Sera ya Chadema ya "Utawala wa Majimbo"

Subirini muone; kwa uzuri wa sera hii, soon kupitia mgongo wa Katiba Mpya na propaganda nyingine MAGAMBA watai-download, kui-customize then watadai ni yao.

Kinachoudhi sio ku-implement hizo sera za wizi alimradi ni kwa faida ya wananchi na taifa kwa ujumla bali tatizo ni hizo dhihaka, dharau, na kejeli zao dhidi ya waasisi wa wazo husika.

Nashauri CHADEMA waiwekee hatimiliki (copyright) fasta ikibidi CCM wai-copy baada ya ku-acknowledge maana magamba wameishiwa ubunifu kabisa sasa hivi.
 
..naipinga sera ya majimbo.

..itaongeza gharama za utawala nchini.

..italeta migogoro[kutunishiana misuli] isiyo ya lazima kati ya serikali kuu na serikali za majimbo.

..itarudisha nyuma juhudi zetu na mafanikio tuliyoyapata ktk kujenga utaifa wa Tanzania.

..tatizo letu siyo mfumo wa utawala, bali viongozi na watawala wanaotuongoza.

..watetezi wa hoja hii wamejikita ktk malalamiko dhidi ya mgawanyo mbaya wa rasilimali za maeneo mbalimbali. tatizo hilo litatuliwe kwa kuleta formula nzuri zaidi ya mgawanyo na matumizi ya rasilimali zetu, na siyo kutuletea sera za majimbo.
 
kindafu

Asante kwa topic yako, binafsi niliwahi kuanzisha thread ya aina hii yenye heading 'CHADEMA haijajiandaa kuunda serikali' ikaondolewa. Lakini nilitegemea kujadili hasa juu ya sera ya majimbo ambayo CDM inatarajia kuitumia kuunda serikali endapo itafanikiwa kuingia madarakani. Tatizo lililopo kwa CDM hata kama hii sera ni nzuri au la haijulikani wala viongozi hawaiuzi majukwaani, ni bahati nzuri juzi nimemsikia m/kiti wa CDM akiizungumzia bungeni. Lakini hiyo haitoshi wananchi wanapaswa kuelimishwa na kuanza kuizoea jinsi inavyofanya kazi. Thread yenyewe niliyoanzisha ni hii hapa...

 

Naikubali mno hii sera ya Majimbo, kwani italeta chachu ya uwajibikaji na kuharakisha maendeleo
 
Pax

Very well said and point taken.
 
Last edited by a moderator:


Mkuu JokaKuu,
Ungaliiweka hiyo "Sera" mezani ndo ukaanza kuichambua na kuikosoa ningefurahi sana, ila pengine unakosoa bila hata kujua undani wake! Ombi langu kwa viongozi wa Chadema mnaotembelea hili Jamvi - tafadhali tuwezesheni kutembea pamoja!
 

Kindafu, my take ya nini tena? Ila kama usemavyo nadhani hii ni sawa na ile ambayo ilikuwa enzi hizo (ambayo tulisikia ilikuwepo) ya madaraka mikoani
 


Pax,

..majimbo huwa na mamlaka fulani ktk mambo ya kodi, elimu,sheria etc etc.

..USA kuna majimbo yanayoruhusu hukumu ya kifo na kuna majimbo yanakataa hukumu hiyo.

..yalikuwepo majimbo USA ambayo yalikuwa yamehalalisha segregation na ndoa za weusi na weupe zilikuwa zimepigwa marufuku, ingawa federal government ilikuwa inaelekeza vingine.

..pia sasa hivi kuna majimbo yamekwenda mahakamani kupinga utaratibu wa Health Care aliopendekeza Obama.

..katika masuala ya kodi, USA yapo majimbo ambayo hayana sales tax na mengine yana sales tax.

..kwa mtizamo wangu bado demokrasia yetu haijakomaa kiasi cha kuweza kuhimili utawala wa majimbo.

..ninachoogopa mimi ni gharama kubwa zinazotokana na mfumo huo, pamoja na kutunishiana misuli kunakoweza kutokea baina ya majimbo, au baina ya majimbo vs serikali kuu.
 
at least you dont know what you are saying or you are saying the opposite! kila ulichokisema ukweli ni kinyume chake kabisa! yaani mkuu sera ya majimbo hakunaga!
 
kwa taarifa yako mfumo wa majimbo ni rahisi sana kuliko wa sasa ila kuliona hilo inategemea na orientation yako maana rahisi is subjective.aidha mfumo wa majimbo utasaidia sana kukuza demokrasia.aidha kutunishana misuli kutasaidia sana kuwa na serikali makini na imara na pia itaongeza uzalendo wa kuipenda na kuilinda nchi yetu kutoka maadui wa nje
 

Admiral Elect,

..watu watayapenda majimbo na siyo taifa.

