hapa sasa sana wasioipenda hii sera watakuja na 'nyimbo' zao zilizoshindwa za ukabila, ujimbo nk lakini kwa nchi kama tz, hii ni sera nzuri.kufanya ufisadi kwenye single controlled state kama tz kwa ujumla ni rahisi kuliko kufanya ufisadi kwenye majimbo......hata kama ukiangalia kwa mbali unaweza fikiri labda unataka kuigawa nchi vipande vipande, ukiangalia vizuri utakuwa hii sera ni bora sana na watz kwa sasa hatuwezi kugawanyika, labda kwa uzanzibari na ubara...lakini sio utanganyika hata kama tungemega vipi..
Chadema ina uhakika mkubwa wa kushika Dola katika uchaguzi ujao kama utakuwa kweli huru na wa haki. Naunga mkono Sera yao ya Utawala wa Majimbo, na ningependekeza kwamba waiweke hadharani tangu mapema ili iweze kufanyiwa Pannel beating kwenye Vijiwe, Media, Mitandao na Forums mbali mbali. Wakati mwafaka ukifika wataunda tu kamati maalum kuchambua maoni yatakayokuwa yametolewa na wadau na kutoa kitu kilicho bora - kinachokubalika na kinachowezekana! Ningetamani kwa sasa waainishe bayana yafuatayo:
i. Ni jinsi gani wataigawa Tanzania ki-Majimbo i.e. Majimbo mangapi na mipaka yake ki-Jiografia.
ii. Mfumo wa Utawala utakavyokuwa ngazi ya Taifa na ngazi ya Jimbo.
iii. Mfumo wa uchaguzi utakaotumika kuwapata viongozi ya Kitaifa na wa Majimbo.
iv. Mipaka ya Utawala/Maamuzi Kitaifa na katika Majimbo.
v. Mfumo wa Utawala wa Fedha Kitaifa na katika Majimbo.
vi. Nk, nk, nk, .. waweza kuongeza vipengele kadiri ya upeo wako!
My Take:
i. Hili litapunguza muda na gharama za Uelimishaji Umma wakati utakapofika.
ii. Itawezesha wanachama wengi zaidi kuifahamu vema sera ya Chama chao na kuweza kuinadi katika ngazi na nafasi zao.
iii. Itawezesha wanachama wanaotamani kuwania nafasi mbali mbali za Uongozi kuanza kujipanga mapema kwa nafasi za Kitaifa na katika Majimbo.
iv. Nk, nk, nk Waweza kuongeza!
Mtoa mada, naweza ipata wapi hiyo sera ili niisome kwanza niielewe ndio nije nitoe mchango.
Hata kama ni nzuri kiasi gani lazima wananchi tuelimishwe, isije kuwa another sera maslah.
Mikoa mimngine haina hata ulanga sijui itakuwaje.
Jaribu kupekua threads zilizopita hoja hii ishajadiliwa kwa kirefu siku nyingi
Hivi mnadhani hata Chadema ikichukua Dola 2015 itatawala milele? kama kila chama kitakuja na mfumo wake wa ugawaji wa Nchi tutafika kweli?
Hiyo Sera ya majibu ni mzuri lakini ni lazima iwe ni sera inayokubalika na kwamba iingizwe kwenye katiba. kama kweli CDM wanaifagilia hiyo sera basi waifanyie kazi ili iingie kwenye katiba na kuwa mfumo rasmi ambao chama chochote kitachochukua dola hakitaweza kuubadili kirahisi tu. Unatakiwa uwe ni mfumo kama tunaotaka wa kuwa na idadi flani za wizara, mawaziri etc; rais anaechaguliwa anateua tu watendaji na si kupanga pangua ma wizara.
Kama CDM wakichukua dola na kutaka kuuleta huo mfumo wa majimbo nakuhakikishia katiba yote itabidi iandikwe upya kabisa. Maeneo mengi sana yataathirika kuanzia serikali kuu hadi za mitaani, na kubwa kuliko zote Muungano.
Haitokuwa rahisi kivile. Kwa wale mliowahi kufanya project za System changeover mtakubaliana na mimi, kwa mfumo huu wa uchaguzi kila baada ya miaka 5; muda utaisha system itakuwa haijakaa inavyotakikana, wasioitaka hiyo system watapata vya kuongea CDM 2020 itaangushwa atakaeingia nae atataka ku restore old system so it 'll be 10 years za vurugu za kimfumo.
So kimsingi mfumo wa majimbo ni mzuri maana unasaidia sana katika kukuza maendeleo maana serikali kuu itakuwa inakusanya kutoka serikali za majimbo na jimbo lenye kuchangia zaidi ndilo litakuwa na nguvu zaidi kwenye kura za urais wa Serikali kuu. kiuwajibikaji kama serikali kuu itakuwa haiwajibiki then serikali za majimbo zitazuia fund zao mpaka wahusika wawajibike. Utawala wa majimbo kimsingi unapunguza sana nguvu ya serikali kuu na rais kwa ujumla.
Mfano tulionao kwa hapa Tanzania ni Serikali ya zanzibar ndo ingekuwa serikali ya jimbo la Zanzibar, Huku bara napo tunakuwa na Serikali ya Jimbo la kaskazini, jimbo la Mashariki etc.
Tatizo kuu la utawala wa majimbo:
Kwa nchi zetu za kiafrika ni rahisi sana jimbo kujitenga. kwa sababu za kidini au kikabila. kwa hapa TZ kidini zaidi.
Pia sababu za kiuchumi; jimbo likijiona linalea sana majimbo mengine kupitia serikali kuu basi laweza kujitenga na kuwa nchi huru.
Kuna kila haja ya kuinyanyambua hiyo sera kwa undani wake kabla ya kuichukua. vinginevyo itatugharimu.