SEPAH: Iran iko tayari kwavita vya muda mrefu

SEPAH: Iran iko tayari kwavita vya muda mrefu

wrong turn

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
438
Reaction score
170
Naibu Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa
Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH)
ameitahadharisha Marekani akisema Jamhuri
ya Kiislamu imejitayarisha kwa ajili ya vita vya
muda mrefu na kwamba haiogopi kuingia vitani
na Marekani.

Brigedia Jenerali Hussein Salami ambaye
alikuwa akijibu vitisho vya maafisa wa serikali
ya Marekani vya kuishambulia Iran amesema
kipindi cha kutumia mabavu na nguvu za kijeshi
kimepita na kwamba Marekani inafanya makosa
kulinganisha ushindi wake mbele ya majeshi dhaifu
na vita vyovyote na Jamhuri ya Kiislamu. Amesema
vituo vvyote vya nchi kavu vitakavyotumiwa na
Marekani kuishambulia Iran vitachomwa na
kuangamizwa na kwamba anga ya Iran itawaka moto
mbele ya ndege za kivita za Marekani.

Siku chache zilizopita maafisa wa serikali ya Marekani
walikariri tena vitisho vya kuishambulia kijeshi Iran
suala ambalo limekabiliwa na majibu makali kutoka
Tehran.

Source: kiswahili.irib.ir
 
With deep regret !! Vita vitamsaidia nini..... huu ni wakati vita au kutanuwa uchumi, ili wananchi wao waishi maisha bora?
 
sasa kama anachokozwa kwa nini asijibu ulitaka Tehran ikae kimya??
 
Kwa nini iran isiwe na haki ya kuwa na nuclear?
 
Back
Top Bottom