Ishindwe mara ngapi? Watu wamehitimu ualimu, nafasi ziko wazi nyingi sana lakini hela ya kuwaajiri haipo. Takwimu za TRA ni kwamba kodi inakusanywa nyingi - inaenda wapi! Mwezi huu wafanyakazi wa serikali wanakula xmass bila mshahara; sitashangaa hata mwaka mpya ikawa bado. Serikali imekopa nssf karibu inaifilisi, ikahamia kwenye benki za biashara ambako riba ni ya kufa mtu, kisa hawawezi kuuza treasury bills; hakuna wa kuzinunua!