Serikali: Atakayebainika kuihujumu nchi kuhusu kushikwa kwa ndege ya ATCL atafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi

ipo kwa ajili ya kunyonga,husikii wenyewe wanajiita serikali ya wanyonge
Awamu ya kuzulumu kila kitu,wakulima wanalia,wastafuu wanalia,wafanyakazi wanalia,wafanyabiashara wanalia,sasa hii serikali ya awamu ya tano IPO kwa ajiri ya nani na kwa sababu gani?Wadanganyika amkeni
 
Ikifika mahakamani ndio utajua ni uhaini kivipi, Ni kwamchakato halali wa kisheria au kutoa Siri za ndani kwa faida ya Taifa lingine. Ndebile kakupa mfano. Km ukiwa unadaiwa alafu mkeo akashirikiana na mdai wako ukapelekwa mahakamani. Ukigundua usaliti wa mkeo huwezi muacha salama hata km deni utalipa.
Lipeni deni muone kama kuna kelele. Hii inawasumbua aibu
 
Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Dk Hassan Abbas amesema watakaobainika kuihujumu Serikali kuhusu kuzuiwa kwa ndege ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) nchini Afrika Kusini watafunguliwa kesi.

Abbas amesema watafunguliwa mashtaka ya kuihujumu nchi mara baada ya kumalizika kwa kesi ya kuzuiwa kwa ndege hiyo inayosikilizwa katika Mahakama Kuu ya Afrika Kusini.

Akizungumza mjini Dodoma leo Jumamosi Agosti 31, 2019 Dk Abbas amesema wapo Watanzania wanaishiriki kuihujumu Serikali kuhusu ndege hiyo, kwamba kuna siku uhujumu huo utawasaidia.

“Wapo wazawa wanaofanya mawili, matatu kuhujumu nchi lakini niwaeleze tusubiri kesi iishe huko Afrika Kusini, tutawafungulia kesi ya kuhujumu nchi yetu.”

“Hakuna Nabii katika historia ya Manabii aliyewahi kuaminiwa kwa asilimia 100, hivyo huwezi kukubaliwa na watu wote, hata hii ndege inayoshikiliwa ikija Tanzania ipo siku wanaochukia watatumia usafiri huo kwenda Afrika Kusini kama sio wao basi watoto wao,” amesema Dk Abbas.

Jana Mawakili wanaoiwakilisha Tanzania katika kesi ya kuzuiwa ndege hiyo waliitaka mahakama Kuu ya Afrika Kusini kutupilia mbali zuio la kuzuia ndege ya shirika hilo ya Airbus A220-300, wakisema ilitolewa kimakosa.

Nikisema kuwa Siku hizi hakuna utofauti kati ya mwenye PhD / Doctorate na Yule wa Darasa la Saba hasa katika Fikra na kuna muda unaweza Kukuta Yule wa Darasa la Saba akawa na Upeo mkubwa na Mjenga Hoja mzuri kuliko Msomi wa Shahada ya Uzamivu kama huyu Msemaji wa Serikali.

Mimi nilitegemea Kwanza angekiri kuwa kuna Makosa ya Kiutendaji hasa ya Kisheria yaliyotokea na Uzembe fulani ulikuwepo hivyo kama Serikali watajirekebisha ili lisitokee tena Yeye Uwasilishaji wake mzima ni wa Kulipa Kisasi dhidi ya Watanzania ( Watu ) anaowasingizia kuwa ni Wasaliti na wanaihujumu nchi wakati Logically tu Serikali ndiyo Wahujumu Namba Moja wa Kodi za Watanzania kwani kama kweli walikuwa wanajua Siku nyingi kuwa Bwana Herman Styen anatudai basi wangehakikisha wanamalizana nae Kistaarabu tu bila Kutumia Ubabe wao ambao leo umetugharimu na Kuifikisha nchi hapa na hadi kupata Aibu hii.

