Serikali 3 haziepukiki

Serikali 3 haziepukiki

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
25,950
Reaction score
25,327
Mfumo wa serikali 3 hauepukiki hata kidogo. Nawashangaa sana wale wanafiki wachache wanaokataa uwepo wa serikali huku wakijua kwamba wazanzibar wao wana serikali yao kamili--wana rais, jeshi, benki kuu, wimbo wa taifa, bunge, mahakama, na bendera ya nchi yao.

Hakuna mtanganyika anayeruhusiwa kumiliki hata futi moja ya eneo la ardhi nchini zanzibar lakini wao wakija huku bara wanamiliki ardhi kadri wapendavyo. Sasa huu ni muungano wa aina gani ambao upande mmoja unakubali kunyonywa na unafurahia unyonyaji huo?

Aidha, wazanzibar (wanyonyaji) wao wako tayari kuwepo kwa serikali 3 hata kuanzia leo lakini eti watanganyika (wanyonywaji) hatutaki. Haya mbona ni mambo ya ajabu sana?

Wazanzibar tayari wao wana serikali yao ila wanatuunga mkono watanganyika ili nasi tupate serikali yetu. Sasa kwa nini tunawakatisha tamaa wakati wao wanatusaidia ili nasi tuwe na serikali yetu?
Jamani, watanganyika tuache unafiki ndugu zangu. Mfumo wa serikali 3 hauepukiki katu.
 
Kweli kaka huu ni upuuzi wa hali yya juu kuwa na serikali 2
Mpango mzima ni serikali 3 tu
 
Ukweli ni kwamba kuendesha serikali 3 ni gharama kubwa ambayo tunataka kuikubali ili kulinda muungano. Tungeweza kubaki na serikali 2 zilizoboreshwa maana kusema kweli wanaozungumzia muundo wa serikali ni wazanzibari na si watanganyika. Watanganyika wanazungumza kuhusu maadili ya viongozi na matumizi ya rasilimali. Sema kinamuunganochoshangaza ni kwamba wazanzibari wanalalamikia muundo wa serikali bila kujua kwamba wao wana serikali tayari na wao ndio wanaonufaika na muundo uliopo. Kwa kifupi serikali 3 ni hasara kwa taifa, faida kwa tanganyika na ni hatari kwa muungano. Nawasilisha.
 
Acha kukariri mambo. Toa mchanganuo wa hizo gharama tuone. Warioba kafafanua vizuri swala la gharama na kaeleweka. Muundo uliooo una gharama kubwa kuliko serikalu.i 3
Ukweli ni kwamba kuendesha serikali 3 ni gharama kubwa ambayo tunataka kuikubali ili kulinda muungano. Tungeweza kubaki na serikali 2 zilizoboreshwa maana kusema kweli wanaozungumzia muundo wa serikali ni wazanzibari na si watanganyika. Watanganyika wanazungumza kuhusu maadili ya viongozi na matumizi ya rasilimali. Sema kinamuunganochoshangaza ni kwamba wazanzibari wanalalamikia muundo wa serikali bila kujua kwamba wao wana serikali tayari na wao ndio wanaonufaika na muundo uliopo. Kwa kifupi serikali 3 ni hasara kwa taifa, faida kwa tanganyika na ni hatari kwa muungano. Nawasilisha.
 
Ukweli ni kwamba kuendesha serikali 3 ni gharama kubwa ambayo tunataka kuikubali ili kulinda muungano. Tungeweza kubaki na serikali 2 zilizoboreshwa maana kusema kweli wanaozungumzia muundo wa serikali ni wazanzibari na si watanganyika. Watanganyika wanazungumza kuhusu maadili ya viongozi na matumizi ya rasilimali. Sema kinamuunganochoshangaza ni kwamba wazanzibari wanalalamikia muundo wa serikali bila kujua kwamba wao wana serikali tayari na wao ndio wanaonufaika na muundo uliopo. Kwa kifupi serikali 3 ni hasara kwa taifa, faida kwa tanganyika na ni hatari kwa muungano. Nawasilisha.

ndivyo ulivyokaririshwa?
 
Back
Top Bottom