..kutunishiana misuli kutasababisha maendeleo kukwama, na siyo demokrasia.

..wenye majimbo na wakafanikiwa ni wale ambao hawana makabila na hawasumbuliwi na mambo kama udini wa hapa kwetu.
 
Admiral Elect,

..watu watayapenda majimbo na siyo taifa.

..kutunishiana misuli kutasababisha maendeleo kukwama, na siyo demokrasia.

..wenye majimbo na wakafanikiwa ni wale ambao hawana makabila na hawasumbuliwi na mambo kama udini wa hapa kwetu.
ndiyo watayapenda sana majimbo na halafu wataipenda zaidi nchi yao maana upendo ni mbegu ikishaota huzaa matunda mengi zaidi. NB charity begins at home!
misuguano huleta maendeleo na kukuza demokrasia maana wtu wataipractise at their own local areas. NB ukiona vinaelea ujue vimeundwa
hakuna nchi duniani isiyo na makabila! nchi hii hii haina udini ila kuna wajinga wachache wanaowafitini watanzania kwa manufaa yao ya kisiasa .NB divide and rule!
 

Admiral Elect,

..model unayoizungumzia wewe ni ya wapi??

..mimi naangalia USA na kinachoendelea kwao nadhani kikiletwa Tanzania tutasambaratika muda si mrefu.

..USA mwizi akiiba gari New Jersey halafu polisi wakianza kumfukuza, akiweza kuingia New York polisi hao inabidi wamuache na badala yake wawasiliane na polisi wa New York ili mwizi huyo aweze kukamatwa.

..pia kuna majimbo ya USA mfano California wameruhusu ndoa za ushoga, na wanataka kuvuta bangi, majimbo mengine ya USA yamekataa.

..I feel like the system ur proposing is too complicated and we will just be bogged down in trying to make the system work rather than kushughulikia matatizo ya wananchi.

NB:

..
 
 

Admiral,

..unaweza kutueleza Ghana na China mfumo wao wa majimbo unafanya vipi kazi??

..naomba utupe mifano ktk masuala kama kodi, mahakama na sheria, vyombo vya ulinzi kama Polisi etc etc.

..Nigeria wanayo majimbo lakini sidhani kama mambo yao ni mazuri sana.
 
Sera ya majimbo inafaa kwa mataifa makubwa yenye ardhi kubwa na population kubwa, mathalani nchi kama ya china yenye eneo mara kumi ya eneo la nchi yetu wamegawa majimbo ambayo baadhi ya majimbo ni makubwa kuliko nchi yetu, sasa kwa nchi kama ya tanzania ambayo ukubwa wake ni sawa na majimbo katika nchi za wenzetu sioni sababu ya kuigawa zaidi. Mimi naamini tanzania hii hii ikiwa chini ya serikali kuu inaweza kufanya vizuri iwapo sababu za kutofanya vizuri zitafanyiwa kazi.

kWA NCHI AMBAYO BADO INAFANYA JUHUDI KUPAMBANA NA UDINI NA UKABILA Kuigawa nchi katika majimbo ni kukaribisha sumu za " udini" kwenye maeneo yenye watu wengi wa dini moja, ni kukaribisha ukabila kwenye watu wengi wa kabila fulani.

Majimbo yatafaa tu iwapo east africa itakuwa nchi moja otherwise, tanzania kwa eneo lake hili na idadi ya watu wake bado inatawalika vyema na maendeleo kupatikana bila kuwepo kwa serikali za majimbo iwapo kanuni za maendeleo zinazingatiwa.
 
Mkuu nilidhani ya china na ghana ni homework yako? kwa nigeria ni mfumo wa majimbo ambao umesaidia angalau kufika hapo ilipo sasa vinginevyo ingeshagawanyika vipande 3
 
admiral elect can not respond to this msg! it is below army standards!
 
Somo linahitaji tuition na juhudi ya kutosha ktk kwa mwl.mda hautoshi ila tusichelewe sn.ni hayo 2.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…