Na wakati huyu Msemaji wenu mwenye PhD akisema kuwa Serikali ikiwajua Watu waliohusika katika kile anachokiita Kuhujumiwa akumbuke kuwa nimesikia hata wale Wadeni wengine kama Symbion na wale wa Lake Tanganyika bila kusahau wengineo sasa wanajipanga Kuishtaki Serikali na kuna uwezekano hata Yeye ( Msemaji wa Serikali ) nae akaja Kukamatwa pale Ndege zote zikikamatwa mpaka Bosi wake alipe Madeni yao ndipo ataachiwa.

Na huu ndiyo umekuwa ' Udhaifu ' mkubwa wa Serikali hii ya Awamu ya Tano kwa tabia yake ya Kupenda kutumia Mabavu / Ubabe katika mambo yake badala ya Hekima kama si Busara ndogo tu katika Kuyakabili mambo yake. Labda Serikali ya Awamu hii ijiulize tu ni kwanini hili halikufanyika katika Awamu zote ( japo Malipo yalikuwa yakilipwa ) lakini limekuja Kuibuka katika Awamu hii ambayo Msemaji wa Serikali anaitumikia?

Sijui hizi PhD's huwa mnapewa kwa Vigezo gani wakati kwa Uwasilishaji wenu tu huu mnaonekana kuwa hamna Akili kabisa.
 
Lipeni deni muone kama kuna kelele. Hii inawasumbua aibu

Inaonekana umekurupuka. Hakuna nchi duniani ambayo haidaiwi. Kabla ya kulipa lazima tujiridhishe kwamba hilo ni deni sahihi, sio kulipalipa tu kwa sababu tuna pesa, huo ni ulofa tumewaachia mburukenge.
 
Awamu ya kuzulumu kila kitu,wakulima wanalia,wastafuu wanalia,wafanyakazi wanalia,wafanyabiashara wanalia,sasa hii serikali ya awamu ya tano IPO kwa ajiri ya nani na kwa sababu gani?Wadanganyika amkeni
Umewasahau wafugaji . Ng'ombe zao zilipigwa mnada na wao kuambiwa wachukuwe wake zao na watoto waondoke
 
serikali imetangaza nia ya kumfungulia mashtaka ya kuhujumu uchumi yeyote atakayebainika alishiriki kusababisha ndege yetu kuzuiliwa kwa amri ya mahakama nchini Afrka kusini.
wananchi tunaomba tushirikishwe kwa njia huru kabisa tupate kuwataja hadharani ili hatua zianze kuchukuliwa haraka.

Wa kwanza kushtakiwa awe aliyegoma kumlipa mkulima.

Wananchi wapo tayari kutoa ushirikiano.
 
Wanahujumu kivipi wakati serikali yenyewe imekiri kuwa inadaiwa? Kuhujumu ni kama kungekuwa hakuna deni na zikafanyika njama za kuikamata hapo tungeelewa. Lakini kama kosa lipo dhahiri mtu anadai haki yake hujuma iko wapi hapo? Mbona Bombadia ilishikiliwa Canada tukalipa na ikaachiwa sasa hujuma iko wapi?

Mimi nashauri wote walioshiriki biashara ya kununua madiwani na wabunge wa upinzani kwa kisingizio cha kuunga mkono serikali pamoja na wahamaji wenyewe ndio wakamatwe na kushitakiwa kwa kuhujumu uchumi kwani tumelazimika kutumia mabilioni ya pesa kurudia chaguzi za kijinga kabisa eti za kuwachagua tena wao, mabilioni ambayo tungemlipa huyo mkulima anayetudai na ndege yetu leo ingekuwa kazini. Hawa ndio wahujumu uchumi namba moja katika awamu hii ya tano ya wanyonge na masikini wa nchi hii.
 
Kama kweli kuna mtanzania alishiriki kufanya huu unaoitwa uhaini he/she is really going to pay
Ila kama hayupo basi serikali itabidi ilipie but
Ole wake aliyehusika......
 
Wanajiamini itarudi S.A hana makubaliano yoyote ya kimataifa kwenye maswala ya arbitration zaidi ya NY Arbitration Convention.

