Ndugu unaweza kuwa na point nzuri lakini je unauhakika hao wameshafikisha umri wa kustaafu? Are you sure Mkandala kafikisha 60!? Nadhani point ni utafutwe utaratibu ambapo wakuu wa vyuo na wakuu wa vyuo wasaidizi hawatateuliwa na raisi. Maana the way it is now its too political!
Website ya udsm inaonesha kazaliwa 1953! Atastaafu kwa lazima mwakani! Then your point will be valid, as of now its premature
Thrd hii ilikuwa na lengo la kuwazungumzia viongozi wakuu watendaji. Vice-Chancellors na wasaidizi wao. Kila chuo kikuu cha serikali kinaendeshwa na Charter. Utaratibu wa kuwapata viongozi wa vyuo hivi vyote, zinafanana kabisa. Hakuna kiongozi anayepatikana kwa uteuzi wa Rais. Wooote wanapatikana kwa kamati (Search committee).
Kwa VCs wote wanatakiwa wakae madarakani kwa vipindi viwili vya miaka mitano kila kimoja. Kwa maana nyingine ukishamaliza muhula wa miaka mitano unaweza kuomba tena au kupitishwa kama umri unakuruhusu miaka mitano mingine. Hapo ndo kuna muzozo na kuna makundi ya watu;
1. kuna viongozi umri hauwaruhusu kuendelea na madaraka kwa kuwa hawana miaka mitano mbele yao
2. kuna watu wamemaliza vipindi viwili vya uongozi na kimya kimya wamepewa tena kinyume cha charter.
3. kuna wengine wamestaafu kwa umri (miaka 60 lakini wamepewa tena kuongoza vyuo.
Tuamini kwamba nchi haina muelekeo kwa sababu haya yote yanatokea hata ktk taasisi zingine za serikali. Nawashangaa sana watu wa vyuo vikuu kwa sababu wao walistahili kuheshimu sheria na taratibu za vyuo vyao lakini sasa yaonekana ni kufahamiana.
Na kibaya sana ni jinsi hizo search committee zinavyopatikana. Zinapendekezwa na baraza la chuo. Mkuu wa baraza wa kila chuo ni mstaafu. Mkuu wa baraza anapatikana kwa kupendekezwa na viongozi wa chuo chenyewe tena na kumpelekea Rais ambaye mara zote hupitisha. Kwa hiyo ni mzunguko, yaani anapitishwa kwa mapemdekezo ya viongozi ambao nao wanapitishwa kwa mapendekezo yake tena! RUBBISH!!
Kama mmoja wetu alivyoeleza vyuo vimejaa ufisadi bila hata kuingiliwa. Eti wakiguswa wanasema wanataka uhuru wa vyuo. uhuru wa kuiba?
Tusiwateteee. Wanauwa elimu na sasa kazi kubwa yao ni kujikomba kwa wanasiasa na tuuuu!