Serengeti Breweries yaimarisha ushirikiano na serikali kukuza uwekezaji na uchumi

Serengeti Breweries yaimarisha ushirikiano na serikali kukuza uwekezaji na uchumi

Blasio Kachuchu

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
573
Reaction score
359

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imekutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, katika kikao cha kimkakati kilicholenga kuimarisha ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya uchumi wa Tanzania.

Kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam kilijikita katika kujadili nafasi ya sekta binafsi katika kusaidia utekelezaji wa vipaumbele vya maendeleo ya taifa, hususan kuelekea utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 inayolenga kuifanya Tanzania kuwa uchumi wa dola trilioni moja.



Kwa upande wa SBL, mazungumzo hayo yaliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo, Paul Makanza, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Obinna Anyalebechi.

Akizungumza katika kikao hicho, Anyalebechi alisema kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali katika kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia uwekezaji wa ndani na kuimarisha mnyororo wa thamani wa uzalishaji nchini.

“Tanzania itaendelea kuleta mageuzi ya kiuchumi kupitia ushirikiano imara kati ya Serikali na sekta binafsi. Sisi kama Kampuni ya Bia ya Serengeti tunaendelea kujizatiti kuwekeza katika uzalishaji wa ndani, kuimarisha mnyororo wa thamani wa ndani na kusaidia ukuaji wa uchumi shirikishi,” alisema.

Aliongeza kuwa mazingira mazuri ya uwekezaji yataendelea kuwa kichocheo muhimu cha kufungua fursa zaidi za kiuchumi nchini.



Taarifa zinaeleza kuwa SBL ni miongoni mwa kampuni kubwa za uzalishaji nchini na walipa kodi wakubwa, ambapo kampuni hiyo huchangia zaidi ya shilingi bilioni 220 kila mwaka katika uchumi wa taifa kupitia kodi, uwekezaji, ushirikiano na wazabuni pamoja na miradi ya maendeleo ya jamii.

Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, kampuni hiyo imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 165 kwa ajili ya kupanua na kuimarisha shughuli zake nchini, hatua inayodhihirisha dhamira yake ya kuendeleza uzalishaji wa ndani na kukuza sekta ya viwanda.

Mbali na uzalishaji wa bia, SBL pia hununua malighafi kutoka kwa wakulima wa ndani ikiwemo shayiri, mahindi na mtama vinavyotumika katika uzalishaji wake. Hatua hiyo imekuwa ikisaidia kuongeza kipato cha wakulima na kuimarisha mnyororo wa thamani wa ndani.

Kupitia shughuli zake, kampuni hiyo imetoa ajira rasmi kwa Watanzania zaidi ya 800 huku takribani watu 140,000 wakinufaika na mnyororo wa ajira unaotokana na shughuli zake mbalimbali nchini.


Kwa upande wake, Profesa Mkumbo alisisitiza umuhimu wa sekta binafsi katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya taifa, akibainisha kuwa ushirikiano kati ya Serikali na wawekezaji ni muhimu katika kukuza uchumi na kuongeza ajira.

“Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 inalenga kuifanya Tanzania kuwa uchumi wa dola trilioni moja, ambapo sekta binafsi itakuwa na nafasi kubwa katika kuchochea uwekezaji, ajira na ukuaji wa uchumi,” alisema.

Aliongeza kuwa mazungumzo na ushirikiano unaoendelea kati ya Serikali na wadau wa sekta binafsi kama Kampuni ya Bia ya Serengeti ni hatua muhimu katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuimarisha uchumi wa taifa.

Kikao hicho kilihitimishwa kwa makubaliano ya kuendelea kuimarisha ushirikiano, kukuza uwekezaji, kuimarisha mifumo ya sera na udhibiti pamoja na kuongeza uzalishaji wa ndani ili kuchochea maendeleo ya uchumi jumuishi nchini.​
 
Back
Top Bottom