Serikali ebu imulikeni kampuni ya S.T.E (substation engineering technology)

cleokippo

JF-Expert Member
Dec 21, 2014
2,070
1,687
Habari za majukumu mabibi na mabwana, ni matumaini yangu nyote mko salama.

Nisiwapotezee sana muda niende moja kwa moja kwenye mada. kampuni tajwa hapo juu ni kampuni inayoshughulika na ujenzi wa vituo vya kuzalisha umeme pamoja na usambazaji wake.

Mkurugenzi wa kampuni hii anaitwa Mr TOGO na site manager anaitwa Mr NIKO NGIMBA , ofisi za hii kampuni zipo mkoani MOROGORO na kwasasa kampuni hii ina mradi mkoani Kagera, wilaya ya Biharamulo, kijiji cha Nyakanazi ila mradi upo kwenye hatua ya mwisho kumalizika.

Hii kampuni imekuwa ni kero kubwa sana kwa wafanyakazi wake kwani uongozi umekuwa haulipi wafanyakazi mishahara yao hali inayopelekea site manager Mr NIKO kupelekwa mbele ya vyombo vya sheria mara kwa mara

pili : ni kampun ambayo haitoi mikataba kwa wafanya kazi hali ambayo inapelekea serikali kupoteza mapato kwa kukosa kukusanya kodi

tatu: mazingira hatarishi ya kiusalama kwa wafanyakazi wake...hii inapelekea wafanyakazi kupata ajali za mara kwa mara

Sasa bas kwakuwa serikali hii ni sikivu tunaomba iimulike kwa jicho la tatu hii kampuni ili iweze kubain madudu yanayofanywa na hii kampuni. Wapo wafanyakazi ambao toka mwezi wa 10 mpaka hv leo hawajalipwa mishahara yao, Serikali ya mtaa inafaham hilo jambo, kituo cha polis nyakanazi kinafaham hilo jambo pia na mpaka kesho bas madai yao hayajashughulikiwa.

Kero za mishahara kwa wafanyakazi zilianza tangu mwanzo wa mradi mpaka hv sasa mradi unaelekea mwisho lakin bado hazijatatuliwa..

Kwa hiyo Mama Samia tuma watu wako wakomeshe hz kampuni za kiswahili zinazofanya kazi kiujanja ujanja ikiwezekana anza na hii kampuni ya S.T.E
 
hizo ziko nyingi za wazawa heri uachane nayo wakikulipa utapoteza muda bure miye yalisha nikuta
 
Bado subiri itakapopanda hadhi kutoka substation kuwa station kamili mambo yatakuwa mswano.
 
Back
Top Bottom