Serikali haijatoa misaada kwa walioathirika na mafuriko

Serikali haijatoa misaada kwa walioathirika na mafuriko

Wakuu

Katika hali ya kushangaza na kustaajabisha, mpaka sasa serikali haijajihusisha na utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa wahanga wa mafuriko kwa Tanzania Dar es salaam na huko Zanzibar.

Misaada inayozungumziwa hapa ni ile inayohusu malazi na chakula, kiukweli sijapata kuona wala kusikia serikali ikilifikiria swala hili ambalo ni muhimu kuliko vyote

Ni kweli wanaopatwa na janga hili walikwisha amuliwa hapo awali wahame mabondeni lakini ndio hali ya watanzania hivyo serikali inatakiwa ithamini wananchi wake

Au mpaka UN ilete maturubai na msosi ndio nshituke?
Mafuriko ni janga kama majanga mengine, serikali mliangalie hili hata kwa kugeukia kwa mfuko wenu wa maafa.
Jibu ambalo lipo na liliishatolewa kitambo ni kuwa majanga yote yanayotokea HAYAJALETWA NA CCM. hivyo wananchi wapambane na hali yao. Rejea Tetemeko la ardhi Bukoba.
 
Hawa wa mabonden hatupaswi kuwaendekeza wala kuwaonea huruma pumbavu sana hawa yan vibur vyao ad wanahatarisha maisha ya watoto,
Kama kuna mtoto nimeona clip yake yan sijui amepona uko aisee na yale maj yalikua na nguvu sana

Mwsho wa cku haya mafuriko hayajaletwa na serikal kwaio kila mtu awajibike kiupande wake
Serikal itajenga miundo mbinu iyo athirika na wananchi wajenge nyumba zao
 
Msaa wanaoweza kutoa ni kuwasha HEDIKOPTA na kupita juu wakiwachungulia wahanga wa mafuriko,

Kati ya mikoa ambayo hakutakiwa kuwa na msamiati mafuriko ni Dasalama,

Aliepokea daraja la jangwani na kurusu kujenga zile ofisi pale kwenye hifadhi ya mto sijui yuko wapi mda huu

Nashirikiana na wewe kushangaa hili jambo
 
Kuna watu walishapewa viwanja lakini bado hawataki kuhama then wanapata matatizo (ya kujitakia) unalaumu serikali....hapo sioni tatizo la serikali kukaa kimya, ingekuwa hawajapewa mahali pa kuhamia ningeilaumu serikali....kuna watu wanataka kuchukulia haya majanga pia sehemu ya kutokea.

Ukiona kule ulipopelekwa hapakufai maana hakuna mzunguko wa pesa au sababu nyingine yoyote ukaamua kukomaa sehemu hatarishi, ikitokea hatari unatakiwa upambane na hali yako.
Hicho unachosema ni sawa na unapoambiwa gari 2 zimegongana uso kwa uso madereva wote wameumia vibaya.tukawasaidie, ukajibu, " speed limit wameshaekewa 60kmph, hiari zao"
 
Wakati mwingine wananchi waache Ubishi.Ukipita Pale Msimbazi Centre kama unakuja mikumi kuna nyumba zipo kwenye Kingo za mtu halafu mtu yupo comfortable anakaa pale.Mafuriko yakitokea aanze kulalamika.Kuna watu wa kusaidia lkn wengine sidhani kama wanahitaji kusaidiwa.
Pia serikali nao ni wa ajabu kweli nani aliwashauri wajenge kituo cha Mwendokasi Pale Jangwani?
 
Waulize wahanga wa Tetemeko Kagera kwanza ndo uje tena.
 
Wao nao waache ubishi waondoke maeneo hayo haiwezekani kila msimu wa mvua wao ni kuhitaji misaada tu. Matatizo mengine ni ya kujitakia. Kila wakiambiwa waondoke wabishi utadhani nchi imekwisha hakuna sehemu nyingine za kuishi. Serikali nayo iache siasa nvua ikiisha ibomoe nyumba zote zilizopo mabondeni. Mbona Mkwajuni walibomoa sasa fikiria kama wangekuwa hawakubomoa hali ingekuwaje leo? Tatizo wataalamu wakishauri wanakuja wanasiasa wanaanza kujifanya wanawatetea. Ubungo mpaka Kiluvya watu wamebomolewa na wanaendelea kubomolewa nyumba na maisha yanaendelea. Hao wa msbondeni wana nini? Kama ni misaada walitakiwa sasa kupewa watu wa Kimara hadi kiluvya. Hatuwezi kuwa tunawapa misaada watu wale wale kila mwaka. Penye ukweli lazima tuseme!

Sent from my SM-N9005 using JamiiForums mobile app
Haiingii akilini serikali imeweza kubomoa kimara inaogopa Mabondeni.Halafu serikali Nayo inajicontradict itaanzaje kubomoa wakati yenyewe ndo inajenga
 
Wewe uliambiwa na wazazi wako kwa unyenyekevu na maombi juu uwe tajiri uwakomboe .swali umeshakua tajiri mpaka umesahau ilivyo shida kujenga !!!???
Kujenga ni shiiida lkn huwezi risk maisha kisa tabu kujenga.Kama ni tabu kujenga je hela za msaada zitatoka wapi,hawa watu wahame tu haiwezekani Kila mwaka wimbo ukawa huo huo
 
wachana na mihemko!
inamaana hyyo maeneeo yalitolewa pia kwa watu wa vingunguti, mikochen, keko, na tandale?
Mkuu kuna watu wanahitaji msaada lkn kuna wengine si halali kupata msaada.kule Jangwani sidhani kama wanastahili kuhurumiwa tena
 
Wewe uliambiwa na wazazi wako kwa unyenyekevu na maombi juu uwe tajiri uwakomboe .swali umeshakua tajiri mpaka umesahau ilivyo shida kujenga !!!???
Kama kujenga ni shida kwanini walipokea viwanja walivyopewa? Huo ni utapeli na ndiyo sababu waliviuza wakapata pesa, sasa msaada kwanini tena.
 
Amiri Jeshi Mkuu kazi yake ni kuamrisha vita tu? Sio kuokoa wananchi wake na maafa?
Kweli Rais wa wanyonge hajawatendea haki watu wa Dar....Kuna chuki kubwa sana kati yake na watu wa Dar

Jamani, Video zinaonekana watu wanaelea, Jeshi na Polisi wana Helicopter....

Serikali ijenge maeneo ya dharura ubungo au Kibaha, weka mahema na peleka misaada

Jamani..Rais huyu ana roho ya Jiwe au ubinadamu?

Sasa Maendeleo anayojitapa anamletea nani? kama watu wanakufa?
 
Tuwe realistic. Serikali inaweza kusaidia wote waliopatwa na mafuriko??? Maana kwa Dar peke yake, karibu kila mtu amepatwa na mafuriko kwa namna yake.
 
Back
Top Bottom