Sera mpya ya elimu inapatikana wapi na wadau wanaoipitia na kuijadili ni akina nani?

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,296
3,967
Nimesikia tu kuwa kuna sera mpya ya elimu ambayo kwa sasa wanadau wanaipitia.

Swali langu je sera hii inapatikana wapi? Je, kuna forum yoyote inayoijadili?

Au ndio mnaini ninyi mlio serikalini ndio wenye akili pekee kujadili sera hiyo?

Je hamuwezi kuruhusu hata sisi wa kawaida tuulize hata maswali yanayoweza kusaidia mkaboresha maeneo fulani?

Mfano ni kwa nini baadhi ya maarifa ya kawaida kabisa anayoweza kijifunza mtoto wa shule ya msingi, mnafundisha watu wa masters tu?

Mbona elimu yetu kama ya kichawi tu na inalenga kumpotezea mtu muda tu wa kuwa shuleni?

Kuna elimu za diploma zina vitu vingi vya kipumbavu na vitu vya msingi vimeachwa ni kwa nini watu wanaotunga mitaala wasiwe waangalifu kwenye kutengeneza mitaala hii?

Kwanini waziri husika asilete sera hiyo kwenye forum hii tuijadili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…