Sensei Jerome, Willy Ringo kuongoza Karate Tanzania

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
Jerome na Naka Tatsuya Shihan.JPEG
Jerome Sensei (kushoto) akiwa na Naka Tatsuya Shihan kwenye makao makuu ya JKA/WF jijini Tokyo, Japan mwaka 2014
Jerome.JPG

Jerome Sensei akionyesha kwa vitendo namna ya kujihami na kushambulia.


Walimu wa siku nyingi wa karate nchini Tanzania, Willy Ringo Rwezaura Sensei na Jerome George Mhagama Sensei, leo wamechaguliwa kuongoza Karate katika chama cha Tanzania Shotokan Karate (Tashoka), uchaguzi uliofanyika kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Willy Ringo Sensei amerejea tena kwenye nafasi ya uenyekiti wa chama hicho baada ya kumshinda mpinzani wake wa karibu Yahaya Mgeni Sensei.

Ringo Sensei ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha West Coast Shotokan Karate (WCSKA), alijitoa kwenye uongozi wa chama hicho tangu mwaka 2008, lakini sasa ameamua kurejea tena.

Aliyechaguliwa kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Kambi Sensei, ambaye alikosa mpinzani kwenye nafasi hiyo.

Jerome Mhagama Sensei (5th dan black belt), alichaguliwa kwa kura 60 kushika nafasi ya Katibu Mkuu akimbwaga mpinzani wake aliyeambulia kura mbili huku kura tatu zikiharibika.

Jerome Sensei (35), ambaye ni mkufunzi mkuu wa Japan Karate Association/World Federation tawi la Tanzania (JKA/WF-Tanzania) ni miongoni mwa wacheza karate mahiri kabisa nchini Tanzania ambaye siyo tu kwamba anajulikana kimataifa, bali ameweka rekodi nyingi katika mchezo huo kiasi cha kutambuliwa na Wajapani wenyewe.

Miaka minne iliyopita aliweka rekodi ya kuwa mwalimu mdogo kabisa katika historia ya JKA/WF kutunukiwa cheti cha ukufunzi pamoja na uamuzi wakati aliposhiriki semina na mashindano kwenye makao makuu cha chama hicho jijini Tokyo, Japan.

Aidha, mwaka 2014 aliweka rekodi nyingi kwa kuwa mwalimu mdogo zaidi kuwa mwamuzi katika mashindano ya dunia yaliyofanyika pia Tokyo, Japan.

Kutokana na hali hiyo, kuna kila dalili kwamba uongozi mpya unaohusisha wakongwe na vijana, utaleta mabadiliko na maendeleo ya mchezo huo wa kujihami nchini Tanzania.
 
Back
Top Bottom