiba na kuzitambuwa kero mbali mbali ziliomo katika Muungano ambazo zimekuwa kikwazo kwa maisha yao hivyo hawahitaji kupewa muongozo na serikali.
  Akionesha kukerwa na badhi ya watu wanaotumia kampeni ya kukusanya saini za watu kukataa muungano, alisema anapinga kampeni hiyo na kuwataka wananchi waache tabia hiyo na badala yake wajitayarishe kutoa maoni wakati tume itakapofika kuwahoji wananchi.
  “Naomba nitoe wito kwa wale wenye kupita kila nyumba usiku na kukusanya saini za watu wakatae muungano naomba waache tabia hii mara moja na wasubiri tume wende wakatoe maoni yao” alisema Balozi.
  Alisema tabia hiyo sio nzuri ya kuwasemea watu ambayo inadumaza demokrasia iliopo na kuwataka wananchi waache kufanya hivyo kwani kila mmoja atapewa fursa ya kusema mwenyewe na na hakuna sababu watu kuzungumza na niaba ya wengine.
  Akifafanua mambo mengine alitaja masuala ya migogoro ya ardhi kuwa bado yanaendelea kuisumbua serikali lakini aliahidi kuendelea nayo na kamwe serikali haitasita kuchukua hatua za makusudi katika kukabiliana na matatizo hayo.
  Aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba migogoro ya ardhi kwa kiasi kikubwa imechangiwa na viongozi lakini utatuzi wa migogoro hiyo bado inaendelea na sio kweli kama walivyosema baadhi ya wajumbe kwamba nguvu ya soda ambapo alisema utatuzi wake unahitaji busara za hali ya juu kwani matatizo hayo yameanzia ngazi za juu hadi chini.
  Alisema migogoro ya ardhi ni moja ya tatizo ambalo limekuwa likiisumbuwa Serikali akiwemo rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Sheni ambaye amelivalia njuga kulipatia ufumbuzi wake kwa kuwataka wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya na watendaji wengine kulishungulikia katika ngazi za chini.
  “Dawa ya migogoro ya ardhi ipo wala mimi sijavunjika moyo….lakini Serikali inalifanyia kazi tatizo hilo kuona kwamba ufumbuzi wake unapatikana, kwani tukumbuke tatizo hili linahitaji busara katika utatuzi wake” aliwaahidi wajumbe hao.
  Hata hivyo alisema amepata moyo na matumaini makubwa kwamba baadhi ya maeneo yameanza kupata ufumbuzi wa kero hizo zinazohusiana na migogoro ya ardhi katika ukanda wa pwani ambapo baadhi ya wananchi wamepata muamko wa kwenda mahakamani kuhusiana na kesi hizo.
  Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa sauti moja jana walipitisha makadirio na mapato na matumizi ya bajeti ya ofisi ya makamo wa pili wa rais kwa mwaka wa fedha 2012-2013.


  Imewekwa na MAPARA at 9:51 AM [​IMG]
   
 2. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa sie ni mmoja kati ya kizingiti kikubwa cha kubinya Zanzibar katika Muungano kwa sababu tu ana damu ya huko , na sio yeye tu liko kundi lukiongozwa na Ali hassan Mwinyi na wenzake kufanya hujuma zidi ya Wazanzibar ikiwemo kutuma usalama wa taifa ueneza fitna za kuwagawa Wazanzibar kwa kutumia misingi ya upemba na unguja.

  Na hivi karibuni kutuma polisi wa usalama waliokuwa na nguo za polisi gengi specel kuishambulia kwa risasi gari ya sheh Farid lakini Bahadi mzuri hakuwemo, Seif iddi ni watu wenye kulinda damu yao ya kitanganyika wakichirikiana na watu wasio na asili za Zanzibar kama vile Mohammed Abudu.
   
Loading...