Serengeti: Mgambo apoteza maisha kisa ushindani wa kunywa pombe

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Serengeti.
Ushindani wa kunywa pombe aina mbili za Shujaa na Shimwaa umesababisha kifo cha askari mgambo, Zakayo Thomas (50) maarufu Hayaishi huku mwenzake Patrick Paul akikimbizwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara kwa matibabu.

Tukio hilo limelotokea Aprili 10, 2018 katika baa ya FM mjini Mugumu na limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Jafari Mohamed na uongozi wa hospitali Teule ya Nyerere ikielezwa kuwa chanzo ni unywaji pombe kupita kiasi.

Kamanda Mohamed amesema Thomas alifariki dunia kabla ya kufika hospitali kwa matibabu.

“Chanzo ni kunywa pombe kupita kiasi huyo mwenzake Paulo (23) mkazi wa Morotonga anaendelea vizuri baada ya kupata matibabu. Tunaendelea na uchunguzi wa tukio hilo baadaye tutatoa taarifa,” amesema.

Mganga Mkuu wa Hospitali Teule ya Nyerere, Emiliana Donald amesema Thomas alifikishwa hapo akiwa ameshafariki dunia.

“Chanzo ni unywaji wa pombe kupita kiasi na inawezekana hawakuwa wamepata chakula baada ya matibabu Paulo tumeishamruhusu kutoka maana hali yake ni nzuri,”alisema.

Habari kutoka kwa baadhi ya mashuhuda wa tukio wamesema kuwa wawili hao walifika baa ya FM wakiwa wameshalewa na inasemekana walikuwa wakinywa kwa kuchanganya pombe aina mbili Shujaa na Shimwaa.

“Walikuwa wanakunywa pombe kwa ushindani inawezekana walikuwa hawajala chochote, baadaye Thomas alinyanyuka kama anaenda uani akaanguka, hakuna aliyemjali kwani watu walidhani amelewa ataamka,” amesema mmoja wa mashuhuda.

Amesema wakati Thomas akiwa amelala chini, walianza kupata wasiwasi baada ya kuona mwenzake akitapika mfululizo huku akiishiwa nguvu.

“Baada ya kumtazama Thomas tukaona hapumui ndipo watu wakashtuka na kutoa taarifa polisi, yeye alichukuliwa akiwa maeshafariki dunia.”



mwananchi
 
Hii inanikumbusha tukio moja la mfanyakazi wa kaka angu....alisifiwa kunywa k vant chupa kubwa bila kupumzika..chupa ya kwanza akamaliza..chupa ya pili alipomaliza na yeye alianguka...baadaye polisi wakamchukua kumpeleka hospitali

Baada ya kufika hakuna tulichojua ila asubuhi watu walijihimu kwenda kumuona hawakumkuta, wakajua labda tu alipona pombe zilipoisha akaondoka...baada ya siku tisa ndo tukapata taarifa kuwa jamaa yuko mochwari na manispaa wanataka kumzika....iliuma sana
 
Back
Top Bottom