Serengeti: Ahukumiwa miaka mitatu jela kwa wizi wa mbuzi

tang'ana

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
11,813
15,077
Mkazi wa kijiji cha Nyiboko, kata ya Kisaka, Mwita Karege (19) amehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Serengeti kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kukiri kuiba mbuzi watatu wenye thamani ya Sh150,000.

Hukumu hiyo katika kesi ya Jinai namba 326/2020 imesomwa leo Jumatatu Oktoba 25 na hakimu mkazi wa wilaya Adelina Mzalifu kufuatia mshitakiwa kukiri mahakamani hapo kuiba mbuzi hao.

Amesema kutokana na kosa alilotenda, mahakama inamhukumu kutumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo.

Awali, mwendesha mashitaka wa Jamhuri, Paschal Nkenyenge ameiambia mahakama kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Novemba 29, 2020.

Na kuwa alikutwa na mbuzi watatu wenye thamani ya Sh150,000, mali ya Mugusuhi Mwita, mkazi wa kijiji hicho, akidaiwa kuwapeleka mnadani kuuza.

Hata hivyo mshitakiwa alipopewa nafasi ya kujitetea alidai hana la kujitetea.
 
Back
Top Bottom