The good news kwao Tanzania ni member pia, the bad news ukijiunga unachagua articles unazopokea na Tanzania imekataa domestic cases kuwa enforced nje au kuwa enforced na mataifa ambayo hawana makubaliano nayo mengine.

S.A na Tanzania hawana such rectified enforcement ndio maana wanajiamini, isitoshe kesi yenyewe ni domestic matter kwa sheria za Tanzania.
Dawa ya Deni ni kulipa waache kuingiza Taifa kwenye gharama zingine zisizo na tija,
 
Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Dk Hassan Abbas amesema watakaobainika kuihujumu Serikali kuhusu kuzuiwa kwa ndege ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) nchini Afrika Kusini watafunguliwa kesi.

Abbas amesema watafunguliwa mashtaka ya kuihujumu nchi mara baada ya kumalizika kwa kesi ya kuzuiwa kwa ndege hiyo inayosikilizwa katika Mahakama Kuu ya Afrika Kusini.

Akizungumza mjini Dodoma leo Jumamosi Agosti 31, 2019 Dk Abbas amesema wapo Watanzania wanaishiriki kuihujumu Serikali kuhusu ndege hiyo, kwamba kuna siku uhujumu huo utawasaidia.

“Wapo wazawa wanaofanya mawili, matatu kuhujumu nchi lakini niwaeleze tusubiri kesi iishe huko Afrika Kusini, tutawafungulia kesi ya kuhujumu nchi yetu.”

“Hakuna Nabii katika historia ya Manabii aliyewahi kuaminiwa kwa asilimia 100, hivyo huwezi kukubaliwa na watu wote, hata hii ndege inayoshikiliwa ikija Tanzania ipo siku wanaochukia watatumia usafiri huo kwenda Afrika Kusini kama sio wao basi watoto wao,” amesema Dk Abbas.

Jana Mawakili wanaoiwakilisha Tanzania katika kesi ya kuzuiwa ndege hiyo waliitaka mahakama Kuu ya Afrika Kusini kutupilia mbali zuio la kuzuia ndege ya shirika hilo ya Airbus A220-300, wakisema ilitolewa kimakosa.
Hivi kuna sababu gani ya kujitetea?
Serikali/wat waliopewa dhamani na serikali wamekuwa wepesi sana kulaumu na kuelekeza makosa yao juu ya watu wengine.

Je mtu anakuwa adui kwa sabau ya kudai haki yake?
Kama Serikali haikuwa na kosa kwenye sakata hili, ni nani angejitokeza na kukamata ndege yao bila sababu?
Shda iko kwa serikali na haya yote yanasababishwa na watendaji wenye makusudio maovu juu ya serikali na wanaitia serikali hasara kubwa.
Wanashindwaje kuishauri serikali kulingana na sheria za kimataifa?

Ingekuwa ni mamlaka yangu, hawa wanasheria walikuwa wa kufunga gerezani ili wajifunze kutumia taaluma zao kwa amanufaa ya nchi na si kutudanganya na kutumia mabavu
 
Na kama rais alishauriwa vizuri halafu aka kataa na kupuuza ushauri itabidi yeye ndiye ashitakiwe kwa kuhujumu uchumi. Hakuna namna! Si ulisikia alisema yeye ni dereva wa roli hasikilizi kelele za abiria? Akasema pia kuwa yeye ni jiwe haelekezwi cha kufanya. Sasa unategemea nini hapo!
nikitegemea wale waliomshauri vibaya Rais ndio wangewajibishwa.
 
Mkuu serikali inatumia mawakili 16 kujustify ujinga ilioufanya kwenye ubunge wa Lissu,Sasa serikali inashindwaje kutumia wakili angalau mmoja tu kwenda mahakamani kujustify ufake wa Steyn na ndege yetu ikaachiwa na badala yake mnatupigia makelele tu hapa na msiba wenu
Cyprian musiba kawaroga mtukufu kabudi na wenzao wanamtii kama mungu sasa kila ujinga anaowashauri wanaukubali wamelishwa limbwata kubwa na kuwa mazezeta wa cyprian musiba
 
Back
Top Bottom