Sera ya CCM na ACT-Wazalendo ya Ujamaa na Azimio la Arusha na Tabora zinafanana

NJUGHU

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
383
269
Teuzi za kutoka ACT-Wazalendo zimeonekana kuwa ni kuua upinzani lakini ukiangalia kwa umakini ni jambo jema la kuuweka Utanzania mbele zaidi kwa maslahi ya nchi zaidi.

Hili ni jambo jema na kutoa changamoto hasa kwa wanaccm kuamini wao tu ndio wenye kustahili katika ujenzi wa Taifa. Rais ameweka bayana hii ni nchi yetu sote na uongozi utatolewa kwa sifa si kwa ukada.

Katiba na sera za CCM misingi yake mikubwa ni ujamaa na kujitegemea,ambayo msingi wake mkubwa ni Azimio la Arusha. Ukipitia sera za ACT-Wazalendo hasa katika kuamini Azimio la Tabora utaona zinafanana. Hivyo falsafa ya vyama hivi viwili inalandana.

Kwa mantiki hii uteuzi toka ACT-Wazalendo ni rahisi mteuzi kutekeleza sera ya chama kinachotawala.

ACT-Wazalendo imekuwa ikiweka maslahi ya Taifa mbele hasa pale Rais anapofanya jambo jema kwa maslahi ya Taifa si kupinga kila kitu. Kwa vyovyote vile ni rahisi kuteuliwa kuliko toka upinzani mwingine.

Huu ni mwanzo mpya wa kuwa na katiba ya serikali mseto hivyo tumuunge mkono Rais.

Huyu Rais kuna dalili ataunga mkono katiba ya Warioba hebu tuvute subira maana anayoyafanya na kutekeleza yanashabahiana.

Kweli hali ngumu lakini tukumbuke baba akiwa na ujenzi wa nyumba lazima familia mjibane kwa ajili ys kesho.

Watañzania tuungane kwa awamu hii kuijenga Tanzania,na tuweke Uzalendo mbele .

Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom