Sentensi 5 tata za Kikwete zilizoleta mshtuko mzito kwa wawania Urais

manizzle

JF-Expert Member
Apr 29, 2015
3,421
4,317
Hizi ni kauli 5 tata alizotitoa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa JMT, je una maoni gani?

1.Chama hakitamvumilia yeyote aliyevunja na anayevunja Kanuni na hakiwezi kujifanya hamna lolote lililotokea.

2. Zama za kuamini kuwa CCM ikipitisha mgombea basi huyo ndio anakuwa Rais zimepitwa na wakati. Wana CCM ni wachache kuliko Watanzania wapiga kura. Hivyo tusichague kwakujidanganya kwa kuwa aidha tunampenda sie au tunamuogopa. Wananchi hawatatuogopa hawatatuchagua.

3. Chama hakitachagua kwa shinikizo la mtu yeyote bali kitasimamia misingi wala hakitamuogopa mtu. Chama kwanza mtu baadae.

4. Chama kinazo taarifa za wagombea Urais, waNEC na wapambe wao wanaofanya mambo ya ajabu na lazima kitachukua hatua.

5. Wananchi wana matarajio makubwa na CCM na hatuko tayari kuwaangusha.
 
Nje hakimwogopi mtu ila ndani hata kumwangalia wanajawa na hofu
 
Kwa kauli hizo 5 za JK, tuhesabu maumivu makali sana kwa yule mtangaza nia aliyejaza uwanja kwa kutumia zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa 'kuwawezsha' wananchi hao wafike uwanjani hapo.

Mwenyewe kwa kile tulichokiona uwanjani hapo anakiita huwezi kuzuia mafuriko kwa mikono.

Lakini nasi wananchi tuna wajibu ws kumuuliza swali alilowahi kuuliza Mwalimu Nyerere.

Hivi hayo mabilioni anayotumia kuisaka Ikulu ameyapata wapi?

Kama ameyakopa atayarudishaje wakati Ikulu hakuna biashara yoyote?

Tunapaswa kwa kuhitimisha kuwa huyo mtu anapaswa kuogopwa zaidi ya UKOMA/UKIMWI.
 
JK hajui kitachokea, Lowasa anajua kile alichofanya na si mjinga kufanya kile alichofanya juzi
 
Mkuu unguturuhusu tuongezee ningeongezea ile ya kuziita fedha ya Tanzania pesa ya madafu,kwangu niliona kama nayo ni kauli tata.
 
Huyu ndiye Rais Dakta,mh,Leutenant,his excellence,comander in chief,Jakaya Mrisho halfan kikwete.
 
Chama Kiliogopa kuwavua watu magamba,Chama kiliogopa kuwashughulikia waliopata uongozi wa Jumuiya kwa RUSHWA,
 
Kwa kauli hizo 5 za JK, tuhesabu maumivu makali sana kwa yule mtangaza nia aliyejaza uwanja kwa kutumia zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa 'kuwawezsha' wananchi hao wafike uwanjani hapo.

Mwenyewe kwa kile tulichokiona uwanjani hapo anakiita huwezi kuzuia mafuriko kwa mikono.

Lakini nasi wananchi tuna wajibu ws kumuuliza swali alilowahi kuuliza Mwalimu Nyerere.

Hivi hayo mabilioni anayotumia kuisaka Ikulu ameyapata wapi?

Kama ameyakopa atayarudishaje wakati Ikulu hakuna biashara yoyote?

Tunapaswa kwa kuhitimisha kuwa huyo mtu anapaswa kuogopwa zaidi ya UKOMA/UKIMWI.
Mkuu hayo maswali yalikuwa na nguvu kabla ya kufuta maadili ya viongozi wa umma.
Azimio la Zanzibar lilifuta azimio la Arusha na Mwl alikuwa bado hai,na katiba pendekezwa watz tumeshuhudia maadili
ya viongozi yakifutwa waziwazi tena kwa mbwembwe nasi tunachekelea.

Nadhani kwa maneno ya m/kiti wa chama hatuwezi kutoa majumuisho
kumbuka sakata la jairo,PM alisema ningekuwa ni mimi nimemweka
ningemwajibisha leo lakini nitampigia simu mkuu kwa maelekezo.
mkuu aliporudi alijitahidi kumuokoa ikashindikana.

Hata katika hili tuwaachie wajumbe wa NEC,ndo wataamua
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom