Serikali angalieni huu utofauti wa ada za vyuo vikuu hasa vya serikali

Serikali angalieni huu utofauti wa ada za vyuo vikuu hasa vya serikali

ngasha

Senior Member
Joined
Jul 9, 2016
Posts
145
Reaction score
74
Habari zenu wadau wa elimu,

Nimekuja na suala moja tu ambalo naona kama halipo sawa katika hii sekta ya elimu, suala hili ni ada !!

Ivi inakuwaje vyuo kama UDOM,UDSM,MZUMBE,SUA, n.k ambavyo ni vya serikali kuwa na viwango tofauti vya ada kwa course/faculity moja?

Mfano degree ya education UDOM ni laki 7 lakini UDSM degree hiyo hiyo ni million moja na laki kadhaa

Kinachonishangaza ni utofauti uo mkubwa wakati vyote vinaongozwa na kusimamiwa na serikali ile ile,

Nika jiuliza maswali kadhaa;
1.Au malectures wa UDOM wanalipwa kidogo kuliko wa UDSM?

2.Au degree ya UDSM ina thamani kuliko ya UDOM?

3.Au vyuo hivi navyo ni private ndo maana kila kimoja kinajiamulia kiwango cha ada?

Ingekuwa vizuri serikali ingeweka viwango sawa vya ada kwa vyuo vyote nchini ilikupunguza competition ya watu kukimbilia vyuo kadhaa vyenye ada ndogo matokeo take ndo hayo wengine kukosa nafasi kutokana na vyuo husika kujaa

Pia vyuo vya private viangaliwe katika upangaji wake wa ada kwani elimu sasa imekuwa biashara wanajiamulia tuu na kuwa umiza wananchi wa hali ya chini !!

Au nyie wenzangu wa JF mnalionaje suala hili?

#Ni mtazamo tuu
 
..From my point Of view,hii ni kama michango kwa secondary schools,maana hizo hela ndo zinatumika kuendesha sehemu husika nadhan ivyo kila mtu anapanga
Mbna shule za secondary ambazo ni za serikali ada ni sawa nchi nzima pamoja na utofauti was maeneo zilipo shule hizo?
 
Basi wange weka kiwango sawa cha ada ila michango mingine ya uendeshaji wa chuo ndo iwetofauti kulingana na hali ya maisha ya eneo husika
 
1475129083836.png
 
Kuna screenshot hapo nimeweka hebu soma vizur then uje na hoja nyingine
 
Sio education zote ada yake ni laki saba kwa kifupi ww mtoa mada
 
Huenda kulingana na tofauti ya gharama za maisha ,,
Basi ada iwe sawa michango mingine ndo itofautiane kulingana na eneo au vp, iyo ni kwa mujibu wa point yako

#Ni mtazamo tuu
 
Mbna shule za secondary ambazo ni za serikali ada ni sawa nchi nzima pamoja na utofauti was maeneo zilipo shule hizo?
Usitake kulinganisha shule na chuo kwa mfumo wa ulipaji ada.... Kila chuo kinajiendesha kulingana na facilities zinazohitajika..then unataka kuniambia education inayotolewa udsm zote ni bei moja??
 
Then kwa udsm kuna baadhi ya education program ni 1m so huo utofauti ni kama nilivyosema inatokana namna chuo kinavyojiendesha ni kama vile kuna baadhi ya program unakuta katkia chuo kimoja ni miaka 4 kwingine unakuta miaka 3 haimaanishi kuwa anayesoma miaka minne ndo atakuwa yuko vizuri sana bali kutakuwa na mapungufu baini ya pande mbili so kila mmoja anaweza kujidai kwa upande wake....
 
Usitake kulinganisha shule na chuo kwa mfumo wa ulipaji ada.... Kila chuo kinajiendesha kulingana na facilities zinazohitajika..then unataka kuniambia education inayotolewa udsm zote ni bei moja??
Kwamaana hiyo unataka kuniambia facilities za kuendeshea bachelor of arts with education in Udom ni tofauti na zile zinazo hitajika Udsm
 
Nahis hamja nisoma fresh bado, ninachoongelea ni utofauti wa ada kati ya chuo na chuo na si kwa course na course katka chuo kimoja
 
Then kwa udsm kuna baadhi ya education program ni 1m so huo utofauti ni kama nilivyosema inatokana namna chuo kinavyojiendesha ni kama vile kuna baadhi ya program unakuta katkia chuo kimoja ni miaka 4 kwingine unakuta miaka 3 haimaanishi kuwa anayesoma miaka minne ndo atakuwa yuko vizuri sana bali kutakuwa na mapungufu baini ya pande mbili so kila mmoja anaweza kujidai kwa upande wake....
Bado point yang inabaki palepale najua si education zote ada ni ile ile ila kwanini ktk aina iyo moja tu ya education ada iwetofauti kwa chuo na chuo ikiwa mda wake ni sawa labda kote miaka 3 na facilities zinazohitajika ni zilezile?
 
Nenda kwa mkurugenzi wa chuo cha UDOM NA UDSM watakupa majibu mazuri
 
Hilo nalo tatizo kubwa sana kwa mfano SUA wanatoa Bsc. in wildlife management na ada yake milion moja kama na laki mbili ivi lakini course hiyohiyo inatolewa MWEKA ada yake ni million 4 na laki 4 yaani nashindwa hata kuelewa na vyou vyote ni serikali hapo utata sana.
 
Sana tuu ata hawarleweki yan
 
Back
Top Bottom