Serekali vs mashehe znz vs mfumo kristu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serekali vs mashehe znz vs mfumo kristu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kitero, May 31, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. k

  kitero JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 563
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikifuatilia sakata la ZNZ juu ya muungano, kwa macho ya nyama inaonekana mashehe wamechukua kazi ya wanaharakati au pengine wanasiasa ya kudai uhuru wa ZNZ kama wanavyosema.


  Kwangu binafsi naona hatari sana hasa kuchanganya dini na siasa. Waislamu wa bara wamebaki bila kauli pengine ni kutokana na uelewa mkubwa au mdogo juu ya dini yao. Je uislamu unaruhusu haya yote? Ingekuwa vema kama waislamu wa bara wangetoa kauli yao juu ya hili bila kuogopa aliyefanya ni muislamu/shehe au yoyote ili ukweli uweze kujulikana.


  Kikundi cha uamsho (kinaongozwa na mashehe) kinasema hakiusiki na uvunjifu wa amani uliotokea na wala uchomaji wa makanisa. Yes pengine ni kweli hakikutoa kauli hiyo, lakini je wameweza kufanya analysis ya mafundisho waliyokuwa wakiyatoa pamoja na madhara yake kwenye jamii (whether is positive or negative).


  Tafadhali kikundi cha uamsho, waliowaweka kwenye muungano ni viongozi wenu wa serikali na sio kanisa. Kama walirubuniwa bado haipaswi kuliadhibu kanisa, kama ni adhabu basi waadhibuni waliowafikisha hapo. Ila lililo bora zaidi NI KUTAFUTA NJIA YA AMANI BILA KUCHOMA MAKANISA


  Najua mnaelekezwa kuua ili kutetea uislamu ila lililo la hekima ni kutoua ili huyo unayetaka kumuua apate nafasi ya kubadilika na kuwa muislamu na mwisho afike kwa Mungu kama ni kweli.  Asante.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...