Serikali 2 sasa wahamia kwa wanafunzi vyuo vikuu

Serikali 2 sasa wahamia kwa wanafunzi vyuo vikuu

MchunguZI

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2008
Posts
4,038
Reaction score
2,224
Nina taarifa ya uhakika kwamba serikali imeanza kutumia pesa za walipa kodi kuwashawishi viongozi wa vyama vya wanafunzi kushawishi wanafunzi wenzao ili watoe matamko ya kuunga mkono serikali 2. Walioko vyuo vikuu sasa mutashuhudia mikutano ambayo imelipiwa (sponsored) na serikali ili kutoa matamko ya aina hiyo.

Tutakapoanza kusikia matamko ya aina hiyo tusishangae sana. Nayo inachukuliwa kwamba ni mbinu ya kisiasa kuanza kuwashawishi wananchi kupitia wanafunzi. Binafsi naomba tu kwamba matamko hayo yasiwe kama yale yaliyotumwa kwa mzee warioba. Matusi hapana!
 
Naamini nimeelimika. Atakayekuja kujaribu kumwaga sumu ya serikali 2 anazotaka yeye atajikuta ni mpenzi wa serikali 3 za wananchi. Sio kiongozi wa wanachuo, ila nitakula nao sahani moja.

Ccm wanakataa siasa vyuoni ila wao wanajieta, nawasubiri
 
Patrickcharles. Ukweli ni kwamba serikali 3 ndio ufunguo wa maendeleo yetu. Tanganyika yetu itarudi kwasababu kila siku najiuliza wenzetu wanaitwa wazanzibar,sisi huku wanatuita wanatanzania na kila kiongozi anajua kabisa huku ni tanganyika inauma sana.
 
Ajabu ni kwamba wengi nilio kutana nao (sio wanachuo) kwa kufuata mkumbo tuu wanashabikia serikali mbili...

Ukimwambia sasa akutajie hizo serikali mbili utamuonea huruma... Hajui 'A' wala 'B'
 
Kuna wanafunzi wachuo kukuu cha Zanzibr walihojiwa na BBC Jana jioni kuhusu muungano. wale wanafunzi wanajitambua na kujielewa na sio wa hapa Tanganyika wasaka tonge
 
Anayeongoza kampeni hiyo kwa wanafunzi vyuoni ni Wasira. Yaaminika amewaita baadhi ya viongozi na kuwapa ahadi ya pesa.

Sijui yale maelezo ya Lisu ameyajibu! Maana ndiye aliyehamia NCCR mpaka baada ya kifo cha Nyerere ndo kajirudisha CCM.
 
hata sasa tuko dom kwa kazi hiyo
 
Wanafunzi wa vyuo vikuu ndio walitakiwa wawe na ulewa wa muungano upi unafaa na siyo wa serikali 2 ambao umewaletea kupigwa mara kwa mara na serikali lazima mabadiliko yaje wawe na uelewa tunawapita hata sie wa sec school
 
kula pesa,halafu unabaki na msimamo wako,wacha walete hiyo pesa.
 
Back
Top Bottom