Jamaa mwenye familia anaonekana ni mtu mstaharabu na mwenye heshima kwenye familia yake na jamii kiujumla kumbe nyuma ya pazia ni muuaji wa kulipwa na katili ile mbaya na akiua huwa haachi ushahidi na bahati mbaya ana rafiki ambaye ni polisi lakini hawajui shughuli halisi ya jamaa ni ipi?
Kitaaluma ni muhasibu anasingiziwa kuwa ameiba hela zote za wawekezaji wa hiyo organization kwa kuwa kakosa namna ya kujitetea kutoka kwenye huo msala anajikuta anakimbia sehemu ili akae mbali na huo msala Sasa huko alikoenda anajikuta anaishi maisha ambayo hakuwahi kutegemea kwasababu yeye katoka kwenye familia ya kishua
Ni series ambayo inazungumzia police ambao Wana deal na kuchunguza mauaji yanayotekea kibaya zaidi wanagundua Kuna picha inayomuonesha police mwenzao anatokea sehemu ya tukio lililofanyika mauaji wakamuuliza je ni yeye kwenye picha jamaa akajibu sio yeye je ni kweli sio yeye? na kama ni yeye je kazi yao ya kumtafuta muuaji inawezaje kuwa nyepesi ikiwa mmoja wao ni muuaji maana ripoti zote kama police lazima yeye aipate
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.